Uchumi sio suala la Muungano

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha, Mipango na Uchumi Zanzibar, Omar Yussuf Mzee

Uchumi sio suala la Muungano

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wazanzibari kuzungumzia kwa kina suala la uchumi liondolewe katika orodha ya Muungano wakati wa kuchangia rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha, Mipango na Uchumi Omar Yussuf Mzee wakati akijibu swali la nyongeza katika cha baraza la wawakilishi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, aliyetaka kujua kwa nini suala la uchumi kuratibiwa wa muungano wakati sio suala la Muungano.

Waziri huyo alisema kuwa hatua hiyo itaweza kumpa fursa nzuri ya kuweza kuyasimamia masuala hayo ya uchumi kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

“Nakubaliana na Mwakilishi wa Mji Mkongwe Mheshimiwa Jussa kwamba suala ya uchumi si ya Muungano lakini yamo baadhi yake tu na yakiondolewa nakubaliana na mheshimiwa kwamba yatanipa nafasi nzuri ya kuyasimamia katika katiba ya Zanzibar, lakini pia nawaomba sana wazanzibari walisimamie hilo ili likija suala la kujadilia katika mpya watoe maoni yao” alisema Mzee.

Mwakilishi wa Jimbo la Chonga, Abdallah Juma Abdalla alitaka kujua kwa nini makusanyo na matumizi hayo na baraza la wawakilishi kwa kuzingatia kuwa matumizi ya mapato hayo yanatumika Zanzibar,jee serikali haioni kuwa wakati umefika kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu Zanzibar kukagua matumizi ya taasisi hizo.

“Kwa nini baraza la wawakilishi kupitia kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika (PAC) haina nafasi ya kujua namna gani mapato na matumizi ya makusanyo hayo” alihoji Mwakilishi huyo wa Chonga Kisiwani Pemba.

Akijibu swali hilo la msingi Mzee alisema serikali inapowasilisha bajeti ya mwaka katika baraza la wawakilishi huwa inawasilisha pia mapato na matumizi ili yarithiwe na baraza hilo. Aidha mapato yanayokusanywa na taasisi za muungano zilizopo Zanzibar yanaingia katika mfuko mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na kutumiwa na wizara na taasisi za serikali ya Zanzibar.

Alisema kwa maana hiyo, taasisi zinazotumia mapato hayo kukaguliwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mapinduzi Zanzibar. Kwa taasisi za muungano ambazo hazitumii mapato yanayoingia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar taasisi hizo hukaguliwa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mheshimiwa Spika kama nilivyotoa ufafanuzi katika kifungu (a) na (b) baraza lako tukufu kupitia kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika inayo nafasi ya kujua namna gani mapato hayo yaliyokusanywa pamoja na matumizi yake, baraza hilo ndilo lililopewa dhamana ya kupitisha kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar makadirio ya makusanyo hayo na matumizi yake kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Wasio na uwezo wasamehewa

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema itawachukulia hatua walimu na viongozi wanaowanyanyasa na wanaowarejesha nyumbani wanafunzi wanaoshindwa kutoa michango ya shule kutokana na wazazi wao kukosa fedha za kuchagia elimu hiyo.

Sambamba na hilo imewataka viongozi hao kuwarejesha madarasani watoto wote ambao wamewafukuza baada ya kushindwa kwa wazazi wao kulipa fedha kwa kuwa serikali imeanzisha suala la kuchagia ili kuimarisha elimu na sio kuwalazimisha wanafunzi hata kama wazazi wao hawana uwezo huo wa kutoa michango mashuleni.

Naibu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Ali Hamad aliyasema hayo katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza Mjini hapa wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake, Mwanaidi Kassim Mussa ni kiwango gani cha kutoa wanafunzi mashuleni na kama waziri anafahamu kwamba kuna baadhi ya wanafunzi hurejeshwa nyumbani baada ya kukosa ada hiyo.

