Ubakaji watoto wataka vitendo

Hawa ni watoto wa Kangagani Kisiwani Pemba umri wa watoto kama hawa ndio wanaosakwa sana na wabakaji, na tatizo la ubakaji hivi sasa limekuwa kwa kiasi kikubwa hasa maeneo ya Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba ndio anayoongoza katika ubakaji kwa mujibu wa takwimu za serikali

Kelele za ubakaji watoto zataka vitendo

Na Ally Saleh

Kauli nyingi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa na viongozi wetu
kuhusiana na suala la unyanyasaji na ubakaji wa watoto wa hapa kwetu
Zanzibar lakini matokeo yake yamekuwa si ya kupendeza na kwa hakika
yanatisha.

Takwimu zimekuwa za kwenda mbele kama wanavyosema vijana na kwa hivyo
kudhihirisha kuwa kauli hizo hazifanyi kazi ama kwa dharau, ukosefu wa
hatua madhubti au liwe liwalo kwa kuwa watu hwaogopi sheria
(impunity). Kwa ujumla kumeonekana haja ya kuwepo vitendo tena vitendo
vya kweli.

Halafu kwa jamii yetu hali hiyo inaendelezwa na kuendekezwa kwa sababu
ya kitu kinachoitwa muhali ambacho kwa kweli kimesaki katika jamii
yetu kiasi ambacho sio tu kinaturudisha nyuma lakini kwa kweli
kinazamisha jamii yetu.

Halafu pia mnasaba na hili ni suala la aibu ya kijamii ambapo matendo
kama hayo yanpotokea na kuhusisha wana familia basi kila juhudi
hufanywa kulisuluhisha suala hilo ndani kwa ndani na matokeo yake ni
kumdhulumu mtoto na kumpa fursa muharibifu arudie kosa lake tena.

Pia suala la aibu kwa familia hulazimisha familia kulimaliza suala
hilo na mkosaji ile habari zisieenee na kuna taarifa za watu kutakiwa
walipe fedha na kuna kesi moja hata mkosaji kuambiwa atoe dhahabu kwa
mtoto wa kike, astaghfirullah, lakini ndio yanayotkea.

Hivi karibuni Rais wa Zanzibar Dk Ali Muhammed Shein alilipigia kelele
suala la ubakaji wakati alipokuwa akijumuisha ziara yake ya Mkoa wa
Kaskazini Unguja na kuulaumu uongozi wa Mkoa huo kutomuarifu juu ya
tatizo hilo au kwa maana nyengine kulificha tatizo hilo.

Ila ukweli kuwa tatizo si la Kaskazini Unguja peke yake kwani ubakaji
umetandawaa katika jamii yote ya Kizanzibari ila linaloonekana ni kuwa
Serikali haizifanyii kazi tafiti mbali zinazofanywa na mashirika ya
kijamii au ripoti nyenginezo.

Ripoti ya Haki za Binaadamu ya Zanzibar ni chanzo kizuri sana cha
kupima hakimbali mbali ndani ya jamii na moja wapo ya haki inayovunjwa
bila kujali ni hii ya kudhulumu watoto na Kituo cha Sheria cha
Zanzibar ZLSC kinasaida sana katika kufichua mambo kama haya.

Wakati umefika sasa sio tu wanasiasa na viongozi kuhudhuria katika
uzinduzi wa ripoti kama hizi, lakini ripoti kama hizi zijadiliwe
katika mapana yake ili kuona matukio yaliotajwa ya uvnjifu wa haki za
binaadamu hayarudiwi au yanapungua na moja wapo ni hili la ubakaji wa
watoto wakike na kiume.

Mwaka huu Jumuia ya Mawakili Wanawake wa Zanzibar walizindua filamu
inayoonyesha ukubwa wa tatizo hili hapa kwetu Zanzibar na kupendekeza
hatua kadhaa za kuchukuliwa. Sijamuona mwanasiasa hatz mmoja katika
uzinduzi ule.

Ila Jaji Mshibe Ali Bakari alijikita katika suala hilo na kusema kuwa
wakati umefika wa Mahakama kuchukua uongozi wake kwenye sheria ili
watendaji wa makosa kama hayo wajue kuwa hapatakuwa na njia ya kupenya
kwa maovu na dhuluma zao kwa watoto au kike na wa kiume. Mkono wa
Mwendesha Mashtaka Mkuu ni muhimu sana katika hili pia, alisema na
kuongeza pia mbinu za utafiti wa masuala hayo lazima ziimarishwe kwa
Polisi.

Pia hivi karibuni Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd alizindua
kituo maalum kilichomo ndani ya eneo la Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa
ajili ya kushughulikia visa vya matendo hayo.

