Ahsanteni kwa msaada

Hoteli ya Serena Inn ya Zanzibar kupitia Jumuiya isiyo ya kiserikali, Zanzibar Outreach Program (ZOP) inayojishughulisha na huduma za jamii, imekabidhi msaada wa vitanda 14, magodoro na vifaa vingine vyenye thamani ya shlinngi milioni 55 vilivyotolewa msaada kutoka Hospitali ya St. Jude ya Uingereza kwa ajili ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ya Mjini Zanzibar. Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk. Malik Abdallah Juma (wa pili kupia), Mwenekiti wa bodi ya wadhamini wa ZOP, Maalim Mohammed Idrissa, na Meneja wa Serena Inn Daniel Sambai na wafanyakati wakiwa katika picha ya pamoja kwenye sherehe ya makabidhiano iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena Inn Mjini Zanzibar

HOSPTALI ya Rufaa ya Mnazimoja leo ilipata vitanda maalum 14 vya wagonjwa ili kuongeza mahitaji ya vifaa hivyo kwa wagonjwa.

Vitanda vyenye thamani ya shilingi milioni 55.4 ni msaada wa taasisi ya kiraia iitwayo Zanzibar Outreach Group (ZOP) kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo.

Mkurugenzi wa ZOP, Kuki Aggarwal, alisema wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo kuwa, vitanda hivyo vimetolewa kwa taasisi yake na Hospitali ya St Jude ya Uingereza, kupitia Aga Khan Foundation huko Zanzibar.

Aggarwal alisema taasisi yake imeamua kutoa vifaa hivyo kwa Hospitali ya Mnazimoja chini ya utekelezaji wa mpango wake endelevu wakusaidia sekta za huduma za afya, maji na elimu.

Msaada wa vitanda hivyo ulikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Malick Juma na Meneja wa Hoteli ya Serena, Daniel Sambai.

Akiipongeza taasisi ya ZOP kwa msaada huo, Dk Malick alisema vitanda ni miongoni mwa mahitaji muhimu kwa hospitali hiyo ya Mnazimoja yenye jumla ya vitanda 400.

Hata hivyo, Dk. Malick hakueleza kama Hospitali ya Mnazimoja ina upungufu wa vitanda au imejitosheleza kwa mahitaji hayo, lakini hospitali hiyo hivi sasa inakabiliwa na ukosefu wa vifaa muhimu katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) bvaada ya mashine zote za tano za kusaidia wagonjwa kupumua kuharibika tangu mwaka jana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s