Malengo ya ZIRPP yatatimia?

Mmiliki wa Blog ya zanzibaryetu na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi/Citizen na Radio DW Salma Said akifanya mahojiano na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Sera za Umma Zanzibar (ZIRPP) muda mfupi baada ya uzinduzi huo ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani

 

HOTUBA FUPI YA DR. AHMED GURNAH KATIKA UZINDUZI RASMI WA TAASISI YA SERA ZA UMMA (ZIRPP) JUMAMOSI TARE 18 JUNI 2011, HOTELI YA BWAWANI, ZANZIBAR

 Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Dk. Ali Mohammed Shein, Rais waZanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;

Mheshimiwa Dk. Salim Ahmed Salim, Mlezi wa ZIRPP na Waziri Mkuu Mstaafu waTanzania;

Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, Makamu waKwanzawa Rais;

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais;

Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi;

Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu waZanzibar;

Waheshimiwa Mawaziri;

Bibi Maryam Hamdani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa ZIRPP;

Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;

Waheshimiwa Mabalozi;

Wageni Waalikwa;

Mabibi na Mabwana;

Assalam Aleykum,

Kwanzanapenda kutoa  shukurani zangu za dhati kwa “Zanzibar Institute for Research in Public Policy (ZIRPP)” kwa kunipa fursa ya kusema machache juu ya historia ya kuanzishwa kwa Taasisi hii hapaZanzibar.

Mnamo mwaka 1992, Profesa Abdul Sheriff alinialika kuhudhuriya mkutano juu ya “History and Culture of Zanzibar” uliofanyika katika Makumbusho ya Kasri (PalaceMuseum).  Katika waraka wangu niliouwasilisha kwa ajili hiyo, nilishauri juu ya umuhimu na haja ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Sayansi ya Jamii (Institute ofSocial Science), ambayo itaweza kufanya kazi na idara za serikali na baadaye kuwa na uwezo wa kuwa Chuo Kikuu kamili.  Wakati ule, hapakuwa na vyuo vikuu vya elimu ya juu (higher education) hapaZanzibar.

Kuanzia 1992, serikali, kwa kushirikiana na jamii na washirika mbali mbali wa maendeleo imefanikiwa kuanzisha vyuo vya elimu ya juu vifuatavyo:

-StateUniversityofZanzibar(SUZA)

-ZanzibarUniversity, Tunguu

-CollegeofEducation, Chukwani

-Karume Institute of Science and Technology

-CollegeofHealthScience

-Zanzibar Institute of Financial Administration

-Zanzibar Indian Ocean Research Institute (ZIORI)

-Open University centres in Beit Rus na Chake Chake

-Chuo cha Utumishi wa Uma

-Chuo cha Utalii , Marhubi

-InstituteofAgriculture, Kizimbani

-Chuo cha Uandishi wa Habari

-Chuo cha Ualimu cha Kiislamu, Mazizini

-Chuo cha Ualimu-BWMpaka, Wete

-Chuo cha Kiislamu, Micheweni

Naomba radhi Ikiwa nimesahau kitu chochote kingine.

Sasa, mwenye busara atauliza, ikiwa tumeshafunguwa vyuo vyote hivi, kwanini tunamualika Gurnah kuzungumzia juu ya waraka wake wa 1992? Hii ni kwa sababu bado yapo masomo ya sayansi ya jamii ambayo “ZanzibarInstitute for Research and Public Policy (ZIRPP)”, kwa mujibu wa katiba na malengo yake, inategemea kuyashughulikia. Kwa bahati mbaya, vyuo hivi bado havina muelekeo wala uwezo wa kuyashughulikia masuala haya ipasavyo.  Waraka wa 1992 ulizungumzia haja ya kufanya utafiti kwa madhumuni ya kujifunza na kuyafahamu zaidi masuala yafuatayo:

Mabadiliko yaliotokea baada Mapinduzi

Kujifahamisha juu ya mahitaji ya wananchi na vipi yatatekelezwa

Haki za wananchi katika elimu, afya, kazi na vipi zitapatikana

Namna nyengine za kutawala kwa maarifa na hekma

Ufatiliaji wa ufanisi katika serikali

Utafiti wa kuongeza demokrasia, maaendeleo na uhuru

Kuwapa nguvu zaidi wananchi na uwezo wa kuendesha nchi

Njia za kupigana na ubaguzi wa kila namna, i.e. ubaguzi dhidi ya wanawake, watu wenye ulemavu, kabila, na umasikini

Njia bora za kuwakaribisha Wazazibari wote kuchangia ujuzi, hata wale walioko nje ya nchi

Utafiti juu ya sera za jamii, utawala na serikali

Mafunzo juu ya uwezo wa utawala na kujenga serikali njema na imara

Waheshimiwa Wageni Waalikwa,

Mabibi na Mabwana,

Kwa kumaliza, napenda kusema tu kuwa leo tuna furaha kubwa kujumuika na nyinyi katika hafla hii adhimu ya uzinduzi wa taasisi yetu. Ni tegemeo letu kuwa tutafanikiwa katika jitihada za kufanikisha na kutekeleza malengo na majukumu ya taasisi yetu hii kwa maslahi na faida yaZanzibarna Wazanzibari kwa jumla.

Ahsantenisana.

HOTUBA YA BWANA MUHAMMAD YUSSUF, MKURUGENZI MTENDAJI WA ZIRPP KATIKA HAFLA YA UZINDUZI WA TAASISI SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 18 JUNI 2011 KATIKA UKUMBI WA SALAMA, HOTELI YA BWAWANI

 

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Dk. Ali Mohammed Shein, Rais waZanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;

Mheshimiwa Dk. Salim Ahmed Salim, Mlezi wa ZIRPP na Waziri Mkuu Mstaafu waTanzania;

Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, Makamu waKwanzawa Rais;

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais;

Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi;

Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu waZanzibar;

Waheshimiwa Mawaziri;

Bibi Maryam Hamdani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa ZIRPP;

Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;

Waheshimiwa Mabalozi;

Wageni Waalikwa;

Mabibi na Mabwana;

Assalam Aleykum,

Kwanzakabisa, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye wingi wa Rehma kwa kutuwezesha kufika hapa leo katika hafla hii muhimu ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya “Zanzibar Institute for Research and Public Policy” (ZIRRP) tukiwa sote katika afya njema. Pia, napenda kutumia fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwako wewe Mheshimiwa Rais na kwa viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kwa kukubali mwaliko wetu wa kuja kuchanganyika nasi katika kusherehekea uzinduzi wa taasisi yetu.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Kamatutajifunza kutokana na historia ya ulimwengu, basi tunaweza kugundua kuwa wazo la kuanzishwa jambo fulani muhimu au itikadi fulani ya kifalsafa, au uvumbuzi wa kiteknologia na kadhalika; mara nyingi wazo la aina hiyo huwa limebuniwa na mtu mmoja, au wawili, au hata kikundi kidogo cha watu. Lakini, wazo kamahilohaliwezi kuleta maana yoyote ikiwa halikuungwa mkono na kutekelezwa na walio wengi.

