Maalim Seif ateta na UAMSHO

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Amiri wa Jumuiya, Sheikh Msellem Bin Ally na Naibu Amiri, Sheikh Azzan Khalid Hamdan walipofika ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza nchini wanafanyiwa tathimini ili kuweka mazingira mazuri yenye kufuata mila utamaduni na silka katika sekta hiyo.

Sambamba na hilo suala la misamaha ya kodi inaotolewa na serikali kwa wawekezaji hao itabidi liangaliwe upya kwa lengo la kuinua uchimi kwani misahama inaotolewa ni mikubwa kwa wawekezaji hao wanaokuja kuwekeza jambo ambalo linapunguza mapato kwa serikali.

Kauli ya Maalim Seif imekuja wakati kukiwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbali mbali kuhusiana na sekta ya utalii inavyochafua mila na utamaduni wa mzanzibari.

Maalim Seif alikuwa akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) waliofika jana ofisini kwake Migombani, kwa kusalimiana naye, na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kuwa makamu wa kwanza wa rais pamoja na kubadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali yanayoihusu jamii ambapo kwa sasa kumekuwepo na manung’uniko mengi juu ya utamaduni wa Zanzibar kuharibika.

Alisema suala la uharibifu wa mazingira unaotokana na maendeleo ya utalii, unaokuwa siku hadi siku lakini alisema serikali italishughulikia ipasavyo suala hilo kwa wale wenye dhamira ya kuwekeza miradi yao katika sekta hiyo itafaniwa tathmini juu ya uchafuzi wa mazingira na kwa ile itakayoonekana kuchafua mazingira, haitaruhusiwa kabisa.

Aliwathibitishia Mashekhe hao kuwa katika dhana ya kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii, kumekuwepo upungufu mkubwa wa misamaha ya kodi inayotolewa lakini hivi sasa chini ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa serikali iko makini sana katika suala hilo kwa kutambua athari zake katika kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumzia suala la watembezaji wageni ambao hupotosha historia ya Zanzibar kutokana na watembezaji hao kuwa ni wageni Maalim Seif alisema suala hilo analifahamu na ni lazima hatua za kulisawazisha zichukuliwe ili wageni wanaokuja wasipotoshwe na wapewe historia iliyo sahihi.

Alisema kuna umuhimu kwa Serikali kupitia wizara yake ya utalii kuhakikisha watembeza watalii wote wanafahamu historia ya Zanzibar, ili kuepuka upotoshaji kwa wageni.

Akigusia suala la madawa ya kelevya, Maalim Seif alisema Serikali imekuwa ikiendelea na juhudi ya kulitafutia ufumbuzi suaala hilo na kwa kiasi limeanza kupata mafanikio ya kupungua kwa vitendo vya uhalifu katika baadhi ya mitaa hapa Unguja.

Alisema tatizo hilo linachangiwa zaidi kwa kuwa nchi Zanzibar ni nchi ya Visiwa, hivyo kuwa na milango mingi ya kuingizia bidhaa hiyo haramu na kuwathiri vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya taifa la baadae.

Serikali inakusudia kuliingiza somo la madawa ya kulevya katika mitaala mashuleni ili wanafunzi waweze kuelewa athari za madawa ya kulevya na hatimae kujiepusha nayo kwani vijana wengi wanaonekana kuwa ni watumiaji wa madawa ambao baadhi yao huanza wakiwa wadogo mashuleni.

Aidha Makamu wa Kwanza wa Rais alisema bila ya kuingilia uhuru wa Mahakama, serikali itaendelea na juhudi za kuzitaka taasisi zinazosimamia sheria kufanyakazi kwa uadilifu ili kufikia lengo la kuwaondolea kero mbali mbali wananchi.

Amesema kumekuwepo na tatizo la kutafsiri sheria katika Mahakama, hali inayotokana na baadhi ya watendaji wake kutokuwa waaminifu na kukosekana uadilifu kwa kufanyakazi kulingana na utashi au maslahi yao binafsi na hivyo kusababisha malalamiko mengi kuishia bila ya kupata suluhu sahihi.

Maalim Seif alilazimika kutoa kali hiyo ya watendaji wasio waaminifu wa mahakama kufuatia malalamiko yaliotolewa na viongozi hao wa kidini juu ya kushamiri kwa vilabu vya pombe (baa) katika maeneo mbali mbali yanaoishi watu, (yakiwemo yale ya ibada na shule) kinyume na sheria za Bodi ya vileo inavyoelekeza.

Viongozi hao walilamikia mahakama inavyofanya kazi zake bila ya kuzingatia sheria ambapo baadhi ya malalamiko ya wananchi katika maeneo yao wenye vilabu vya pombe hutolewa hukumu lakini na kuwekewa pingamizi mahakamani lakini mahakama hazifanyi wajibu wake na badala yake wananchi kupandwa na hasira na kuchukua sheria mikononi mwao jambo ambalo limeshawahi kujitokeza katika baadhi ya sehemu za Zanzibar.

Naibu Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Azzan Khali Hamdan alisema baadhi ya majaji wamekuwa na tabia ya kutoa maamuzi ya kesi za aina hiyo kulingana na utashi wao unavyowasukuma, bila ya kuzingatia sheria zilivyo.

Naye Amiri wa jumuia hiyo ya Uamsho, Sheikh Mselem Bin Ally alisema ipo haja serikali kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyafanyia kazi kwani inaonekana baadhi ya taasisi hazifanyi wajibu wake na hivyo kusababisha malalamiko ya wananchi kulimbikizana na baadae wananchi kuchukua sheria mikononi jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Viongozi hao wamezunguzia mambo mbali mbali anayoikabili jamii kwa sasa na kutaka serikali kuyashuhulikia malalamiko ya wananchi ili kuepusha migongano isio na lazima kuwepo katika jamii kwani bila ya kufanya hivyo mbali ya wananchi kuyokuwa na imani na serikali yao ambayo wamejenga matumaini makubwa lakini pia itapelekea kurejesha chuki na migogoro katika ya serikali na wananchi.

Wamesema ili kuepusha hilo lisitokee ni busara serikali ikalichukuliwa suala hilo kwa umakini mkubwa na kutatua kero za wananchi kwani hivi sasa inaonekana kuwepo kwa malalamiko ya aina mbali mbali ikiwemo suala la kutoheshimiwa mila na tamaduni za mzanzibari, migogoro ya ardhi inayochangiwa na watendaji wa serikali na hata kukithiri kwa kumbi za starehe na vilavu vya pombe kinyume na sheria.

Advertisements

One response to “Maalim Seif ateta na UAMSHO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s