PPF kufanya utafiti ili kusaidia elimu


MFUKO WA Hifadhi ya Jamii (PPF) unafanya utafiti ili kuona uwezekano wa mfuko huo kutoa mafao ya elimu kwa wanafunzi wa kidato cha tano, sita na vyuo.Hatua hiyo inakusudia kutoa jibu la kilio cha muda mrefu cha wadau wa mfuko huo kutaka wananfunzi wa ngazi ya elimu hiyo kupewa stahili ya mafao hayo kama ilivyo kwa wanafunzi wa mkondo wa elimu kuanzia vituo vya chekechea hadi wa kidato cha nne.

Meneja wa PPF wa Kanda Ilala, Dar es Salaam , Zahra Rashid Kayugwa alisema jana mjini hapa kuwa utafiti huo unaendeshwa chini ya utaratibu wa unaofanyika kila baada ya kipindi cha kati ya miaka mitatu hadi mitano ili kuangalia uwezo wa PPF kulipa mafao.

Zahra alisema hayo wakati anazungumza na wadau wa huduma za PPF walioshiriki katika semina ya siku moja ya uelimishaji wanachama juu ya shughuli za uandikishaji, ulipaji michango na ulipaji mafao kwa wanachama kwenye Hoteli ya Ocean View, Kilimani.

Bila kusema muda wa kuanza na kukamilika kwa kazi ya utafiti huo, Zahra alisema matokeo ya kazi hiyo ndio yatakayowezesha PPF kuamua kuwashirikisha wanafunzi wa elimu ya ngazi ya kidato cha tano, sita na vyuo katika mpango wa malipo ya mafao ya elimu.

Chini ya utaratibu wa sasa, mpango huo unawanufaisha wanafunzi wa chini ya umri wa miaka 18, ambao wazazi wao wamefariki, kwa mujibu wa Zahra na kwamba wanafunzi wenye sifa ya kulipwa mafao hayo ni wale ambao uchangiaji katika mfuko huo umetimiza miaka mitatu.

“Utafiti huu unafayika baada ya PPF kuzingatia maoni ya wadau kwamba wananfunzi wa ngazi ya kidato cha tano, sita na vyuo, nao wapate malipo ya mafao ya elimu kwa sababu wengi wao, pia bado wapo chini ya utegemezi wa wazazi,” alisema Zahra.

Alisema mpango wa malipo ya mafao ya elimu unaowanufaisha wanafunzi katika elimu ya chekechea hadi kidato cha nne kwa elimu ya sekondari ulianza mwaka 2003.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s