Tunakupongeza kijana

Mbunge wa Kilwa Kusini Mkoani Lindi (CUF), Selemani Bungara maarufu kwa jina la Bwege (kulia) akishangilia pamoja na wengine, wakati Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko

WANACHAMA wa CCM wametakiwa kuacha tabuia ya kuchagua viongozi kwa nyimbo za ‘maarufu’ na badala yake wachague viongozi wanaouzika ili kukifanya Chama cha mapinduzi kushinda katika uchaguzi Mkuu ujao.

 

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili kwa ajili ya Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya ya WanawakeTanzaniakatika matawi 45 ya CCM Wilaya Kaskazini ‘B’ Unguja iliyofanyika katika ukumbi wa Bernard Membe huko Kitope.

 

Mama Asha, alisema haitapendeza kuona wanawake wanaendeleza nyimbo za kuwapamba wagombea kwa kelele za maarufu na badala yake wachague viongozi wanaouzika ili CCM iweze kushinda katika chaguzi zijazo.

 

Alisema kelele za ‘maarufu’ hivi sasa zimepitwa na wakati kwani zimekuwa zikichangia kutoa ushawishi kwa viongozi wabovu kuonekana kuwa na sifa jambo ambalo limekuwa likikitia chama kupata viongozi wanashindwa kuwatumikia wananchi.

 

Alisema kuendelekeza nyimbo hiyo imesababisha kuwavunja nguvu wengine kwa kushindwa kuwatoa dosari wagombea wanaowaona kutokuwa na sifa.

 

Alisema lazima wanachama wa CCM waanze kujibadili na tabia hiyo kutokana na uchaguzi ujao wa CCM unaotarajiwa kufanyika 2012 utakuwa ni wenye mazingira mgumu.

 

Hali hiyo alisema itakuja kutokana na maandalizi yajayo yatahitaji kufanyika kwa umakini kutokana na CCM kuhitaji kupata viongozi bora na sio watu maarufu , watoa Michele ama kuangalia sura zao.

 

Jambo wanalotakiwa kufanya mama Asha alisema itakuwa vyema kuona viongozi wa Matawi wanatumia ushawishi wao kwa kulihamasisha kundi la vijana kuona wanajitokeza kuchukua fomu.

 

Alisema kundi la vijana ndilo linalopaswa kuhamasishwa hivi sasa kwani ndilo litaloongeza nguvu kazi katika uongozi bora na sio kuwapiga mateke huku wakikumbatia viongozi wasioweza kuwatumikia wananchi.

 

“Msiwaongope watoto wahamasisheni wakachukue fomu wagombee sio mun’ga ng’anie viongozi ambao wakirudi chama kinapigwa madogo hivyo sivyo chagueni wataokuwa na ushawishi wa chama kushinda na wataokuwa karibu na jamii” alisema Mama Asha.

 

Akiendelea kwa vile hivi sasa serikali iliopo madarakani ni ya Umoja wa kitaifa bado wanachama wa CCM wanapaswa  kujitambua kuwa wanakabiliwa na kazi kubwa ya kukihakikishia Chama cha mapinduzi Kinashinda katika uchaguzi Mkuu ujao.

 

Alisema kwa kutokana na mfumo mpya wa utaratibu wa shughuli za Chama kuagiza kuanza kushirikisha ngazi ya matawi ni vyem kwa wenyeviti na makatibu hao kuona wanatumia nafasi zao ili kuihamasisha wanachama wao kushiriki katika uchaguzi wa 2012.

 

Mapema Naibu Katibu Mkuu upande wa Zanzibar Salama Aboud Talib, akitoa maelezo yake alisema Jumuiya ya wanawake inamchango mkubwa kuona CCM inabakia marakani na aliahidi kuona Chama hicho kinakuza makundi ya wanawake ili kukipa ushindi Chama hicho katika chaguzi zake za hapo baadae.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s