Kwa mfano, itikadi ya uchumi wa kibepari (Capitalism) ilibuniwa na Adam Smith, “Baba wa Ubepari” ambaye alikuwa Mwana-falsafa mashuhuri kutokaScotland. Maudhui ya kitabu chake kuhusu Ubepari: “An Inquiry into the Wealth of Nations” kilichochapichwa mnamo mwaka 1776, muda mfupi tu kabla ya waanzilishi wa taifa jipya la Marekani ambao walivutiwa sana na Wana-Falsafa wa Ulaya kujitangazia uhuru kutoka kwa mtawala wa Kiingereza yaliungwa mkono na kutekelezwa na nchi za Marekani ya Kaskazini, zikiongozwa na Marekani, na kutapakaa katika sehemu ya Magharibi ya Bara la Ulaya, Asia na hata Afrika. Hivi sasa ubepari umekuwa ndio mfumo wa kiuchumi unaotawala duniani kote.

Kwa upande mwengine, itikadi ya mfumo wa uchumi wa kikoministi au kijamaa (Communism), ilibuniwa na Karl Marx na mwenzake Freidrich Engels kule Ujarumani baada ya kuchapisha kitabu chao mashuhuri kilichojuulikana kwa jina la “The Communist Manifesto” mnamo mwezi Februari 1848 na ambacho maudhui yake yalikuja kuungwa mkono na Vladimir Ilych Lenin, kiongozi mahiri wa Mapinduzi yaliyoongozwa na chama cha Bolshevik mnamo mwaka 1917; na hatimaye kutekelezwa na nchi nyingi za Ulaya ya Mashariki zikiongozwa na Urusi ya Kisovieti na kutapakaa katika nchi za Asia, Afrika na Marekani ya Kusini.

Kwa kweli, itikadi mbili hizi ndizo zilizokuwa chimbuko kubwa la kuendelezwa kwa Vita Baridi baina ya kambi ya Magharibi na ile ya Mashariki na kumazikia mwezi wa Novemba 1989 pale ambapo ukuta waBerlin ulipoangushwa baada ya kusambaratika kwa Urusi ya Ki-Sovieti.

Dk. Ahmed Gurnah, katika maelezo yake mafupi, ameelezea kwa ufasaha mkubwa kabisa jinsi wazo la kuanzishwa kwa ZIRPP lilivyobuniwa na sababu zilizopelekea kubuniwa kwake. Mimi nitaongelea jinsi wazohilolilivyopata kuungwa mkono na kutekelezwa kwake – hatua ambayo imetufikisha hapa hii leo kushuhudia uzinduzi rasmi wa taasisi yetu; na hivi sasa ZIRPP iko wapi na inakusudia kwenda wapi katika utekelezaji wa majukumu na malengo yake.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Waheshimiwa Viongozi,

Wageni Waalikwa,

Mabibi na Mabwana,

Kabla sikuelezea jinsi taasisi ilivyoanzishwa, ningelipenda kwa muhtasari tu, kutoa ufafanuzi juu ya maana halisi ya taasisi ya sera au think-tankkamainavyojuulikana zaidi. Think-tank ni jumuiya yenye kujikita katika kufanya shughuli za kitafiti kuhusu masuala ya sera za kijamii, mikakati ya kisiasa, uchumi, sayansi na teknologia, biashara na viwanda na hata kutoa ushauri kuhusu masuala ya kiulinzi na kiusalama. Jumuiya nyingi za aina hii huwa zinafadhiliwa na serikali, au vikundi vyenye itikadi fulani, au makampuni ya kibiashara na kadhalika; au zinapata fedha kutokana na kazi za ushauri au utafiti zinazofanya katika utekelezaji wa miradi yake kwa njia ya malipo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2009, imegundulika kuwa kuna jumuiya za aina hii zipatazo 5,465 duniani kote. Kati ya hizi 1,777 zina makao makuu yake nchini Marekani; na takriban 350 kati ya hizo ziko WashingtonD.C.  Neno “think-tank” lilikuwa linatumika hapo awali kwa kumaanisha jumuiya zilizokuwa zikifanya shughuli zake kwa madhumuni ya kutoa ushauri wa masuala ya kiulinzi na kiusalamakamailivyokuwa ikifanya jumuiya maarufu ya Kimarekani inayojuulikana kwa jina la “Rand Corporation” iliyoanzishwa mwaka 1946 kutokana na kampuni iliyokuwa ikitengeneza ndege za kivita iliyokuwa ikijuulikana kwa jina la “Douglas Aircraft”.

Kuanzia miaka ya 40 hadi hivi leo, “thinks-tanks” zimekuwa zikianzishwa katika nchi mbali mbali duniani. Ukiacha nchini Marekani, mji mkuu waBelgium,Brussels, umekuwa ndio makao makuu ya jumuiya nyingi za kimataifa, zikiwemo “Global Governance Institute (GGI”) na “The European Policy Center (EPC). “The Centre for Economic Policy Research (CEPR)” yenye makao makuu yakeLondon ni mtandao mkubwa wa watafiti waliozagaa katika Bara la Ulaya unaochangiasana katika mijadala ya masuala yanayohusiana na maendeleo ya Ulaya.

Nchini Marekani kuna “think-tanks” nyingi zinazofadhiliwa moja kwa moja na serikali zenye kujikita zaidi katika utafiti wa masuala ya ulinzi na usalama zikiwa ni pamoja na “Institute for National Strategic Studies”, “Institute for Homeland Security Studies” na “Center for Technology and National Security Policy” iliyopo katika Chuo Kikuu cha “National Defense University” kule Washington.D.C..

