Waziri ashindwa kujibu swali

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dk Sira Ubwa Mamboya ambae ni mtaalamu wa kifua kikuu hapa Zanzibar na pia Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rais kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana alishindwa kujibu swali ndani ya baraza la wawakilishi akisema swali hilo ni kubwa kuliko uwezo wake.

Naibu Waziri ashindwa kujibu swali

NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Dk Sira Ubwa Mamboya jana alishindwa kujibu swali aliloulizwa na mjumbe ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi akisema suali hilo kubwa kuliko uwezo wake wa kujibu na kulazimika Waziri wake kusimama na kujibu.

Suali lililomshinda Naibu huyo liliulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman aliyetaka kujuwa lini wizara itawapatia magari madaktari wakuu kutokana na umuhimu wa kazi zao za kutoa huduma kwa wananchi.

“Mheshimiwa Spika hilo swali naliona ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kujibu….” Alisema Naibu huyo ambapo wajumbe wenzake walikuwa wakipiga makofi na Spika kumtaka Waziri na Afya kusimama na kujibu swali hilo la nyongeza.

Akijibu swali hilo msingi Naibu Waziri wa Afya Dk Sira alisema kwa sasa haina uwezo wa kuwakopesha magari madaktari kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali ikiwemo za dharura kwa wananchi.

Sira alisema umuhimu wa madaktari unafahamika zaidi wakati pale inapotokea dharura muhimu na kutakiwa kufika haraka katika hospitali kuu lakini kwa sasa bajeti ndogo ya serikali haiwezi kukidhi mahitaji yote hayo.

“Mheshimiwa Spika umuhimu wa madaktari kuwa na usafiri wao ni muhimu sana katika kuimarisha huduma za matibabu kwa wananchi wetu na hilo serikali inalifahamu lakini kwa sasa wizara haina uwezo wa kuwapatia madaktari hao kila mtu gari yake”alisema Dk Sira.

Alisema kwa sasa madaktari hao wanatumia magari yaliopo wizara ya afya katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ajili ya kutoa huduma zaidi za dharura ili kuweza kufika haraka katika hospitali hiyo wanapohitajika.

Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae (CCM) Mohammed Said Mohammed aliyetaka kujua utaratibu gani unaotumika kuhakikisha madktari wanaopangiwa kazi wanakuwepo muda wote, Dk Sira alisema kwamba madaktari bingwa wanakuwepo katika hospitali ya Mnazi Mmoja ili kutoa huduma za afya hasa dharura.

“Utaratibu maalumu umepangwa kwa madaktari kuwepo kazini wakati wa usiku ‘first on call’ kwa kila idara za hospitali. Na kama kuna haja ikitokezea kuyakiwa daktari bingwa ‘second on call’ anatafutwa na gari la hospitali kwa kuja kutoa huduma” alisema waziri huyo.

Akijibu suala la nidhamu Dk Sira alisema hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa madaktari ambao watashindwa kuwepo katika maeneo yao ya kazi kwa ajili ya kutoa huduma za kwa wagonjwa katika hospitali zote kuu Unguja na Pemba.

“Mheshimiwa Spika endapo itabainika kuwa ushahidi na kuthibitisha kwa daktari kufanya kosa hilo basi hatua za kinidhamu za kiutumishi zinazhukuliwa dhidi yake mara moja” alisisitiza Waziri huyo.

Hata hivyo waziri huyo amesema hivi sasa kumeanzishwa kitengo maalumu cha mahusiano ambapo nambari za simu zimebandikwa kila wodi na maafisa wanahusika ni kutoa ‘quality control unit na public relation officer wapo kwa ajili ya kupokea taarifa hizo.

Advertisements

One response to “Waziri ashindwa kujibu swali

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s