Mkurugenzi wa Manispaa awajibishwe

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, Rashid Ali Juma katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) ofisini kwao Wekesi Kikwajuni siku chache baada ya matatizo yaliojitokeza kati ya Baraza la Manispaa na wafanyabiashara wa maduka ya Makontena Darajani ambapo maduka yote alifungwa kutokana na amri ya baraza hilo.

MKURUGENZI MANISPAA AWAJIBISHWE

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameliweka “kiti moto” Baraza la Manispaa Zanzibar kwa kutaka Mkurugenzi wake awajibishwe kwa kwa kuikosesha serikali mapato ya mamilioni ya fedha.

Wakijadili makadirio ya bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) kwa mwaka huu wa fedha wa 2011-2012, wajumbe hao walisema manispaa hiyo inaikosesha serikali mapato kwa kuingia katika mikataba yenye lengo la kuwanufaisha watu binafsi.

Mwakilishi wa Kiwani (CUF), Hijja Hassan Hijja, alisema mikataba hiyo inahusu ukodishaji wa Bustani ya Jamhuri kwa kwa gharama ya shilingi milioni moja kwa mwezi, lakini baada ya kulipwa fedha hizo, shilingi 900,000 kati ya hizo zinazirudisha kwa mkodishaji ikiwa ni gharama ya matunzo ya bustani

Alikiambia kikao cha baraza hilo kinachoendelea Chukwani Mjini hapa kuwa
mkataba wa ukodishaji bustani hiyo huo ni wa muda mrefu, lakini kutokana utekelezaji wake haoni kama utainufaisha serikali kimapato.

“Kila mkodishaji anapolipa shilingi milioni moja, kati ya hizo shilingi 900,000 zinarudi kwa mkodishaji kwa maelezo kuwa ni za kugharamia matunzo ya bustani, hapa pana harufu ya rushwa mheshimiwa Spika tunahitaji maelezo sahihi katika hili” alisema Hijja.

Mbali na kuikosesha serikali mapato, Hijja alisema uamuzi wa manispaa hiyo kufunga maduka 84 ya wafanyabiashara wa Darajani, kilikosesha pia serikali mamilioni ya fedha kitendo ambacho kinapaswa kuangalia kwa undani zaidi.

Alisema maduka analipa kodi kutokana na maduka hayo inaingiza serikali kiasi cha shilingi milioni 760 kila mwaka kutokana na kodi ya kila mwenye duka kwa mwaka.

Hijja alisema katika kipindi cha miezi sita kinachoishia mapema mwaka huu, maduka hayo yalifungwa kwa amri ya manispaa na kwamba hatua hiyo ilisababisha serikali kupoteza mamilioni ya fedha kwa kukosa mapato hayo.

“Maduka hayo yalifungwa kwa miezi sita kwa amri ya manispaa, serikali imepoteza mamilioni ya shilingi lakini mara mahakama inasema maduka yafunguliwe sasa hapa lazima tuwe makini katika masuala haya ya mapato kuna vitu vinafanyika huku baraza la manispaa hayaeleweki ni watu wachache wanatumia madaraka vibaya ” alisema Mwakilishi huyo ambaye yupo barazani kipindi cha pili

Alisema mkataba wa ukodishaji wa Bustani ya Jamhuri na kufungwa kwa maduka katika eneo la Darajani kumesababisha mgogoro mkubwa kati ya serikali na wafanyabiashara jambo ambalo serikali ilitakiwa kulingalia suala hilo kabla ya kuamua maamuzi ambayo hayana tija kwa wananchi wake na kusababisha wanachi kuichukia serikali yao kutokana na mamuzi ya watu wachache wenye kutumia vyeo vibaya kinyume na dhana ya uwajibikaji na utaala bora.

Alisema hatua ya kufunga maduka hayo ilitolewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa misingi ya mbaguzi na kusababisha chuki kubwa miongoni mwa watendaji wa manispaa na wananchi.

“Mkurugenzi wa manispaa ni mbaguzi, kwa muda mrefu sasa analalamikiwa kwa tabia hiyo, lakini bado anaendelea kulindwa,” alisema Hijja na kuongeza kuwa “kama mnampenda mchukueni akafanye kazi Ikulu.”

Kauli ya Mwakilishi huyo iliungwa mkon wa takriban wajumbe wengi ambao wamesema kuna tatizo kubwa ambao serikal imeshindwa kuchukua dhidi ya Mkurugenzi ambaye anaonekana kwamba utendaji wake una mshaka makubwa kiutendaji huku shutuma nyingi za rushwa zikielkezwa kwake kutokana na mikataba ya makampuni ya simu za mkononi.