Mnamo miaka ya 1960, Dk. Kwame Nkrumah alianzisha, jumuiya za kiserikali zilizojikita katika utafiti wa masuala ya kiuchumi na kimaendeleo. Jumuiya za aina hiyo zilizagaa kwa wingi Barani Akrika katika miaka 1990. Nchini Tanzania Bara, kuna jumuiya za aina hii tatu hivi sasa ambazo zimekuwa zikishiriki kikamilifu katika utafiti wa masuala ya kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo; zikiwa ni pamoja na “Economic and Social Research Foundation (ESRF)”, “Research and Education for Democracy in Tanzania (REDET)” na “Research on Poverty Alleviation (REPOA)”.

ESRF iliyoanzishwa mwaka 1994 imejijengea umaarufu mkubwasanakutokana na shughuli zake za utafiti; na sasa serikali yaTanzania, sekta ya binafsi na hata jumuiya ya wafadhili zimekuwa zikiitaka jumuiya hiyo kuwafanyia tafiti kuhusu masuala mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo. ESRF imechangia katika utekelezaji wa majukumu ya kimaendeleo ya serikali na hasa zaidi pale ilipopendekeza utekelezaji wa michakato ya mabadiliko katika sera za kijamii na kiuchumi.

Isitoshe, ESRF imeshiriki sanakatika kubuni sera mbali mbali za serikali kamavile “National Development Vision 2025”; “Poverty Reduction Strategy Paper (PRSP)”, “National Strategy for Growth and Reduction of Poverty (NSGRP-MKUKUTA na MKUZA na nyingi nyenginezo.  Tokea mwaka 1994, ESRF imeweza kufanya tafiti zaidi ya 200 na imetoa ushauri zaidi ya mara 300 kuhusiana na masuala mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo. Vile vile, ESRF imeandaa mikutano, warsha na semina zipatazo 500 nchini kote.

Katika utekelezaji wa majukumu yake, ESRF imekuwa ikifadhiliwa na taasisi mbali mbali, kama vile Serikali ya Tanzania, International Development Research Centre (IDRC)” kupitia mradi wa “Think Tank Initiative (TTI)”, “African Capacity Building Foundation (ACBF)”, “Foundation for Civil Society (FCS)”, “Global Development Network (GDN)”, “African Development Bank”, “The Ford Foundation”, “UNDP”, “Overseas Development Institute” na Serikali ya  Norway. Wakati wa kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1994, Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, alitoa mchango mkubwa sana kwa ESRF pale alipoamua kuipatia jengo taasisi hiyo kwa ajili ya ofisi pale Mlimani na TZS 50 milioni taslimu ili kuisadia kuanza kazi.

Kwa upande wake, REPOA imeanzishwa mwaka 1995kamajumuiya isiyokuwa ya kiserikali (NGO); na sasa imekuwa moja kati ya jumuiya muhimusanaza kitafiti nchiniTanzania. REPOA imejikita zaidi katika utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii. Katika miaka ya awali tokea kuanzishwa kwake, REPOA ilikuwa inafanya shughuli za utafiti Tanzania Bara naZanzibartu pekee. Lakini, kwa mujibu wa Mpango wake wa kazi wa mwaka 2010 – 2014, REPOA imeazimia kupanua shughuli zake za utafiti katika nchi jirani za Afrika ya Mashariki. Wafadhili wakubwa wa REPOA ni serikali zaNetherlands,Norway,United Kingdom,Sweden,FinlandnaTanzania. UNICEF, Benki ya Dunia na ILO pia zimekuwa zikiisaidiasanaREPOA kifedha katika utekelezaji wa malengo yake.

REDET imeanzishwa mwaka 1992 baada ya kurejelewa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini. REDET ilivutiwasanana mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali sio tu juu ya umuhimu wa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, lakini vile vile juu ya haja ya kuuelimisha Umma kuhusu demokrasia nchini. Tokea mwaka 1992, REDET imekuwa ikitoa mafunzo mbali mbali kuhusu maendeleo ya demokrasia nchini. Lengo kubwa la REDET ni kuanzisha mfumo madhubuti wa kidemokrasia wenye misingi ya utawala bora nchiniTanzania. Kwa muda mrefu sasa, REDET imekuwa ikifadhiliwa na Shirika la Misaada la Serikali yaDenmark, DANIDA. Kupitia Chuo Kikuu chaDar es Salaam, Serikali yaTanzaniaimekuwa ikichangia katika kuipatia REDET jengo la ofisi, wafanya kazi, watafiti na mabingwa wa taaluma.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Sasa nije katika suala la kuanzishwa kwa taasisi yetu. Harakati za kuanzishwa kwa taasisi ya ZIRPP zilianza mnamo mwezi wa Oktoba 2008 baada ya kikundi kidogo cha Wazanzibari walioafiki wazo la kuanzishwa kwake kukutana na kujadiliana juu ya hatua zinazofaa kuchukuliwa.Kwanza, iliamuliwa kufanya mashauriano na Wazanzibari kutoka fani mbali mbali za kimaisha; i.e. wasomi, wanasiasa, wafanya biashara, wanafunzi, watu wenye ulemavu, wana-michezo, na kadhalika. Matokeo ya mashauriano hayo ni zaidi ya kurasa 20 za mawazo mbali mbali tuliyoyakusanya.

La msingi ni kuwa karibu asilimia 99 ya waliotoa mawazo na fikra zao kuhusu suala hili waliwafiki dhana ya kuanzishwa taasisi hiyo na walisisitiza sanakuwa itakuwa ni jambo la busara na “muhimusanataasisi itakayoundwa ionekane kwa fikra, dhana na vitendo kuwa ni taasisi huru (independent) na pia haijaegemea upande wowote miongoni mwa vyama vya siasa (non-partisan)”.

Kwa hivyo, na kwa mujibu wa katiba yake, iliamuliwa kwa makusudi kabisa kuwa ZIRPP haitofungamana na chama chochote kile cha kisiasa. Kwa lugha nyingine, ZIRPP itakuwa “neutral” kabisa katika masuala ya kisiasa; ingawaje katika kutekeleza majukumu yake, ZIRPP haitosita kuipongeza serikali kila pale inapoonekana kufanya vizuri katika kulinda na kutetea maslahi ya wananchi; na vile vile haitosita kuikosoa serikali kila pale inapoonekana kuwa imekosea kwa madhumuni ya kujenga zaidi kuliko kubomoa.