Hii sio tu ni hatua muhimu lakini ilikuwa ni ya lazima na iliyokuwa
ikisubiriwa kwa muda mrefu na tunataraji sasa kazi itafanywa kwa
umakini, uwazi na haraka ili kutoruhusu wakosaji wapenye kwa sababu ya
kukosa ushahidi.

Utafiti umekuwa ukionyesha kuwa mbali na ujinga wa majumbanikwamba
wazazi husuika katika kupoteza ushahidi kwa njia ya kuwasafisha watoto
kabla ya kuwapelekea hospitali baaa tendo la kudhulumiwa kingono,
lakini pia kumekuwa na rekodi kubwa ya usumbufu wa huduma watoto
wanapofika hospitali.

Tutumaini kuwa hili sasa litakuwa ni historian a haitatokea tena mtoto
amedhulumiwa Jumamosi aambiwe aletwe Jumatatu wakati shahawa, ambayo
ndio ushahidi mkubwa itakuwa imeshapotea.

Lakini pia umuhimu wa kuwa na mashine ya kupima Viini Nasaba DNA ni
muhimu. Maana zaidi ya ushahidi wa manii ya mkosaji lakini pi kuna
sehemu nyingi za mwili kama mate, damu, ngozi, malaika na nywele
nyengine ambazo zinasadia sana kuthibitisha utendwaji wa kosa.

Serikali ijikusuru ili mashine hii iwepo na kuzima mwanya wa wakosaji
kupenya kwa kukosekana ushahidi usio madhubuti ambao ni muhimu katika
makosa ya jinai. Kwa pahala tulipofika kifaa cha kupimia DNA sio suala
la starehe tena ( luxury) ila ni kifaa cha lazima kuwepo katika nchi.

Kuna haja ya hatua za makusudi kufanywa kugundua sababu za matendo
hayo kuongezeka katika jamii ambayo kijuujuu ni yenye upole na upendo
na ambayo pia imeshika dini kwa kiasi kikubwa.

Mabdiliko gani ya kijamii yameikumba jamii ya Zanzibar yaliosababisha
kuongezeka vitendo vya kinyama vinavyotokea ikiwa ni pamoja hata na
kuwahujumu watotow a kike walio na ugonjwa wa akili.

Kwa maana nyingine wakati tunatafuta dawa kwa wahalifu wa matend hayo
ni vyema bsi pia kuzuia uendeaji wa matendo hayo kwa kugundua sababu
zake na kuizifanyia dawa.

Ila lazima tuseme kweli kuwa moja katika taasisi sugu kunakotokea
matendo hayo ni madrassa zetu. Wakati umefika hivi sasa kwa Serikali
kuwa na mkono wake kupitia vyombo vyake kujua sifa na historia za
waalimu wa vyuo vyetu ili kunusuru matendo kama hayo. Lakini pia
Wizara ya Elimu inafaa ilisimamie vyema hili katika maendoe yake maana
mashuleni pia mambo kama hayo nako si haba.

Wito wangu ni Serikali kuwa na mkakati uliokamilia katika hili. Kila
taasisi ipewe majukumu yake na naamini itayokuwa kiongozi wetu ni
Wizara ya Maendeleo Wanawake na Watoto.

Mpango ufanywe kumuwesha mzazi na mtoto kuanza kujua viashiria vya
matendo kama hayo, mtoto ajengwe kujiamini kutoa taarifa kabla ya
tendo kutokea, na mbinu zifanywe ilijamii isiwwafiche watu kama hao
wanapoonekana katika mitaa yao au ikwia wanaishi miongoni mwao.

Matangazo na vipindi na hata vijarida kuhusu dhuluma hii viwe ni vitu
endelevu na kwa makusudi jambo hili lifanywe kuwa ni sekta mtambuka
(cross cutting) kwa sababu lisipochukuliwa hatua leo basi tutakuwa na
jamii goi goi na iliyoathirika kimwili na kisaikolojia.

Kwa mujibu wa elimu ya saikolojia ukiwa na kijana au msichana
aliyedhulimiwa kingono basi jambo hilo litabakia katikaakili yake
maisha. Na thari ni mbili ama kumkosa katika matendo mema au yeye
mwenyewe kuwa katili kwa wengine na kwa hivyo vitendo hivyo kuwa
endelevu katika jamii.

Ndipo nikasema makaripia juu ya ubakaji wa watoto yasio ni kauli tupu
wala zisiwe kauli za kupita, wala wasyiwe ni makeke ya kisisa maana
jamii inaumia sana katika hili.

Vitendo vinahitajika sana na jamii kushirikishwa. Kauli ya Rais na
Makamo wa Pili ni dalili kuwa Serikali iko tayari na jamii nayo
inapaswa ijipange ilie pande hizi zishirikiane maana wanaoumia ni
ndugu, watoto na kizazi cha taifa hili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s