Face to face Seif na Bilali

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa leo Julai 04, 2011.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wajasiriamali nchini kupanua wigo wa kujitangaza ili kuvutia biashara zao katika masoko ndani an nje ya nchi.

Maalim Seif amesema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati alipotembelea Maonyesho ya 35 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya saba saba jijini.

Amesema ni umuhimu kwa wajasiariamali hao kutangaza biashara zao katika masoko ya ndani pamoja na nchi jirani ili bidhaa wanazozalisha iwe kiungo muhimu cha kufanikisha malengo ya kujikimu kimaisha.

Alisema itakuwa sio jambo sahihi kwao kufanya juhudi katika uzalishaji wa bidhaa mbali mbali huku wakitegemea soko la ndani pekee ambalo linaonekana kutokukidhi haja, na kuziacha bidhaa zikibaki na kukosa wateja wa kuzinunua.

Aidha aliwataka wajasiriamali hao kuboresha zaidi bidhaa wanazozalisha ili zifikie viwango vya kimataifa, hatua itakayowezesha kukabiliana na changamoto ya ushindani katika masoko.

Maalim Seif ambae katika ziara hiyo alipata nafasi ya kutembelea mabanda mbali mbali zikiwemo taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki na mikopo kwa wajasiariamali, alitumia fursa hiyo kuzipongeza taasisi hizo kwa hatua kubwa zilizofikia,  ikizingatiwa kuwa zinaendeshwa kiufanisi na Watanzania wenyewe.

Aidha alizipongeza taasisi za kiufundi kama vile VETA kwa kuwa na ubunifu mkubwa katika utengenezaji wa vifaa mbali mbali vya kijamii na zana za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi.

Aliwataka watendaji wa taasisi hilo kujizatiti na kutengeneza vifaaa vilivyo bora zaidi ili hatimae viweze kuwapatia ajira na kuondokana na dhana potofu kuwa ajira ni ile tu itolewayo na Serikali.

Katika ziara hiyo Maalim Seif alitembelea mabanda kadhaa, ikiwemo Wizara ya Fedha na taasisi zake, Banda la ‘Karume Hall’ linalojumuisha wafanyabiashara wa Kichina, Afri Tea &Coffee Ltd, Uhamiaji na Kenya, pamoja na Taasisi ya VETA inayoshughulikia zaidi masuala ya kiufundi.

Mabanda mengine aliyoyatembelea ni pamoja an Farm Equipemnt,CRDB, Baraza la Uwezeshaji wa Taifa linalojumuisha mkusanyiko wa taasisi mbali mbali, pamoja an Baraza la Uwezeshaji la taifa lililo chini ya Mwenyekiti wake Mama Anna Mkapa.

Mengine ni JKT, EPZ, GF Trucks and Equipments, Spray and Fumigation Service, Zanzibar Investment Promotion Authority pamoja na Shirika la Bima la Taifa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s