Bajeti imelenga kutatua kero


BAJETI IMELENGA KUTATUA KERO ZA ELIMU YA JUU: NAPE

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , amesema bajeti ya mwaka 2011/2012 imelenga kutatua kero zilizojitokeza kwenye elimu ya juu .Nape alisema hayo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu kwenye sherehe ya kuwaaga makada wa CCM waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha Kiisilamu mjini hapa.

Akitolea mfano uamuzi wa serikali kutoza kodi ya kukuza ujuzi, ambayo katika hiyo ya 2011/2012 mgawanyo wake umelenga kupeleka asilimia 4 kati ya 6 ya kodi hiyo kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu hivyo kuongeza uwezo wa bodi hiyo kuhudumia wanafunzi.

“mwaka jana kodi hii ilikusanya karibu sh. bilioni 200, na huwa inaongezeka kadri uchumi unavyokua, mategemeo kwa mwaka huu wa fedha , fedha hii itaongezeka hivyo kutenga aslilimia hiyo itasaidia sana kwenye kutatua tatizo la mikopo kwa elimu ya juu”Alisema Nape

Aliwataka wanafunzi kuwapuuza wanaopita na kusema hakuna kilichofanywa na serikali huku wakijua wazi kuwa kila mwaka hatua kubwa inapigwa katika kushughulikia kero mbalimbali za wananchi ikiwemo sekta ya elimu.

“kumekuwa na maneno mengi juu utaratibu wa kutoa mikopo na uendeshaji wa bodi yake, kwa kulitambua hili Rais Jakaya Kikwete ameunda tume ya kuangalia namna bora ya kushughulika na hili la bodi, tume ikikamilisha, na hili ongezeko la fedha bila shaka changamoto nyingi zitapungua” alisema Nape.

Katika sherehe hiyo Nape alikabidhi vyeti kwa makada 65 wa CCM waliohitimu chuo hicho na kupewa taarifa ya chama ya tawi la CCM la wasomi hao.Mjini Morogoro, Nape na msafara wake walipokewa na viongozi wa CCM mkoa huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa, Petro Kingu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s