Akichangia bajeti hiyo Makilishi wa Kikwajuni (CCM) Mohmoud Mohammed Mussa alisema kufunga maduka ya Darajani ni sawa na kusamehe mapato ya shilingi million 760 zinazokusanywa na serikali kutoka kwa wafanyabiashara wa eneo hilo kwa mwaka.

Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alihoji wingi wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya baraza la manispaa wakati baraza hilo makusanyo yake anatosheleza bila ya kupewa fedha serikalini.

“Baraza la Manispaa linapewa ruzuku ya shilingi 1094 millioni kutoka katika mfuko wa serikali makusanyo yake ni 1041 millioni sasa kwa nini wapewe ruzuku wakati fedha wanazokusanya zinatosheleza katika kujiendesha” alihoji Jussa.

Jussa alisema mvujaji wa mapato unaofanywa na baraza la Manispaa hauwezi kufuta dhamira ya utendaji kazi wa serikali katika baraza hilo kwa kuwa wananchi wa Zanzibar wamepoteza imani ya baraza hilo hata kama kuna mipango mizuri ya kuimarisha utendaji kazi.

“Mheshimiwa Spika baraza hili tulitaka iiundwe tume kuchunguza tuhuma zinazotuhumiwa baraza la manispaa ikiwemo mikataba ya simu za mkononi na harufu ya rushwa lakini serikali ilikataa lakini leo tunashuhudia ripoti iliyotolewa ambayo moja kwa moja inaonesha kuna rushwa katika baraza hili, lakini waziri unatwambia kuwa baraza limetayarisha mipango mizuri” alisema na kuongeza kwamba.

“Kitendo kilichofanyika huko nyuma hakiwezi kufunikwa na hiyo mipango mizuri maana hakifunikiki, wananchi wamepoteza imani na baraza hili wasafishwe ndio wananchi wataunga mkono hiyo mipango mizuri” alisema Jussa na kuungwa mkono na wajumbe wenzake.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni (CUF) Subeit Khams Faki alisema manispaa inakabiliwa na tatizo la ubadhirifu kwa miaka mingi sasa, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na serikali

“Ubadhirifu upo manispaa, wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote, kuna tatizo gani tunashindwa kumwajibisha mtu anayeshindwa kuwajibika?,” alihoji Subeit.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Zanzibar, Rashid Ali Juma anatuhumiwa kwa kuitumbukiza serikali katika mkataba wenye utata na makampuni mawili ya simu za mkononi ambapo katika ripoti hiyo imemhusisha moja kwa moja Mkurugenzi huyo.

Wakati hayo yakitendekea kujadiliwa ndani ya baraza la wawakilishi huku nje tayari madiwani katika ripoti yao walitoa mapendekezo na kuitaka serikali imuondoshe Mkurugenzi huyo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuingia mikataba kinyume na sheria, kutumia madaraka yake vibaya na kuacha mji wa zanzibar kuwa katika hali.

Advertisements

2 responses to “Mkurugenzi wa Manispaa awajibishwe

  1. kama serikali itamwacha mkurugenzi huyu hapo manispaa basi mradi wote wa ZUSP hautofanikiwa kwani kwa yeye ameapa kufanya shughuli zake kama kawaida bila ya kujali kanuni wala sheria za baraza la manispaa,nao madiwani kwa upande wao wana sema hawatokwenda Barazani ila kwa mkurugenzi mpya,kwa kweli hali ni mbaya kuliko maaelezo.

  2. sasa huyu anoweza kuiyumbisha serikali na wananchi nama hii ni mkurugenzi tuu au ni rais kabisa, mbona ana cheo kidogo ila maudhi yake ni makubwa? tuseme juu yake yupo katibu mkuu, naibu waziri, waziri mwenyewe , hao wote wamemzidi cheo, tuseme hao pia hawaoni, hayo mabaya anayofanya? au wanamuogopa? sote hatupo makini kuitetea nchi, tutasema midomoni tu, ila nyoyoni bado. tunahitaji kuelimishwa zaidi jinsi ya kuipenda nchi yetu, zanzibar ni nzuri kuanzia jina hadi watu, ila tunatakiwa, kila mzanzibari awe anaipenda nchi kwa moyoni, au kwa dhati, kuanzia raisi hadi mwanafunzi, hapo tutafika,maoni yangu, tunao wasomi wengi tu, muondoweni huyo muekeni mchapakazi, tuwe wakweli, rushwa sio nzuri jamaniiiii.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s