Baada ya kukamilisha zoezi la mashauriano, mkutano rasmi wa kwanza ulifanyika tarehe 17 April 2009 chini ya Uenyekiti wangu; jumla ya wajumbe sita walihudhuriya mkutano huo. Pamoja na mambo mengine, mkutano ulijadili suala la uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Kaimu Meneja wa Fedha kwa madhumuni ya kuiwezesha taasisi kufanya shughuli zake haraka iwezekananvyo. Baada ya majadiliano mafupi, mkutano ulinichagua mimi na Bwana Jumbe Said Ibrahim kwa kauli moja kushika nyadhifa za Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Kaimu Meneja wa Fedha. Mkutano pia uliwachagua wajumbe watano wa Bodi ya Wadhamini ikiwa ni pamoja na Bwana Nassor Mugheiry, Bibi Maryam Hamdani, Bwana. Mbarouk Shaaban, Bibi Fatma Gharib Bilal na Bwana Abdulla Ghassany.

Kikao rasmi cha Mkutano wa pili wa taasisi kilifanyika tarehe 2 Mei 2009 kujadili rasimu ya katiba chini ya uenyekiti wa Bibi Maryam Hamdani. Jumla ya wajumbe 10 walihudhuriya katika mkutano huo; na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini walimchagua Bibi Maryam Hamdani kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini. Mkutano pia ulijadili juu ya suala la uwanachama, ada pamoja na michango mengine. Kwa kuzingatia hali halisi ya kipato cha Mzanzibari wa kawaida kwa mwezi, iliamuliwa kuwa mwanachama anayeishi nchiniTanzaniaatapaswa kulipa jumla ya TZS 13,500/- kwa mwaka; lakini, mwanachama anayeishi nje yaTanzaniaatapaswa kulipa USD 135.00 kwa mwaka.

Baada ya kukamilisha utayarishaji wa rasimu ya katiba, tulimkabidhi rasimu hiyo Marehemu Prof. Haroub Othman kwa madhumuni ya kutupa ushauri wa kisheria. Tunapenda kukiri wazi hapa kuwa Marehemu Haroub Othman alitupa ushauri mzurisanaambao ulisaidiasanakatika jitihada za kutayarisha katiba inayokidhi mahitaji ya taasisikamahii. Kwa vile kila nafsi itaonja mauti; na kwa vile mwenzetu ametutangulia mbele ya haki kabla ya kupata nafasi ya kushuhudia uzinduzi wa taasisi yetu, na kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa, ningelikuombeni msimame kwa dakika moja ili kumkumbuka mwenzetu huyu na huku tukimuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema Peponi – Amin.

Meshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Baada ya kukamilisha masharti yote ya usajili, taasisi ilikabidhiwa shahada rasmi ya usajili wake na Msajili wa Serikali tarehe 2 Aprili 2009 katika hafla mahsusi iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tembo. Mara tu baada ya kupata usajili rasmi, kazi ya kusajili wanachama ilianza haraka ingawaje taasisi ilikuwa bado haina ofisi rasmi ya kufanyia kazi. Nina furaha kutangaza kuwa hadi hivi sanataasisi imefanikiwa kusajili jumla ya wanachama 170. Kati ya wanachama hao, 136 ni Wazanzibari wanaoishi nchiniTanzania, na hasa zaidiZanzibar; na 34 ni Wazanzibari wanaoshi nje yaTanzania, wengi wao nchini Marekani. Miongoni mwa wanachama wetu hao, pia wamo wasiokuwa Wazanzibari ambao ni marafiki zetu wanaoipendaZanzibar na kuitakia nchi yetu maendeleo mema, utulivu na amani ya kudumu.

Azma kubwa ya taasisi ni kusajili wanachama wengi zaidi wanaoishi katika nchi za nje; sio tu kwa madhumuni ya kukusanya fedha nyingi zaidi kutokana na michango ya ada za uwanachama, lakini zaidi kwa sababu Wazanzibari waishio nje ya Tanzania watapata fursa moja nzuri na muhimu sana ya kushiriki katika kuanzishwa kwa chombo kitakachowaunganisha na Wazanzibari wenzao walioko nchini kwa madhumuni ya kuchangia kwa hali na mali jitihada zao za pamoja za kujiletea maendeleo ya kweli na endelevu; na hasa zaidi kusaidia katika jitihada za kupunguza umasikini na kunyanyua hali za maisha yao. Na kwa kweli, hili hasa ndio moja katika malengo muhimu ya kuanzishwa kwa taasisi hii.

Vipi Wazanzibari wanaweza kujiunga na ZIRPP? Ni vyema kutanabahisha kuwa Wazanzibari wanaotaka kujiunga na taasisi wanapaswa kujaza fomu na kulipa ada zao za uwanachama kwa mwaka mzima. Fomu za maombi zinapatikana ofisini kwetu au kwa njia ya Internet. Kwa hivyo, kila anayetaka kujiunga na taasisi yetu yuko huru kujaza fomu hizo na kuzituma moja kwa moja kwa njia ya email au kwa kufika ofisi yetu iliyopo katika jengo la Mazrui, ghorofa ya tatu, nyuma ya Majestic Cinema.

Tokea zoezi la kusajili wanachama lianze mnamo mwezi wa Aprili 2009, jumla ya TZS 50,655,885 zimeshakusanywa kutoka kwa wanachama wetu hadi hivi sasa. Kati ya hizo, TZS 24,245,885 zimechangwa kutokana na malipo ya ada za mwaka za wanachama wetu; TZS 17,000,000 ni ada ya uchauri (consultancy fees) kutoka Kamisheni ya Ukimwi, Zanzibar; TZS 5,000,000 ni mkopo kutoka kwa mwanachama wetu mmoja, na TZS 4,510,000 ni mchango kwa ajili ya uzinduzi wa taasisi. Kwa taarifa zaidi kuhusu ada za uwanachama na michango ya hiari kutoka kwa Wazanzibari mbali mbali, tafadhalini tembeleeni Weblog yetu: www.zirppo.wordpress.com. Kiwango kikubwa cha fedha zilizochangishwa, kwa sasa, kimetumika kwa ajili ya kulipia kodi ya Ofisi yetu; utiaji wa fanicha za ofisi; i.e. meza, viti, meza kubwa za mikutano pamoja na viti vyake na kuunganisha huduma za Fax na simu.