“Ni kosa kuwarejesha nyumbani wanafunzi ambao wazazi wao wameshindwa kutoa michango. Wizara imetoa muongozo juu ya ukusanyaji michango na kuwataka walimu wakuu, wajumbe wa kamati za skuli kutowarejesha nyumbani wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuchangia” alisema Zahra.

Alikitaja kiwango cha fedha ambacho wananchi wanatakiwa kuchangia kuwa ni kwa mwanafunzi wa Msingi 3,000, Sekondari kuanzia kidato cha kwanza na cha pili 5,000, Elimu ya pili kidato cha 3-4 shilingi 7,500, elimu ya Sekondari ya juu kidato cha 5-6 10,000, mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti 15,000 na ngazi ya Stashahada 20,000, michango ambayo yote hayo hutolewa kila mwaka.

Aidha alitoa wito kwa walimu na wajumbe wa kamati za skuli kuhakikisha kuwa wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuchangia hawarejeshwi majumbani na kuwashauri wazazi watimize wajibu wao wa kuchangia maendeleo ya skuli zao kwani michango yao inasaidia sana katika kufanikisha maendeleo ya watoto wao.

Katika suali lake mwakilishi huyo alitaka kujua ni hatua gani zimechukuliwa katika kuwadhibiti waalimu ambao huwanyanyasa wanafunzi ambao wazazi wao wameshindwa kuchangia fedha hizo ambapo Naibu huyo alisema hadi sasa wizara yake haijapokea malalamiko rasmi kutoka kwa wazazi ya kufukuzwa skuli kwa watoto wao kwa kushindwa kuchangia na hivyo hakujawa na haja ya kuchukua hatua za nidhamu kwa viongozi au walimu watakaothibitika kuwa wamewafukuza wanafunzi au kuwanyanyasa kutokana na wazazi wao kushindwa kuchangia fedha.

Sera ya vyuo vya mafunzo ipo jikoni

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kuanza matayarisho ya sera ya Vyuo vya Mafunzo ambayo itasaidia huduma bora kwa wanafunzi kwa lengo la kurekebisha tabia.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini katika kikao cha baraza la wawakilishi wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake, Ashura Sharif Ali, katika kikao hicho kilichoanza jana.

Alisema kuwa kuwa mpango huo unatarajiwa kuanza katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012 na kusema kuwa hatua zinachukuliwa za kuhakikisha mpango huo unakamilika kwa wakati.

Waziri Makame alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Vyuo Vya Mafunzo ni kurekebisha tabia kwa watu wanaohalifu sheria, lakini pia kuna baadhi ya wanafunzi wanaomaliza kutumikia vyuo hivyo hurejea tena katika vitendo viovu, jambo ambalo alisema hali hii hutokana na tabia ya baadhi ya watu.

“Mheshimiwa Spika naomba nimtowe wasiwasi mwakilishi kuwa hali hii haitokani na kupatikana kwa mafunzo yanayotolewa katika vyuo bali inategemea sana na tabia ya baadhi ya wanafunzi hao, na imebainika kuwa wengi wao wanaorejea makosa ni wale wanaotumikia Vyuoni katikavipindi vifupi”, alisema.

Katika suali lake Ashura alitaka kujuwa ni sababu zipi zinazopelekea kwa sasa wanafunzi wengi wanaomaliza kukuitumikia chuo cha mafunzo hurejea katika uhalifu, na je Serikali haioni kwamba ipo haja ya kufatilia ipasavyo mwenendo mzima ili kubaini matatizo yaliyopo na kuweza kukiimarisha kwa mujibu wa malengo yaliyokusudiwa.

Advertisements

One response to “Uchumi sio suala la Muungano

  1. MM NAOMBA KUU ATUTAJIE VYANZO VYA UCHUMI ZNZ HALAFU TUNOMBA KUWA KUNA MENGI TU YAKUONDOLEWA KTK MUUNGANO USIO NA TIJA NA ZNZ NA MNUKUU MOYO”SIO KUZIBA VIRAKA BALI KUUFANYA MPYA TENA NI UANZE MWANZO” IS OVERRRRRR MWISHO WA KUNUKUU tumechoka kusikia lugha za kisaniii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s