Hatuna mvua za msimu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bw Robert Cunnane aliyefika ofisini kwa Balozi Seif, Vuga Mjini Zanzibar kumsalimia.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa mabadiliko yasiotabirika ya hali ya hewa ulimwenguni yamepelekea wakulima wa Zanzibar kutotegemea sana mvua kwa kilimo chao.

Alisema kilimo cha umwagiliaji ndio utatuzi muwafaka na wa kudumu wa tatizo hilo kwa kuwa utawawezesha wakulima kuwa na uhakika wa kuvuna mazao ya kutosha kutoka katika mashamba yao.

Kauli hiyo aliitoa katika mazungumzo yao na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bw. Robert Cunnene aliongozana na mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji Bw. Thomas Hobgood huko Ofisini kwake Vuga.

Alizungumzia suala la mradi wa kujitosheleza na chakula, Balozi Iddi alisema kuwa mchele ndio chakula kikuu cha Wazanzibari ambacho asilimia 80 huagizwa kutoka nje kutokana na uzalishaji wake mdogo wa ndani.

Kwa hivyo, alieleza jitihada za Serikali katika kuimarisha kilimo hicho kwa njia ya umwagiliaji na kufurahishwa zaidi kwa kuona USAID iko tayari kusaidia mradi huo.

Naye Mkurugenzi Bw. Robert Cunnene alisema tayari wameshaanza kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Kilimo ili kuona miundombinu ya kilimo hicho kwa lengo la kurekebisha au kujenga mipya.

Ambapo mtaalamu Bw. Thomas Hobgood alisema zaidi ya kilimo cha umwagiliaji pia wataendelea na miradi myengine ya kilimo ikiwemo kuimarisha kilimo cha mboga mboga ambacho kina soko katika hoteli za kitalii.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dr. Khalid Salum Mohamed na Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani visiwani Zanzibar Bw. David L. Scott.

Katika hatua nyengine Zanzibar inatarajiwa kufaidika na Mradi wa ‘Feed the Feature’ unaofadhiliwa na Serikali ya Marekeani kupitia Shirika Maendeleo la nchini Marekani (USAID), ambao umetenga Bilioni 3/= na Tanzania itapatiwa dola za kimarekani milioni 300.

Waziri wa Kilimo na Mali Asili Mansour Yussuf Himid aliiambia Zanzibar Leo jana baada ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Shirika hilo unaosimamia Kilimo na uhifadhi wa chakula ulioongozwa na Thomas Hobgood.

Alisema fedha hizo Zanzibar itafaidika nazo kwa kuelekezwa katika sekta ya Kilimo kwa vile Shirika hilo inakusudia kuzitenga mbali na zile ambazo zitatumika kwa miradi iliopo Tanzania Bara.

Alisema maeneo ambayo wanakusudia kuyaangalia baada ya fedha hizo kuingizwa ni katika kuimarisha kilimo cha mpunga, mahindi, mboga mboga na lishe.

Waziri Mansoor, alisema hatua ya Shirika hilo kuipatia Zanzibar sehemu ya fedha hizo ni miongoni mwa muendelezo wa mafanikio ya serikali ya awamu ya saba katika kusukuma mapinduzi ya kilimo.

Alisema dhamira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein ni kuona Zanzibar inapiga hatua katika sekta ya Kilimo ili kuleta mabadiliko na kuja kwa Shirika hilo kutaongeza sehemu ya malengo hayo.

Waziri huyo, aliahidi kuona kuwa Wizara yake inasimamia vyema shughuli za shirika hilo kupitia sekta hiyo baada kufunguliwa kwa Afisi yao hapa Zanzibar.

Thomas Hobgood, wa Shirika USAID katika sekta ya uhifadhi wa Chakuna na Kilimo, alisema kuwa dhamira ya shirika hilo ni kusaidia Zanzibar iweze kujitosheleza na chakula kwani bado kuna maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi.

Alisema Shirika lao kwa kutumia fedha ambazo Tanzania imetengewa itahakikisha kuwa Zanzibar inaipa umuhimu wa pekee kwa kuiangalia miradi iliomo katika kilimo na kujitosheleza kwa chakula na kuondokana na upungufu.

Alisema suala la kuongeza hali ya chakula ni moja ya jambo la msingi kwa vile hivi sasa kumekuwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo kutokea kwake hayatabiriki.

Kutokana na umuhimu wa kufanikisha hayo Hobgood, alisema shirika lao linakusudia kufungua Afisi hapa Zanzibar ikiwa ni hatua ya kuona kuwa wanasimamia vyema shughuli ziliopo ndani ya shirika hilo kwa wananchi wa Zanzibar.

Hata hivyo Mwakilishi huyo alisema kuwa katika kuyapa kipaumbele mambo yaliomo katika sekta hiyo watahakikisha kuwa wanawake wanapewa kipaumbele muhimu kwenye miradi hiyo.

Mapema wataalamu wa shirika hilo walieleza umuhimu wa Shirika hilo kuona linaendelea kuisaidia Zanzibar ikiwemo kuinua sekta hiyo ya Kilimo kutokana na kuwa bado inamahitaji makubwa ikiwemo ya miundo mbinu katika kilimo cha umwagiliaji.

Walisema tayari hivi sasa kumekuwa na mafanikio mbali mbali katika sekta hiyo ya Kilimo lakini yanakabiliwa kutatuliwa kwa changamoto zikiwemo za kuongeza uzalishaji wa chakula, kuinua vikundi vya wakulima wa mazao ya baharini pamoja na kuinua hali za wakulima.

Tanzania kwa miaka kadhaa imekuwa ikifaidika na miradi ya Shirika hilo ambapo Zanzibar ikiwa miongoni mwao hasa katika sekta ya Elimu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s