Hata hivyo, bado Taasisi inahitaji fedha zaidi kwa ajili ya kununulia vitendea kazi vyingine, kamavile kompyuta za kutosha. Kompyuta tulizo nazo hivi sasa, ambazo tayari zimeshatumika, zimepatikana kutokana na michango ya wanachama wetu. Kwa mfano, kuna wanachama waliotoa kompyuta 1 au mbili kamili; kuna wengine waliotoa key boards; au monitors, na kuna hata wale waliotoa mouses. Pia, tunahitaji photo copy machines, printers, projector, video cameras, digital cameras, na TV set kwa ajili ya kufanyia utafiti. Hali kadhalika, taasisi inahitaji fedha za kununulia stationaries pamoja na vifaa vyengine vingi vya ofisi.

Kwa bahati nzuri, pamoja na uhaba wa fedha, taasisi inaendeshwa na kuongozwa na wafanya kazi watatu, Mkurugenzi Mtendaji, Naibu Mkurugenzi Mtendaji na Meneja wa Fedha kwa njia ya hiari, kujitolea na bila ya malipo. Lakini, kutokana na haja iliyojitokeza baada ya kuhamia katika Ofisi yetu mnamo mwezi wa Novemba 2009, taasisi ililazimika kuajiri mhudumu wa Ofisi (cleaner); na Executive Assistant kwa madhumuni ya kutoa huduma za kiutawala (Administrative Support). Pia, taasisi imefanikiwa kupata volonteers wengine watatu ambao wamekubali kwa hiariyao kuitumikia ZIRPP kwa njia ya hiari, kujitolea na bila ya malipo.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Nini hasa faida ya kujiunga na ZIRPP? Faida kubwa itapatikana ikiwa taasisi itakuwa imejikita katika kufanya utafiti wa kina kuhusu sera mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo; ziwe katika nyanja za elimu, afya, mazingira, ardhi, utalii, biashara na kadhalika, ambazo utekelezaji wake utasaidia sana katika jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, bora na endelevu kwa manufaa na faida yao.

Pia, taasisi itaweza kutoa mchango mkubwa na muhimu sana kwa kuionesha serikali njia nzuri na bora ya ubunifu na utekelezaji wa sera kwa kuiga mifano mizuri ya ubunifu na utekelezaji wa sera inayofanyika kwengineko. Nchi nyingi, hasa zile zilizoendelea, kama vile Marekani, Ulaya Magharibi, na katika nchi zilizo Kusini Mashariki ya Asia, zimepiga hatua kubwa sana kiuchumi na kimaendeleo kutokana na ubunifu na utekelezaji mzuri wa sera za kiuchumi na kimaendeleo baada ya serikali husika kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na jumuiya kama yetu hii. ZIRPP,kamathink-tank makini, inaweza kutoa mchango mkubwa na muhimusana wa kifikra na kimawazo katika jitihada zetu za pamoja za kupunguza umasikini na kusukuma maendeleo ya kweli na endelevu katika nchi yetu.

Kwa bahati mbaya, kwa muda mrefu serikali imekuwa ikiendelezasanautaratibu wa kubuni sera mbali mbali na kuzipeleka haraka haraka katika Baraza la Wawakilishi kwa madhumuni ya kupitishwa bila ya kufanyiwa utafiti wa kina kwa madhumuni ya kutathmini athari zake (ziwe nzuri au mbaya) kwa jamii. Kwa bahati mbaya vile vile, wawakilishi wetu nao wamekuwa wakizipitisha au kuziidhinisha sera mbali mbali zinazowasilishwa barazani hapo bila ya kutambua kwa undani athari zake kwa jamii. Matokeo yake ni kudhoofika kwa uchumi wa nchi kutokana na utekelezaji wa sera zenye kasoro nyingi na hivyo kusababisha kuzorota kwa uchumi na maendeleo nchini kwa jumla. Inatosha tu kuangalia jinsi utekelezaji wa sera kuhusu ardhi, mazingira, maendeleo ya miji na kadhalika, unavyoathiri vibaya maendeleo ya nchi katika nyanja hizo.

Kinyume chake, nchini Marekani, kwa mfano, serikali inapotaka kuwasilisha Mswada wa Sheria katika Baraza la Wawakilishi (House of Representatives) au katika Baraza la Senate, rasimu ya Muswada kabla ya kupelekwa katika mabaraza hayo, kwa kawaida, huwa inatangazwa katika magazeti rasmi ya serikali pamoja na vyombo vingine vya habari ili kuwajuulisha wananchi kupitia taasisi zao mbali mbali kwa madhumuni ya kuujadili, kuuchambua na kuutolea maoni.

Mfano mzuri ni sera mashuhuri ya Huduma za Afya na Muswada wakekamaulivyobuniwa na kupendekezwa mwaka jana na wadau mbali mbali nchini humo. Muswada huo baada ya kukamilika utayarishaji wake, wadau mbali mbali walipata fursa ya kuujadili kwa muda wa zaidi ya miezi mitano kabla ya kuwasilishwa Barazani na hatimaye kupitishwa na Mabaraza yote ya kutunga sheria nchini Marekani. La muhimu hapa ni kuwa Wamarekani, kwa ujumla wao, walipatiwa nafasi na muda wa kutosha kuujadili Muswada huo kwa kina na kwa wakati unaofaa.

Kwa bahati mbaya, utaratibu wa aina hii hauko kwetu. Matokeo yake, sera na Miswada huwa inapitishwa haraka haraka, tena bila ya mijadala ya kina; na hivyo kuzorotosha kupatikana kwa maendeleo ya kweli kwa maslahi na faida ya wananchi. Kuanzishwa kwa taasisi yetu kutasaidia katika jitihada za kuelimishana ili kuondokana na kasoro za aina hii; na badala yake kuleta ufanisi mkubwa katika utendaji mzima wa shughuli za serikali; na hasa zaidi katika nyanja za ubunifu na utekelezaji wa sera mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mbwana,

“Asiyefanya utafiti, hana haki ya kusema”. Huu ni msemo mashuhuri wa Kichina ambao una maudhui mazuri na ni funzo kubwa kwa nchi zetu ikiwa utazingatiwa na kutekelezwa ipasavyo. Majukumu na malengo makuu ya taasisi yameorodheshwa kwa uwazi na ufasaha mkubwa katika katiba yake. Lakini, kwa muhtasari tu, moja kati ya malengo yake muhimu ni kujaribu kadri itakavyowezekana kuondoa utaratibu wa kubuni na kutekeleza sera mbali mbali bila ya kutoa nafasi na muda wa kutosha kwa wananchi kupitia jumuiya zao mbali mbali kujadili sera zinazobuniwa na kutekelezwa kwa madhumuni ya kuzitolea maoni kabla ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi na kuwa sheria kamili.

