Watakaoichezea SUK kukiona

Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja aliuliza swali a msingi katika kikao cha baraza la wawakilishi akitaka kujua hatua gani zitachukuliwa kwa viongozi wanaoongoza kwa utashi wa kisiasa kinyume na nia na malengo ya serikali ya umoja wa kitaifa.

SERIKALI ya mapinduzi ya Zanzibar imesema kwamba itawachukuliya hatua za kinidhamu watendaji na viongozi wa serikali ambao wataongoza nchi kwa kuweka mbele utashi wa kisiasa kinyume na dhamira na malengo ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Hayo yalisemwa na waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohamed Aboud Mohamed wakati akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja aliyetaka kujuwa hatua gani zitachukuliwa kwa viongozi wanaoongoza kwa utashi wa kisiasa kinyume na nia na malengo ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Aboud alisema lengo la serikali ya umoja wa kitaifa ni kuondosha siasa za chuki na uhasama wa kutoaminiana na kujenga nchi yenye umoja na utulivu maelewano na mshikamano wa wananchi wote bila ya kujali jinsia zao, dini zao, au maeneo wanapotoka kama ilivyo sasa.

“Mheshimiwa sote ni mashahidi sasa serikali ya umoja wa kitaifa tuliyonayo kwa sasa ndiyo suluhisho la matatizo ya kisiasa. Dhamira ya serikali hii ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote, serikali haitamvumilia kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali ambaye atafanya kazi kinyume na dhamira hiyo. Nataka niwahakikishie wananchi wote kwamba serikali yao inawatumikia wananchi wote kwa misingi ya usaa na haki” alisema Aboud.

Alisema dira ya serikali ya umoja wa kitaifa ni kuleta maendeleo ya haraka kwa faida ya wananchi wote wa nchi hii na ni msingi mkuu na falsafa ya serikali ya mapinduzi yenye muundo wa umoja wa kitaifa.

“Mfumo huu wa serikali ndio uliokubaliwa na wananchi wengi kupitia kura ya maoni iliyofanyika 2010 na kwa mnasaba huo na kwa kuangalia hali tulionayo hivi sasa ya maelewano na mashirikiano makubwa miongoni mwa wananchi na serikali yao hivyo ni dhahiri serikali ya Zanzibar inayachukulia kwa uzito mkubwa maneno ya rais Jakaya Kikwete kuwa mafanikio ya kweli yanayokana na serikali na wananchi kuwa na umoja, uwazi na mshkamano” alisema Aboud.

Aboud alisema kwa kiasi kikubwa inaonesha kwamba wananchi walikuwa wanataka kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kama ilivyoonesha katika kura ya maoni iliyopigwa mwaka jana ambapo wananchi walipiga kura na kutaka serikali ya umoja wa kitaifa.

Akifafanua zaidi Aboud alisema serikali haitosita kuwachukuliya hatua za kinidhamu watendaji wote watakaoonekana kuendesha shunguli za kiserikali kwa utashi wa kisiasa.

Aidha alisema wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya wote wanatakiwa kuongoza sehemu zao za kazi kwa kufuata sheria ziliopo na sio utashi wa kisiasa na kiongozi atakayefanya hivyo atafukuzwa kazi.

“Wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya wote wanatakiwa kuendesha shunguli za kazi kwa kufuata misingi na sheria ziliopo sio utashi wa kisiasa na viongozi watakaofanya hivyo watafukuzwa kazi” alisema Aboud.

Aboud alikuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Micheweni (CUF) Subeit Khamis Faki nae aliyetaka kujuwa wakuu wa mikoa na wilaya watakaoleta utashi wa kisiasa katika majukumu yao watachukuliwa hatua gani.

Wazanzibar mwaka jana walipiga kura na kuamuwa kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa,ikiwa moja ya hatua ya kumaliza migogoro ya kisiasa na chuki ambayo iliibuka tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kwanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s