Ali Mzee ateuliwa

Ali Mzee Ali ameteuliwa kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amemteuwa Ali Mzee Ali kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi kupitia nafasi kumi za rais kwa mujibu wa katiba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu kiongozi dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu 66 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa rais kikatiba, Rais anazo nafasi kumi za kuteuwa wajumbe watakaoingia katika baraza la wawakilishi, ambapo kwa sasa rais amezitumia nafasi hizo tisa na kubakiwa na nafasi mmoja tu pekee.

Mzee alikuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi katika kipindi kilichopita ambapo pia aliongoza kamati ya baraza la wawakilishi ya watu sita ya kusimami maridhiano ya kisiasa na kura ya maoni ambayo hatimae imekuja kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hapa zanzibar.

Katika uteuzi huo Dk Sheni amemteuwa Abrahman Mwinyi Jumbe kuwa mwenyekiti wa bodi ya Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), wakati Ali Abdallah Suleiman anakuwa mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa barabara, badala ya aliyekuwa ameshikilia nafasi hiyo Masauni Yussuf Masauni kuwekwa pambeni.

Kabla ya uteuzi huo Suleiman alipata kuwa katibu mkuu ofisi ya waziri kiongozi katika miaka ya 1995.

Aidha katika uteuzi huo Abdulnassir Ahmed Mohamed Abdulrahman ameteuliwa kuwa mkurugenzi mwendeshaji wa shirika la bima la Zanzibar (ZIC), huku Salum Khamis Nassor akiteuliwa kuendelea na wadhifa wake wa mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya kukuza vitega uchumi (ZIPA).

Katika uteuzi huo Mohammed Hafidh Rajab anakuwa mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo anaendelea na wadhifa huo katika kipindi chengine.

Advertisements

2 responses to “Ali Mzee ateuliwa

  1. Ewe mzanzibar kwa kutumia mtandao kama vile facebook, marafiki, badoo, twiter n’k tuma sms zinazohamasisha wazanzibar kudai UHURU kutoka mikononi mwa MAKAFIRI WA TANGANYIKA.

  2. EWE MZANZIBAR KWA KUTUMIA NJIA ZA MITANDAO ELIMISHA NA ONESHA ATHARI ZA TRA NA VIONGOZI WA SMZ WALIOINGIA MADARAKANI KWA WIZI WA KURA KUTOKANA NA KUPATA MSAADA KUTOKA TANGANYIKA ILI KUIMALIZA NA KUIDIDIMIZA ZANZIBAR KIUCHUMI.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s