Jitangazeni nje kiutalii

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akipokea kabrasha ya mpango mkakati la maendeleo ya Utalii Zanzibar kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Issa Ahmed Othman ofisini kwake Migombani

Abdi Shamnah

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, kupanua wigo wa kujitangaza ili kuimarisha soko la Utalii nchini.

Amesema hayo leo ofisini kwake Migombani, wakati alipozungumza na ujumbe wa Bodi hiyo, uliofika kwa ajili ya kujitambulisha.Ameitaka Bodi hiyo kufanya juhudi kubwa za kuitangaza Zanzibar kiutalii ili kuvutia soko lake ambalo alisema limejaa vivutio kadhaa an kutoa wito wa kuviendeleza vivutio hivyo.

Alisema moja ya njia muhimu ya kuitangaza ni pamoja na kushiriki katika matamasha mbali mbali yanayofanyika kila mwaka Duniani kote, ambako Makampuni na wadau wa sekta hiyo hukutana na kuonyesha vivutio vya nchi wanazotoka.

Alisema katika kuimarisha soko hilo, Serikali inalenga kuwa an Wawekezaji makini watakaowekeza katika ujenzi wa hoteli zenye hadhi kubwa ya nyota tano pamoja na kuwa na kumbi za mikutano ili kuvutia watalii, pamoja na kutoa fursa ya kufanyika kwa mikutano ya kimataifa.

Akizungumzia mafanikio ya sekta hiyo, Maalim Seif alipongeza juhudi zinazochukuliwa na Kamisheni hiyo pamoja an wadau nchini, hali iliopelekea kuwepo ongezeko la uingiaji wa watalii na kutaka jitihada zaidi zichukuliwe kuongeza idadi hiyo, kwa kuzingatia nafasi nzuri iliyonayo Zanzibar kama zilivyo nchi nyingine za Visiwa ikiwemo Maldvies.

Alisema ongezeko hilo limeweza kuimarisha shughuli za utoaji huduma muhimu, ambapo wananchi hupata fursa za kuuza mazao yao mbali mbali katika mahoteli.Alipongeza hali ya upatikanaji wa ajira kupitia sekta hiyo, inayokadiriwa kufikia nafasi 20,000 (kwa ajira rasmi) na 45,000 kwa ajira zisizo rasmi kwa mwaka, na kusema hali hiyo inatia moyo sana.

Aidha alionya juu ya matukio mabaya yanayoikabili dunia wakati huu, hususan katika nchi za Kiarabu na kusema kuwa moja ya vyanzo vya matatizo yake yanatokana na vijana kukosa ajira, baada ya kumaliza masomo yao.Hata hivyo, alishangazwa na taarifa za kuwepo tatizo la takwimu (idadi halisi) ya watalii wanaoingia nchini, ikizingatiwa kuwa kuna milango miwili tu ya Uwanja wa Ndege na Bandari, inayotumika rasmi kwa safari zao.

Aliitaka Bodi hiyo kushirikiana na wadau wa sekta hiyo, katika kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazokabili, ikiwemo Idara ya Uhamiaji yenye jukumu la kurikodi taarifa za kuingia na kutoka kwa wageni wote nchini.

Akigusia uharibifu wa mazingira unaotokana na maendeleo kiutalii na maeneo ya kitalii, Maalim Seif alisema, suala la uhifadhi wa mazingira (ambalo liko chini ya Ofisi yake), lina umuhimu mkubwa na kulitahadharisha Taifa kuwa lisipokuwa makini katika uwekezaji, litajikuta mazingira yake kuwepo hatarini.

Alisema eneo la Maruhubi (Maruhubi Ruins),likiwa moja ya eneo lenye uharibifu mkubwa wa mazingira na kutia doa shughuli za kiutalii, hivi sasa linashughulikiwa kwa kufukia mashimo kwa taka, ili hatimae mashimo hayo yafukiwe kwa mchanga.

Alieleza kuwa sehemu hiyo inaingia katika mpango wa Serikali wa ujenzi wa Bandari ya Mizigo kutoka eneo la Mpigaduri. Alipongeza hatua ya baadhi ya wawekezaji kisiwani Pemba ya kujenga Hoteli za kitalii bila ya kukata miti, hatua aliyosema ni matumizi mazuri ya uhifadhi wa ardhi ndogo iliopo.

Katika hatua nyingine, Maalim Seif alitumia fursa hiyo kuukosoa mfumo wa Kamisheni hiyo uliopo, na kusema ni vigumu kujiendesha kama Idara, akiainisha umuhimu wa kujitegemea kwa kuwa na mfuko wake ili kuendeleza shughuli zake.

Mapema Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Issa Ahmeid Othman alisema moja ya changamoto kubwa inayoikabili Bodi hiyo wakati huu ni juu ya uimarishaji wa soko lake, hali inayotokana na sababu mbali mbali ikiwemo mashirikiano duni na baadhi ya wadau wa sekta hiyo.

Alisema mbali na kuwepo mafanikio katika ujio wa watalii nchini,suala la uharibifu wa mazingira katika baadhi ya maeneo (ikiwemo Maruhubi) nalo limekuwa changamoto kubwa inayowafanya wageni kuacha ujumbe mbaya mara wanapoondoka.

Aidha alisema urasimu kutoka katika baadhi ya taasisi za Serikali, imekuwa kikwazo kwa Bodi hiyo kuwa mfuko wake wa kujiendesha.Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni ya Utalii nchini, inafanyakazi chini ya sheria namba 6 iliorekebishwa mwaka 2009.

Advertisements

One response to “Jitangazeni nje kiutalii

  1. Nawaomba viongozi wa zanzibar washirikiane ane office yetu ya wazanzibari Zawa hapa uk,wafungue television hapa uk,ili iwe njia rahisi ya kuitanga zanzibar,television kuingiza katika SKY ili iweze kusambaa duniani kote,au wazo jengine watoe vipindi vya utalii kama ni history ya zanzibar,matanganzo ya biashara,kuna television hapa uk tunaweza kuyapeleka na kuyalipia.

    Lakini kitu kizuri zaidi ni kufungua television ya zanzibar,nafikiri itakuwa njia moja zanzibar kujikwamua kiuchumi na kutambulika kimataifa,na kuongezeka utalii.
    Jengine tumekuwa tukiona matangazo ya tanzania bara ,wanamuziki,mahotel,na taasisi nyengine hapa katika mtandandao wa facebook,tunawashauri wahusika wa utalii zanzibar waangalie hilo,facebook ni mtandano ubebeba asilimia kubwa ya watu,ni njia moja nzuri ya kujitangaza na sisi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s