Taasisi inakusudia kufanya hivi kwa njia ya kuelimishana kupitia utafiti na kwa kutumia nguvu ya hoja kwa madhumuni ya kujaribu kuanzisha utamaduni mpya utakaokwenda sambamba na aina ya taratibu zinazotumika katika nchi zilizoendelea ili Wazanzibari nao wapatiwe nafasi na muda wa kutosha kushiriki kikamilifu katika mijadala ya sera mbalimbali zinazogusa maslahi na maisha yao ya kila siku. Kwa kuzingatia utaratibu tuliojiwekea, baada ya kufanya utafiti kuhusu masuala mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo, taasisi itatoa ripoti kamili kuhusu utafiti uliofanywa kwa kuelezea kwa uwazi kabisa matokeo ya utafiti huo na kutoa mapendekezo kamili juu ya hatua za kuchukuliwa. Ripoti pamoja na mapendekezo hayo yatawasilishwa serikalini kwa madhumuni ya kuitaka serikali kuyatekeleza kadri itakavyowezekana. Katika tafiti zake, Mkakati wa Serikali katika Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA) na Dira ya 2020 zitapewa kipaumbele maalumu.

Ikiwa ZIRPP itaanza kazi zake ipasavyo kama inavyotarajiwa, basi faida kubwa sana itapatikana kutokana na ukweli kuwa Zanzibar itakuwa imeanzisha taasisi ya kwanza kabisa katika historia yake yenye kujikita zaidi katika masuala ya utafiti wa sera za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo; taasisi ambayo itasaidia sana katika kuwafunua macho wananchi wa kawaida na hata Wabunge na Wawakilishi wetu kuelewa namna ya sera zinavyobuniwa na kutekelezwa na serikali kwa njia na utaratibu ulio wazi na wenye ufanisi mkubwa. Kwa kupitia taasisi, serikali pamoja na wananchi wataweza kujifunza jinsi ya kupatikana kwa ufanisi katika ubunifu na utekelezaji wa sera mbali mbali kwa kupitia mifano mizuri inayohusiana na utekelezaji wa sera kama hizo katika nchi nyingine ili Zanzibar isirudiye makosa yanayoendelea kufanywa nchini siku hadi siku; na hivyo kusaidia sana katika kuleta maendeleo makubwa, endelevu na ya kweli kwa wananchi wake.

Isitoshe, faida kubwa zaidi itayoweza kupatikana kupitia ZIRPP itatokana na uwezekano wa kuwaunganisha Wazanzibari kuwa kitu kimoja popote pale walipo duniani bila ya kujali itikadi zao kisiasa, kijinsia, kidini, kirangi na kadhalika. Kwa lugha nyingine, Wazanzibari wataungana na kuachana na tofauti zao za kisiasa kwa misingi ya kujenga nchiyaozaidi kuliko kushabikia siasa za vyama vyao. Hii ni faida kubwasanaitakayoweza kupatikana ikiwa Wazanzibari wataiunga mkono Jumuiya yetu hii, kwa hali namali.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Pamoja na ukosefu mkubwa wa vitendea kazi, fedha za kutosha na mambo mengine, taasisi imefanya mengi tokea kuanzishwa kwake. Kubwa ambalo tunajivunia kuwa tumeweza kulifanya ni kuanzisha taasisi. Na ili taasisi ikamilike, inahitaji kuwa na katiba na dira yenye kuelezea kwa ufasaha mkubwa malengo na majukumu ya taasisi katika kipindi cha miaka minne ijayo. Tunafurahi kusema kuwa haya yote yameshafanyika kwa wakati unaofaa.

Hivi sasa taasisi inayo katiba yake (charter); na imeshakamilisha utayarishaji wa dira yake: “2011-2014: Strategic Medium Term Plan” inayoelezea kwa kina na ufasaha mkubwa programu, shughuli, malengo na majukumu ya Taasisi katika kipindi cha miaka minne ijayo; ikiwa ni pamoja na idadi ya wafanya kazi na mishahara yao, vitendea kazi na gharama zake zote za uendeshaji.

Mnamo mwezi Januari 2010, taasisi ilipatiwa kazi na Tume ya Ukimwi ya Zanzibarya kutayarisha “Documentary Film” kuhusu mawasiliano baina ya mzazi na mtoto. Madhumuni ya picha hiyo yalikuwa ni kuwashajiisha wazazi kuendeleza na kuboresha mawasiliano na watoto wao hasa katika kujadili masuala ya afya na jinsi gani watoto wanavyoweza kujikinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi. Katika kuifanya kazi hiyo taasisi ilishirikiana na kampuni ijuulikanayo kwa jina la “Twaweza Communications” kutokaKenya. Taasisi kwa kuwatumia watafiti na wapiga picha wake waliopo hapa hapa nchini waliifanikisha kazi hiyo ndani ya muda uliowekwa na kwa ustadi mkubwasana. Kwa kweli, katika zoezi la utayarishaji wa picha hiyo (ambayo tayari imeshaoneshwa katika vituo vya TVZ na CBTV) ndipo taasisi ilipogundua kuwa Scriptwriters, directors, na producers wa Kizanzibari katika fani ya utayarishaji wa picha ni miongoni mwa walio bora kabisa katika Afrika ya Mashariki.

Mnamo mwezi wa Juni 2010, Taasisi ilifanikiwa kuitisha Mkutano wa kwanza kabisa wa Baraza Kuu uliojumuisha karibu wanachama wake wote kwa madhumuni ya kupitisha katiba na Mkakati wa Muda Mfupi wa Mpango wake wa kazi kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 na kuchagua Wajumbe 13 wa Baraza la Utawala (Governing Council) ambalo, pamoja na mambo mengine, lina mamlaka ya kujadili Mkakati huo na kuupitisha ikiwa ndio dira itakayoongoza shughuli za Taasisi kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Kazi hiyo ilifanyika isipokuwa, kutokana na ukosefu wa muda wa kutosha, Mkutano Mkuu ulishindwa kupitisha rasimu ya Mkakati huo pamoja na majina ya wajumbe 13 wa Baraza la Utawala. Mkutano Mkuu, kwa hivyo, uliunda Kamati Maalum ya Baraza Kuu kwa madhumuni ya kuujadili na kuupitisha Mkakati huo. Kazi hiyo ilifanyika baada ya vikao viwili vya Kamati hiyo maalum kukutana tarehe  24 Aprili 2010 na tarehe  08 Mei 2010 katika ukumbi wa mkutano wa taasisi.

