Ahsante kwa zawadi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Juhan Toivonen , wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Julai 04, 2011 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini

Balozi Juhan Toivonen kutoka Finland aliisifia Tanzania na kumzawadia Makamu wa Rais Kitabu cha “The Great Savanna” kitabu kilicho na vivutio kadhaa vya utalii nchini Tanzania ambacho kilichapishwa kwa Kifini na kisha kutafriwa kwa Kiingereza. Balozi huyo alimuahidi kutoa kopi nyingine za kitabu hicho zipatazo 9,000 kwa Makamu wa Rais ili zisambazwe kwa wadau wa utalii nchini.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Anuani ya Simu: “MAKAMU” Ofisi ya Makamu wa Rais,
Simu Na.: 2116919 S.L.P. 5380,
Fax Na: 2116990 Dar es Salaam,
Tovuti: http://www.vpo.go.tz Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MABALOZI WA FINLAND NA GERMANY WAMUAGA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL IKULU LEO JUMATATU JULAI 04, 2011

Mabalozi wa nchi za Finland na Ujerumani leo wamefanya ziara katika ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga huku kwa pamoja wakielezea kubakia na kumbukumbu ya namna Watanzania wanavyoishi na walivyowathamini wakati wakifanya kazi za kidiplomasia hapa nchini.

Wa kwanza kufika ofisini kwa Makamu wa Rais alikuwa Balozi Juhan Toivonen kutoka Finland ambaye aliisifia Tanzania na kumzawadia Makamu wa Rais Kitabu cha “The Great Savanna” kitabu kilicho na vivutio kadhaa vya utalii nchini Tanzania ambacho kilichapishwa kwa Kifini na kisha kutafriwa kwa Kiingereza. Balozi huyo alimuahidi kutoa kopi nyingine za kitabu hicho zipatazo 9,000 kwa Makamu wa Rais ili zisambazwe kwa wadau wa utalii nchini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais licha ya kumshukuru Balozi Toivonen, alifafanua kuwa uhusiano wa Finland na Tanzania ni wa siku nyingi na wenye tija nchini na kwamba historia inaonyesha kuwa katika fani ya Jiolojia, nchi ya Finland imesaidia sana katika kutanua rasilimali watu hapa nchini.

Katika hatua nyingine Balozi huyo alitaka kujua namna Tanzania inavyomudu kutanua demokrasia kulinganisha na mataifa mengine ya Afrika na Makamu wa Rais akamjibu kuwa, hali hii inatokana na mahusiano chanya kati ya serikali na wananchi na akatilia mkazo juu ya uongozi uliotukuka wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere hasa katika vigezo vya kujenga ushirikiano na hali ya kukubaliana kama Watanzania.

Katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani Dkt. Guido Herz, Balozi huyo aliyekaa nchini kwa miaka mitatu yeye alianza kusifia makubaliano ya kupatikana amani ya kudumu Visiwani Zanzibar huku akifafanua kuwa namna alivyoona tatizo lililokuwepo, alikuwa akiamini kuwa lingetatuliwa na Wananchi wenyewe. Balozi huyo alifafanua pia kuwa anaamini demokrasia inakuwa nchini na pia akaeleza kuwa siasa za Tanzania bado zina mizizi ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Makamu wa Rais alimuelezea Balozi huyo namna Tanzania ilivyojipanga katika sekta ya Utalii huku ikiwaza kuwa na utalii wenye tija lakini usiokuwa na idadi ya watalii wanaofurika na hivyo kuharibu mazingira. Suala lingine lililojadiliwa lilikuwa juu ya uchimbaji wa madini ya Uranium huku Makamu wa Rais akifafanua kuwa, kazi hiyo itafanywa kwa uwazi kabisa na tayari hatua za awali za kujitathmini kabla ya kuanza kazi hiyo zimeanza zikiwa chini ya wizara zinazohusika na Madini sambamba na Sayansi na Teknolojia.

Imetolewa na: Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s