Afrika Mashariki na utawala bora

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Naibu Katibu Mkuu wa EAC, Beatrice Kiraso wakizungumza muda mfupi baada ya Balozi Seif kufungua mkutano wa kuangalia itifaki ya utawala bora katika nchi za Afrika Mashariki katika mkutano uliowashirikisha mawaziri na watendaji wakuu wa suala la utawala bora katika Hoteli ya Dreams of Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja

KATIKA kujenga ushirikiano madhubuti katika nchi za Afrika Mashariki, viongozi katika jumuia hiyo wamebaini kuwa itakuwa ni ndoto kwa nchi za jumuia ya Afrika Mashariki kufikia malengo ya kimaendeleo ya uchumi na kijamii bila kuimarisha utawala bora.

Hayo yamebainika katika mkutano wa siku mbili wa kuangalia itifaki ya utawala katika nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Hoteli ya Dreams iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akifungua mkutano wa kwanza wa mawaziri wanaoshughulikia utawala bora kutoka nchi zinazounda jumuia hiyo, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alitamka wazi kuwa utawala bora ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya jumuia hiyo.

Jumuia ya Afrika mashariki imekuwa ikimarisha ushirikiano wa kiuchumi, uhuru wa kibiashara, ajira, sarafu, na baadae kisiasa ambapo jumuia hiyo inalenga kuwa na rais mmoja.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo unaowashirikisha mawaziri wa utawala bora, na watendaji wengine wanaohusiana na utawala bora, sheria, na haki za binaadam kutoka nchi za Rwanda, Kenya, Uganda, Burundi, na wenyeji Tanzania na zanzibar, balozi seif Iddi alisema tafsiri ya mataifa yanakubaliana juu ya kuimarisha utawala bora lakini tafsiri ya utawala bora imekuwa katika mtizamo tofauti.

Alisema miongoni mwa kazi kubwa zinazolikabili bara la Afrika ni kujenga mfumo wa kuendeleza misingi ya utawala bora ambapo mfumo huo ulianza kujengwa baada ya mataifa mengi kupata uhuru wa kisiasa katika miaka ya 1960, na kwamba kinachotakiwa ni kuuendeleza kwa kuzingatia mazingira ya sasa barani humo.

Balozi Seif alisema ujenzi wa misingi ya utawala bora uliofanyika baada ya uhuru wa kisiasa na ilikuwa ni hatua ya kuendeleza uliokuwepo kabla ya bara la Afrika kuwa chini ya utawala wa wageni kwa wakati huo.

Balozi Seif alisema ni makosa kwa bara la Afrika kuwa na mawazo kwamba ukosefu wa mfumo wa utawala bora ndio kipimo maendeleo na demokrasia katika nchi zake.

Aidha Makamu huyo wa pili alisema matumaini yake makubwa kwamba dhana ya itifaki ya ushirikiano huo itakuwa na manufaa kwa sababu imeandaliwa kwa kuzingatia mazingira ya sasa ya kundi la nchi zinazounda EAC kutokana na mawazo ya wadau wenyewe na sio utashi wa nchi moja.

Makamo wa pili wa rais aliwataka viongozi wanaohudhuria mkutano huo mjini Zanzibar kujadili rasimu ya kuimarisha utawala bora kwa kuangalia mazingira ya nchi wanachama na maslahi ya wananchi wote.

Pembezoni mwa mkutano huo Balozi seif Iddi pia alitamka kuwa nchi mpya ya Sudan ya Kusini ambayo imepata uhuru wa kujitawala inaweza kukubalika kujiunga na Jumuia ya afrika mashariki iwapo itakuwa na sifa na kutimiza mashariki yaliyowekwa huku Tanzania ikiwa imejifunza kwamba sio vyema nchi moja kuimeza nchi nyengine.

Naibu Katibu Mkuu wa EAC, Beatrice Kiraso alisema utawala bora, ni hatua muhimu kwa maendeleo duniani na kuwahimiza nchi wanachama kutekeleza dhana hiyo.

Alisema maandalizi ya rasimu ya itifaki ya ushirikiano huo yamefanyika kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali, zikiwemo taasisi za kuzuia rushwa, haki za binadamu, kamati za mabunge, tume za uchaguzi, taasisi za kiraia na Jukwaa la Majaji Wakuu wa EAC.

Beatrice alisema kuwa katika miaka iliyopita ilikuwa vigumu kuzungumzia utawala bora na haki za binadamu kutokana na kukosekana demokrasia katika nchi nyingi za kiafrika, lakini hivi sasa ni vigumu kujificha kutokana na kupanuka na uhuru wa habari, na shindikizo za ndani na nje kutaka utawala bora.

Mkutano huo uliowashirikisha wajumbe 60 unajadili rasimu ya ushirikiano na utawala bora, na baadae makubaliano ya mawaziri hao yatawasilishwa kwa marais kutoka jumuia ya afrika mashariki watakapokutana baadae Novemba mwaka huu.Maeneo yanayojadiliwa ni kuimarisha utawala bora, uwajibikaji, haki za binaadamu, uwazi, na usawa wa Jinsia.

Advertisements

One response to “Afrika Mashariki na utawala bora

  1. UKISEMANA TANZANIA HUMANISHA NN MUADISHIOSKAAM AILAGNYA A KUJITIA VITANZI ALIVYOSEMA JUSSA TUMEKWISHAAAAAK WA EAC

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s