Isitoshe, kwa kuzingatia umuhimu wa mawasiliano ya mtandao wa kompyuta (Internet), taasisi ilianzisha Weblog yake pamoja na Ukumbi wa Mazungumzo na Majadiliano (Discussion Forum) ambao ulitoa fursa kwa wanachama kupata taarifa za kila siku kuhusiana na maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Zanzibar; pamoja na kuchangia mada au hoja mbali mbali zinazojadiliwa katika ukumbi huo. Pia, taasisi, tokea mwezi Januari 2010, imeanzisha “Monthly Lectures” zinazofanyika katika ukumbi wa mkutano wa taasisi mara moja kila mwezi. Mada mbali mbali kuhusu sera za kiuchumi na kijamii huwasilishwa na wahadhiri waalikwa na kujadiliwa na wanachama wetu.

Na hivi karibuni taasisi imefanikiwa kuanzisha Website yake rasmi (www.zirpp.org) ambayo, pamoja na mambo mengine, ina madhumuni ya kutoa taarifa kwa ufasaha mkubwa kuhusu shughuli zote za taasisi kwa wanachama wake na hata kwa wasiokuwa wanachama duniani kote.  Hivi sasa, taasisi imo mbioni kukamilisha zoezi la kuweka Database mahsusi kuhusu wataalamu wote wa Kizanzibari waliopo ndani na nje ya nchi kwa madhumuni ya kufahamu walipo na taaluma walizonazo.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Nini taasisi inakusudia kufanya baada ya uzinduzi wake hii leo kwa maslahi yaZanzibarna ya Wazanzibari kwa jumla imeelezwa wazi katika dira yetu ambayo nakla yake atakabidhiwa Rais waZanzibarkwa taarifa yake hivi punde. Kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kutayarisha ripoti mahsusi, baada ya kufanya utafiti wa kina, kuhusu masuala mbali mbali ya kitaifa; iwe katika nyanja za uchumi na biashara, mila na utamaduni, siasa na michezo, na kuwasilisha mapendekezo mahsusi serikalini kwa utekelezaji. Kwa taarifa yenu, hivi sasa, kwa ufadhili binafsi wa wanachama wetu wawili, taasisi imo katika kukamilisha utayarishaji wa ripoti zake mbili za kwanza kabisa ambazo zitawasilishwa serikalini karibuni. Mnamo siku zijazo, na baada ya kupata fedha za kutosha, taasisi inakusudia kufanya tafiti juu ya masuala yafuatayo:

i)         Review of the Efficiency and Effectiveness of Land Use, Housing and Urban Development and Environmental Policies;

ii)        Review of the Efficiency and Effectiveness of Public Health System in Combating HIV/AIDS Pandemic and Other Infectious Diseases;

iii)      The Adverse Effects of Youth Unemployment in the Context of the Emerging Crime Proliferation and Drug Abuse;

iv)       Modern Agricultural Technology and Food Security Policy, and Its Sustainability;

v)        Endangered and Extinct Species: Their Implications on the Country’s Future Natural Resources and Heritage;

vi)       Review of the Efficiency and Effectiveness of the Existing Poverty Alleviation Policies and Strategies;

vii)               Review of the Efficiency and Effectiveness of Procurement Practices within the Zanzibar Government Agencies and Related Institutions.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mabwana,

Ningelipenda sasa kuzungumzia kidogo juu ya changamoto mbali mbali ambazo taasisi inakabiliwa nazo. Niligusia hapo awali kuwa katika kikao cha Mkutano wa Baraza Kuu (General Assembly) kilichofanyika mwaka jana, taasisi ilishindwa kuchagua wajumbe 13 wa Baraza la Utawala (Governing Council) kutokana na ukosefu wa muda wa kutosha. Kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha, taasisi imeshindwa kuitisha kikao kingine cha Mkutano Mkuu mwaka huu na hivyo kushindwa tena kuchagua wajumbe wa Baraza la Utawala. Ni tegemeo letu kuwa baada ya uzinduzi huu, taasisi itaweza kupata fedha za kutosha kutoka kwa wafadhili mbali mbali kuitisha kikao cha Mkutano wa Baraza Kuu hapo mwakani na kumaliza kazi ya uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Utawala. Kwa kweli, kitendo cha kushindwa kuchagua wajumbe 13 wa Baraza la Utawala ni kikwazo kikubwasana kwa maendeleo ya taasisi. Taasisi inahitaji msaada wa haraka ili iweze kukamilisha kazi hii bila ya kuchelewa zaidi.

Mwaka jana taasisi ilipanga kuitisha mkutano wa kimataifa hapaZanzibarambao ungeliwajumuisha Wazanzibari walioko ndani na nje ya nchi kwa madhumuni ya kubadilishana mawazo na fikra juu ya mustakbali waZanzibar. Mialiko ilitolewa na Wazanzibari wengi waliitika kwa kutayarisha mada mbali mbali za kujadiliwa katika mkutano huo. Jumla ya mada 30 zilipendekezwa kwa kuwasilishwa mkutanoni na Wazanzibari walio ndani ya nchi; wakati mada nyingine 7 zilipendekezwa na Wazanzibari pamoja na marafiki zetu walioko nje yaZanzibar. Kwa mujibu wa utaratibu uliopangwa, baada ya majadiliano ya siku mbili, mada zitakazokubaliwa zingechapishwa katika kitabu mahsusi ambacho nakala yake angelikabidhiwa Rais waZanzibarkama mchango wa Wazanzibari kuhusu mustakbali waZanzibar.

Awali, taasisi ilipanga kuwa mkutano huo ufanyike mwezi Septemba 2010; lakini, mfadhili mmoja aliyeonyesha nia ya kutaka kusaidia katika utayarishaji wa mkutano huo alitushauri kuakhirisha kufanyika kwa mkutano huo hadi mwezi June 2011 ili kuipa taasisi yake muda wa kutosha kulizingatia ombi letu.  Kwa kuamini kuwa mfadhili huyo angelilikubali ombi letu, taasisi ilikubali kuakhirisha kufanyika kwa mkutano huo. Kwa mshangao mkubwa, wiki chache tu baadaye, mfadhili aliandika kutuarifu kuwa taasisi yake isingeliweza kufadhili utayarishaji wa mkutano huo. Jumla ya Euro 38,000.00 zilihitajika; na hivi sasa taasisi imo mbioni kutafuta wafadhili wengine watakaoweza kusaidia kufanikisha mradi huu.

