SMZ yaahidi kutunza mazingira

Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakari akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imejidhatiti kuyakabili matatizo na athari za kimazingira zilizojitokeza na kulinda harakati za kimaendeleo ziendane na matakwa ya kimazingira ili kuepusha athari zisitokee hapo baadae.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakari, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.

Waziri Bakari alisema kwa miaka mingi sasa duniani inakabiliwa na matatizo kadhaa ya kimazingira yanayotokana na matumizi mabaya ya mali za nchi kavu na baharini na kuwataka wananchi kuwa makini na kulinda mazingira yao.

Miongoni mwa matatizo hayo ni ukataji ovyo wa misitu uvuvi haramu, utupaji mbaya wa taka taka ngumu zikiwemo za vifaa vya vya umeme, umwagaji ovyo wa uchafu unaotokana na kemikali matatizo yote hayo yanatokana na harakati mbali mbali za maisha ya watu katika kujitafuitia riziki na maendeleo kwa ujumla.

Serikali katika kukabiliana na matatizo yaliyojitokeza ni pamoja na kuchukua hatua ya kuunda idara ya mazingira na kutayarisha sera na Program ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1992 na kuipitisha sheria yake kwa maendeleo ya kudumu.

Alisema hatua hiyo inamanisha kuwa mipango yote ya kimaendeleo na kiuchumi ni lazma iende sambamba na uhifadhi wa mazingira.

“Wazee wetu waliotangulia walikuwa na tabia ya kupanda miti wamepanda miembe, minazi, na mengine ambayo kwa hakika hivi sasa ndio tunayojivutia” alisema Waziri Bakari.

Hata hivyo alisema jambo la kushangaza kizazi cha sasa kimekuwa ni watumiaji wazuri wa ile miti ambayo wazee walipanda kwa tabu na kuitunza kwa kujua umuhimu wake.

“Tena kwa bahati mbaya tumekuwa tunapenda kukata miti ovyo kama hatutakuwa makini siku za karibuni tutaifanya nchi yetu kuwa jangwa”.Alisema waziri huyo.

Aidha alisema maisha ya kila siku hayana budi kwenda sambamba na mfumo wa kuhifadhi na kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kudhibiti maji machafuna na taka taka.

Pamoja na mfumo bora na salama wa matumizi ya nishati na kuacha kuchukua mchanga ovyo,kuhifadhi vyanzo vya maji, kupanda miti na kuitunza ,kuzuiya uvuvi haramu na kuihusisha mipango na miradi ya maendeleop na hifadhi ya mazingira.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani imebebe ujumbe “Misitu ni asili ya maisha yako” ambayo inalenga juu ya njia muafaka za uvunaji rasilimali za misitu pamoja na kuhifadhi ili kuwa na maisha bora.

Jumla ya miti kadhaa imepandwa ikiwa ni ishara ya utunzaji wa mazingira katika maeeo mbali mbali kwa Unguja na Pemba.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s