Changamoto za maji safi

Makamu wa Pili wa Rais Mhe Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe Alfonso E. Lenhardt, aliyekuja agana naye baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini

Tatizo la upatikanaji maji safi na salama ni miongoni mwa chngamoto kubwa zinazoikabili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba.

Hayo yalielezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi katika mazungumzo yake na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Alfonso E. Lenhardt aliyefika Ofisini kwa Makamu huyo kuagana naye, baada ya kumaliza muda wake hapa nchini.

Alisema upungufu au uhaba wa maji katika maeneo mengi ya Zanzibar umeleta kero kubwa kwa jamii ya Wazanzibari na hata kuchangia miripuko ya maradhi kwa baadhi ya sehemu hasa katika nyakati za mvua

Hivyo aliiomba Serikali ya Marekani kuangalia uwezekano wa kuliingiza suala hilo katika mpango wake wa misaada kwa Zanzibar katika kipindi kijacho.

Ambapo aliafiki ushauri wa Balozi Lenhardt wa kutumia maji ya bahari kwa ajili ya kunjwa na kuitaka kampuni husika kuja fanya mazungumzo juu ya mradi huo.

Halikadhalika Mhe Balozi Iddi alieleza changamoto nyengine na namna Serikali ilivyojipanga kuzishughulikia ikiwemo mipango imara ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na zao la karafuu, uvuvi, umeme na Viwanda vidogo vidogo.

Kuhusu tatizo la Maji Balozi Alfonso Lenhardt alisema tatizo la maji kwa Zanzibar linaweza kutatuka iwapo Serikali itaweza kutumia maji ya bahari yaliokizunguuka kisiwa kizima, ingawa mradi huo utakuwa na gharama kubwa mwanzoni.

Hivyo aliishauri Zanzibar kuelekeza azma hiyo kama mojawapo ya njia la kulimaliza kabisa tatizo hilo na pia alieleza hatua za matayarisho yaliyofikiwa katika utengenezaji wa waya wa Umeme wa MCC kutoka bara

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s