Tupo pamoja mkuu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon, wakati alipokutana naye kwa mazungumzo ofisini kwake jijini New York, jana Juni 8, 2011 baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini hapa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameipongezaTanzaniakatika jitihada zake za kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI na akasisitiza kuwa,Tanzaniani nchi ya mfano licha ya kuwa jitihada zaidi zinatakiwa kuendelezwa katika kuhakikisha kuwa maambukizi mapya yanapungua katika kipindi hiki.

 

 

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

Anuani ya Simu: “MAKAMU” Ofisi ya Makamu wa Rais,
Simu Na.: 2116919 S.L.P. 5380,
Fax Na: 2116990Dar es Salaam.
TAARIFA KWA UMMA

 

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIADKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI MOON OFISINI KWAKE,NEW YORK
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameipongezaTanzania katika jitihada zake za kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI na akasisitiza kuwa,Tanzania ni nchi ya mfano licha ya kuwa jitihada zaidi zinatakiwa kuendelezwa katika kuhakikisha kuwa maambukizi mapya yanapungua katika kipindi hiki.
Akizungumza ofisini kwake katika majengo ya Umoja wa Mataifa jijini New York katika kikao chake na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Katibu Mkuu huyo anayemaliza kipindi chake cha kwanza na kutafuta kuchaguliwa tena katika kipindi cha pili alisema anashukuru sana nafasi ya Tanzania katika kupambana na vita dhidi ya Ukimwi na akaeleza kuwa masikitiko yake yapo katika maambukizi kwa watoto wanaozaliwa hivyo ni jukumu la ulimwengu na serikali zote kuhakikisha kuwa watoto wasio na hatia hawaambukizwi Ukimwi wakati wazaliwapo.

 

“Naumizwa sanana hali hii ya watoto wadogo kujikuta wamezaliwa na kisha kuambukizwa ugonjwa huu. Kwetu sie watu wazima unaweza kusema jambo hili tunalifahamu vema lakini kwa watoto hawa inauma kweli kweli,” alisema na kuongeza;
“Ndugu Makamu wa Rais naomba fikisha salamu zangu kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa anashiriki kikamilifu katika harakati za kuepusha maambukizi ya Ukimwi kwa akina mama na watoto. Mchango wake katika Umoja wa Mataifa sambamba na Waziri Mkuu waCanada Harper ni wa kujivunia na ninamtakia kazi njema zaidi.”

 

Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimwambia Katibu Ban Ki Moon kuwaTanzaniainaheshimusanakazi yake na kwamba tangu achaguliwe kushika wadhifa huo katika kipindi kinachomalizika mwaka huu, amekuwa rafiki mkubwa waTanzaniana hivyoTanzaniaiko nyuma yake katika kutafuta kuungwa mkono katika kipindi cha pili.

 

Tanzaniakupitia kwa Rais Kikwete ni moja ya mataifa ya kwanza kabisa kuunga mkono jitihada za kuchaguliwa tena kwa Ban Ki Moon na tayari mataifa kadhaa kutoka Afrika yameonyesha nia ya kumuunga mkono Katibu huyo katika kipindi cha pili. Kwa upande wake, Makamu wa Rais Dkt. Bilal alisisitiza kuwaTanzaniaitaendelea kushirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya Ukimwi na kwamba jitihada za kuhakikisha kuwa maambukizi mapya hayaongezeki bali kupungua katika kipindi hiki.

 

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais aliambatana na Waziri kutoka SMZ, Duni Haji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mahadhi Maalim na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Ombeni Sefue. Pia Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha Rose Migiro alihudhuria mkutano huo.

 

Imetolewa na: Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
08, 06, 2011,New York

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s