Chota elimu kutoka kwa wajuzi

Pata kitabu kipya kilichotungwa na Dkt. Issa Haji Ziddy kiitwacho “Lugha ya Kiarabu Zanzibar: Historia na Mbinu za Ufundishaji” ambacho kinaelezea kwa muhtasari, historia na chimbuko la Waarabu na lugha ya Kiarabu Zanzibar na Afrika ya Mashariki kwa jumla.

Wananchi na wasomaji wapenzi wa vitabu mbali mbali napenda kuwatangazia kwamba kumetoka kitabu kipya kilichotungwa na Dkt. Issa Haji Ziddy kiitwacho “Lugha ya Kiarabu Zanzibar: Historia na Mbinu za Ufundishaji” ambacho kinaelezea kwa muhtasari, historia na chimbuko la Waarabu na lugha ya Kiarabu Zanzibar na Afrika ya Mashariki kwa jumla.

Kitabu hicho pia kinaonesha nafasi ya Zanzibar katika ueneaji wa Kiarabu. Aidha kinachambua taathira za Kiarabu katika Lugha ya Kiswahili, Waswahili na Utamaduni wa Mzanzibari. Hatimae kitabu kinaelekeza mbinu bora za kusomeshea Kiarabu pamoja na kuchambua misingi muhimu anayotarajiwa kuwa nayo mwalimu wa lugha ya Kiarabu.

Kwa wale wasiomfahamu Dkt Issa Haji Ziddy ni Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).Amepata Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Elimu ya Kiislamu (Islamic Education) na Usomeshaji wa lugha ya Kiarabu kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Africa, Khartoum, Sudan mwaka (2001). Anafundisha masomo ya Ualimu na Mbinu za Kusomesha Elimu ya Dini ya Kiislamu na Mbinu za kusomesha Lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha SUZA na Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani.

Aidha amewahi kufundisha masomo ya Utamaduni wa Kiislamu (Islamic Culture) katika Chuo cha Northwest College, Wyoming, Marekani akiwa ni mshiriki wa “Fulbright Visiting Scholars Programme”. Vilevile amesomesha masomo ya Utamaduni wa Kiislamu na kufanya Utafiti wa Mbinu za kisasa za Usomeshaji wa lugha ya Kiarabu katika Taasisi ya “Oriental Studies” ya Chuo Kikuu cha Leipzig, Ujerumani. Amechapisha machapisho kadhaa ikiwemo vitabu na makala katika majarida na Makongamano ya Kitaifa na Kimataifa kuhusiana na Elimu ya Kiislamu kwa mtazamo wa kisasa pamoja na Mbinu za Usomeshaji wa Lugha ya Kiarabu kwa wasiokuwa Waarabu.

Miongoni mwa vitabu alivyochapisha Dkt Issa Ziddy ni pamoja na “Historia na Maisha ya Shekhe Hassan bin Ameir Shirazi”, “Misingi ya Ualimu na Mbinu za kusomeshea na kujifunzia Elimu ya Dini ya Kiislamu” ambavyo vyote vipo madukani chengine ni “Uislamu na Uzazi wa Mpango”. Ambacho kipo katika hatua za mwisho matayarisho ya kuchapishwa amabacho kinatarajiwa hivi karibuni kutolewa hadharani.

Wapenzi wasomaji wa vitabu na wananchi wote kwa ujumla napenda kuwatangazia kwamba vitabu hivyo vipo madukani kwa wale wenye kuhitaji wafike pale Masomo Book Shop au Duka la vitabu la SUZA au wasiliana nasi kwa namba hizi 0777475118, Darajani kwa Sir Major 0776416853, Msikiti Jibril 0777847012, Mlandege 0772807980 au 0777427131 au Salma Said 0777477101 au wasiliana na mtunzi wa vitabu kwa namba hizi hapa 0777508626 au 0713408626. Shime choteni ujuzi kwa walimu wetu na watunzi wazalendo. Kitabu cha Lugha ya Kiarabu Zanzibar ni shilingi elfu kumi tu za Tanzania.
Na vitabu viwili vilivyobakia ni shilingi elfu 5 kwa kila nakala. Soma ufaidike na mengi usiyoyajua kuhusu dini, utamaduni na historia ya nchi yako.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s