Fanyeni kazi kwa mashirikiano

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amwewataka Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya kazi kwa mashirikiano ili kujenga Jumuiya yenye nguvu Barani Afrika.

Maalim Seif amesema hayo leo ofisini kwake Migombani, alipokuwa na mazungumzo na Mawaziri wa nchi wanachama pamoja na watendaji wakuu wa taasisi zilizomo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliofika kumtembelea baada ya kumaliza kikao cha siku mbili cha Itifaki ya Utawala Bora katika Jumuiya hiyo, kilichofanyika katika hoteli ya ‘Diamond Dream of Zanzibar’.

Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi wa Jumuiya hiyo kufanyakazi kwa mashirikiano, ili kuipa nguvu Jumuiya iweze kukabiliana na changamoto mbali mbali ziliozopo pamoja na kuwaunganisha wananchi wake ambao wana uhusiano wa kindugu kwa muda mrefu.

Alikitaka chombo hicho kitumike ipasavyo kama kiungo muhimu cha kuziunganisha nchi wanachama kwa faida ya nchi hizo na watu wake.Katika hatua nyengine Makamu wa kwanza wa Rais alitumia fursa hiyo kuwaeleza viongozi hao mafanikio ya Serikali ya Zanzibar ilio chini ya mfumo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa.

Alisema kuja kwa mfumo huo umeifanya Zanzibar kupata mafanikio makubwa, huku nchi ikiendeshwa kwa amani na mashirikiano na kuondokana kabisa na mifarakano iliodumu kwa kipindi kirefu.

Alisema mfumo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa, umetoa fursa kwa vyama vyote vyenye uwakilishi, kufanyakazi kwa pamoja na kurejesha mshikamano wa Wazanzibari uliopotea pamoja na kuondoa uhasama.Aliwahakikishia viongozi hao kuwa, mbali na kutokuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani katika Baraza la Wawakilishi,ushindani ndani ya Baraza hilo umeongezeka ambapo kila mjumbe (bila ya kuzingatia chama atokacho),hupata fuirsa ya kuikosoa Serikali, hali inayolifanya Baraza hilo kuongeza msisimko wakati wa kujadili mijadala na miswada mbali mbali inayowasilishwa.

Nae Beatrice Kiraso, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya viongozi hao, aliipongeza Serikali ya Zanzibar kwa kupanua wigo wa demokrasia na kupata suluhisho la kisiasa bila ya kutafuta msaada toka nje, hatua aliyosema imelisafisha jina la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s