Kwa kweli, huu ni mradi muhimusanaambao utekelezaji wake utasaidiasanakatika jitihada za kuileteaZanzibarmaendeleo ya kweli na endelevu. Ni tegemeo letu kuwa serikali pamoja na nchi wafadhili na jumuiya za kimataifa zitalizingatia ombi letu hili kwa makini kwa madhumuni ya kuhakikisha utekelezaji wake bila ya kuchelewa zaidi.

Kwa upande mwingine, ili taasisi ionekane kuwa iko makini na inafanya shughuli zake kwa ufanisi wa hali ya juu, inapaswa kuhakikisha kuwa mahesabu yake juu ya mapato na matumizi yanakaguliwa kwa wakati unaofaa. Kwa hivyo, zoezi la ukaguzi kwa ajili ya taasisi yetu lilifanyika vizuri kwa mwaka 2009 na 2010. Sisi Consultants ndio waliokuwa wakaguzi wetu kwa kipindi hicho; na tungelipendasanakuendelea nao hadi mwisho wa mwaka huu. Lakini, taasisi imeshindwa kulipa deni lao la TZS 2,000,000.00 kutokana na upungufu mkuwa wa fedha. Haitokuwa jambo baya hata kidogo iwapo taasisi itapata mfadhili wa kutusaidia kukaguliwa ipasavyo na kwa wakati unaofaa ili tuweze kufanya kazi kwa uwazi na ufanisi wa hali ya juu. Tunatoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa uongozi wa Sisi Consultants kwa ustahamilivu wao.

Kwa kweli, taasisi haiwezi kujiendesha bila ya kupata wanachama wengi wenye kuguswa na kuvutiwa na malengo na majukumu ya taasisi kwa udhati wa nyoyo zao; wanachama walio tayari kuisaidia taasisi kwa hali na mali ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Kusema kweli, idadi ya wanachama tulionao hivi sasa ni ndogosana; licha ya jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa katika kujaribu kuwashajiisha Wazanzibari wengi kutuunga mkono. Isitoshe, inasikitisha kuona kuwa baadhi ya wanachama wetu bado hawalipi ada zao kwa ukamilifu na kwa wakati unaofaa. Matokeo yake, sehemu kubwa ya fedha za kulipia kodi ya ofisi pamoja na hata uzinduzi wa taasisi inawategemea zaidi wanachama wetu wachache. Hata hivyo, tunapenda kutumia fursa hii kuzishukuru taasisi za Benki ya Watu waZanzibar(PBZ), Shirika la Bandari (ZPC) na Multi-Color Printers kwa kujitokeza kuchangia fedha katika shughuli ya uzinduzi wa taasisi yetu hii leo.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Mabibi na Mbwana,

Kwa kumaliza, labda niseme tu kuwa, taasisi ni wanachama. Bila ya wanachama hai na wenye moyo wa kujitolea kwa hali namali, hakuna taasisi. Na ikiwa hakuna taasisi, basi ni dhahiri kuwa hakuna litakaloweza kufanyika. Bila ya shaka yoyote, michango tunayoendelea kuipata kutoka kwa wanachama wetu kila mwaka ni muhimusana; lakini, haikidhi haja ya kuiwezesha taasisi kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kwa ufanisi unaohitajika. Kusema kweli, hata wanachama wetu wote walipe ada zao kwa ukamilifu na kwa wakati unaofaa, basi hazitoshi hata kulipia kodi ya kila mwezi ya ofisi yetu; seuze kuchangia katika shughuli za utafiti. 

Hata hivyo, ni tegemeo letu kuwa kama taasisi ya nyumbani, serikali yetu na wafadhali watathamini mchango ambao taasisi unaweza kuutoa katika masuala ya uchambuzi wa sera; na hasa kwa kuzingatia haja na umuhimu wa Wazanzibari wenyewe kuwa na chombo chao kama hiki. Katika jitihada za kufanikisha malengo yake, taasisi iko tayari kutoa ushindani mkubwa katika kupata fedha za wafadhili wa ndani na wa kimataifa; na hasa kwa kuzingatia uwezo wetu kama taasisi ya nyumbani yenye uzoefu na ujuzi wa kutosha katika kuyaelewa masuala mbali mbali na mazingira ya nyumbani ikiwa ni pamoja na mila na tamaduni za Wazanzibari. Kwa mnasabu huu, ni tegemeo letu kuwa serikali nayo haitosita kuipa taasisi yetu kila fursa itakayojitokeza ili taasisi iweze kuthibitisha uwezo na umahiri wake kiutendaji kila pale serikali inapotaka huduma za kitaalamu au kishauri.

Kwa kuzingatia hayo, taasisi inapenda kutoa mualiko rasmi kwa serikali na kuiomba kuangalia uwezekano wa kuipatia taasisi msaada wa hali na mali; na hasa zaidi katika eneo la kujenga uwezo wake kiutendaji na kiutekelezaji katika wakati huu mgumu wa kuanzishwa kwake. Msaada wowote ule kutoka serikalini utasaidiasanakatika kuiwezesha taasisi kukabiliana na majukumu yake ipasavyo na kujitegemea yenyewe siku za mbele katika utekelezaji mzuri wa malengo na majukumu yake.

Ni tegemeo letu kuwa, baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi yetu hii leo ambao, lazima nikiri, kuwa umepata msukumo mkubwa sana kwa kushuhudiwa na kuungwa mkono na viongozi wetu wa juu, mafanikio yatakayopatikana baada ya hafla hii adhimu, na hasa zaidi muamko utakaojitokeza hapo, utawazidishia wanachama wetu wote nia, ari na kasi kubwa ya kuisaidia taasisi yetu hii kwa hali na mali zaidi kuliko ilivyo hivi sasa. Vile vile, ni imani yetu kuwa baada ya uzinduzi huu, Wazanzibari wengi zaidi watashawishika kujiunga na taasisi yetu hii kwa faida na maslahi yaZanzibarna wananchi wake.

AHSANTENISANAKWA KUNISIKILIZA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s