Serikali haitambagua mtu

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wakiwemo pia wanafunzi, katika eneo la kwale gongo, alipotembelea barabara ya Konde-Wete, akiwa katika ziara ya kutembelea Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuona mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa jukumu lake kubwa ni kuwatumikia wananchi wote wa Unguja na Pemba bila ya ubaguzi.

Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kulikagua bonde la mpunga la Mziwanda ambalo limeathirika na maji ya bahari kutokana na uharibifu wa mazingira ukiwemo ukataji wa mikoko ambayo ilkuwa inazuwia maji hayo ya bahari kuingia katika bonde hilo.

Akizungumza na wakulima wa bonde hilo, Dk. Shein aliwaeleza kuwa kilimo cha kijembe kongoroka mpini haina nafasi hivi sasa na lengo kubwa la serikali ni kuwasaidia wakulima wote wakiwemo wakulima wa muhogo, viazi, mikarafuu pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuhakikisha wanapata mbegu bora, dawa, mabwana shamba pamoja na matekta na pembejeo nyenginezo.

Dk. Shein alitoa nafasi kwa viongozi aliofuatana nao wakiwemo Mawaziri husika kueleza lengo la serikali kupitia Wizara zao katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ambao wote kwa walieleza mikakati liyowekwa ikiwemo kujenga ukuta wa zege paoja na kuutumia mradi wa TASAF 3.

Kwa upande wake Dk Shein alieleza kuwa hatua ya kwanza itakayochukuliwa ni kupeleka wataalamu katika bonde hilo ili wao watoe ushauri unaofaa ktika kutafuta njia za kulitatua tatizo hilo kwa mashirikiano ya Wizara kwa kuwatumia wataalamu wao.

Alisema kuwa ayo yatafanywa na serikali yenyewe na kuwasisitiz wananchi kutoharibu mazingira kwani athari zake ni kubwa sana.

Akiwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maeneo huru ya vitega uchumi huko Michewei, Dk. Shein aliwaeleza wananchi wa Micheweni kuwa azma ya serikali anayoiongoza ni kuwapelekea maendeleo wananchi wa Micheweni na si vyenginevyo na kusisitiza kuwa pato itakalopatkana ltawasaidia wao pamoja na wananchi wote wa Zanzibar.

Katika maelezo yake pia, Dk. Shein alisisitiza wazee wa Micheweni kwuasomesha watoto wao kwa bidii kwani kukamila kwa eneo hilo na kuanza kazi kutahitajia wafanyakazi ambao watakuwa na elimu, hivyo hawaa budi kuendeleza sekta hiyo.

Dk Shein pia, aliwafahamisha wananchi wa kijiji hicho juu ya Mfumo wa Serikali anayoingoza sanjari na njia zilizotumika katika kuwapata viongoi waliomo katika serikali hiyo.

Akiwa katika eneo la shamba la Mtama Mjini Wingwi, Dk. Shein alisisitiza kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Kilimo na Wizara nyengine muhimu zitahakikisha zinatoa msaada mkubwa kwa wakulima hao wa mtama.

Dk. Shein alitembelea ujenzi wa barabara ya Wete-Konde yenye urefu wa kilomita 1.49 ambayo inajengwa na Kampuni ya MECCO ya hapa hapa nchini ambapo kwa maelezo ya Waziri wa Mawasiliao Hamad Masoud alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo uakamilika miezi kumi jayo.

Waziri huyo pia, aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa serikali imeamua kupunguza matumizi kwa kutengeneza njia ya mkato badala ya le ya mwanzo ili kupunguza gharama za ujenzi na kuwaahidi wananchi hao kuwa hata ile barabara ya mwanzo nayo itajengwa na kuwekwa lami hivyo wasione kwua wamedharauliwa.

Kwa upande wake Dk. Shein alisema kuwa lengo la serikali ni kuwatengenezea miundombinu wananchi zikiwemo baabara kwa madhumuni ya kuweza kusafirisha mazao, wagonjwa na kuwasaidia wananchi wenyewe katika shughuli zo za maendeleo. Alisema kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kujiandaa na karne ya 21.

Dk. Shein pia, aliwaeleza wananchi na wananfunzi waliofika katika eneo la Pwale Gongo kuwa serikali imeamua kwa makususdi kuwasaidia wakulima wakiwemo wakulima wa mikarafuu pamoja na kuwasaidia wanafunzi kwa kuimarisha sekta ya elimu.

Pia, Dk. Shein litembelea ujenzi wa Tangi la juu la kuhifadhia maji Gongoni ambapo mradi huo mara utakapomaliza utawasaiida kwa kiasi kikubwa wananchi wa Shehia za Kiuyu pamoja na Maziwangombe.

Aidha, Dk. Shein alielezwa kuwa serikali imo katika hatua za uchmbaji wa visima ambapo umalizika kwake vitaongea nguvu kwenye tangi hilo na kupelekea wananchi wote wa Micheweni kupata maji ya uhakika.

Dk. Shein pia, alifika eneo linalochimbwa matofali huko Kiuyu Mbuyuni na kujionea athari za uharibifu wa mazingira ambapo wachimbaji wa eneo hilo licha ya kuendelea kuchimba matofali hayo lakini wameonesha welew juu ya taratibu za uchimbaji ambapo mara wanapomaliza hufukia mashimo yao pamoja na kupanda mii ya kudumu na pia uchimbaji wao hauende chni sana.

Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein ameitak Wizara husika kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wa Kangagani.

Pia, Dk. Shein alitemebele kituo cha redio jamii Micheweni na kuelezwa kuwa kituo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa wakaazi wa Michewni na vitongoji vyake juu ya elimu ya mazingira, kilimo, afya na mazingira, ufugaji na uvuvi na kupongeza juhudi zinazochukuliwa.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alipata nafasi ya kuzitembelea skuli mpya za Sekondari Wilaya ikiwemo skuli Sekondari ya Konde na Skuli ya Sekondari ya Chwaka ambazo zote kwa pamoja ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi wa Septemba ambapo Dk. Shein aliwasisitiza wanafunzi kujitahidi kusoma ili waje kuzitumia vyema skuli hio za kisasa.

Katika hatua nyengine Dk. Shein amepongeza juhudi za wananchi wa Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba katika kujiletea maendeleo na kueleza kuwa serikali anayoiongoza itaendelelea kuunga mkono juhudi hizo.

Dk. Shein aliyasema hayo katika ziara yake inayoendelea katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo jana alianza kutembelea Wilaya ya Wete kwa kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo barabara pamoja na shughuli za maendeleo wanazofanya wananchi zikiwemo za kilimo, ufugaji pamoja na kuangalia athari za uchimabaji matofali.

Katika maelezo yake, Dk. Shein akizungumza na wakulima wa Bonde la Mpunga la Mangwena, alieleza kuwa jitihada za wakulima hao kaziona na kuwaaka waelewe kuwa uharbifu uliotokana n ujenzi wa barabara Wete-Gando haukuwa wa makusudi.

Alisema kuwa uharibibifu huo umetokana na matokeo ya kazi hatua ambayo mara baada ya kukamilka barabara hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa kusafirishia bidhaa zao, tawarahisishia wao wenyewe usafii pamoja na kuweza kimarisha sekta ya biashara, kilimo, uvuvi na nyengine.

“Hii imetokezea kwa bahati mbaya ambapo sababu yake ni kutokana na mvua na kuwataka wananchi hao kuendelea kuvuta subira. Pia aliwaeleza kuwa miti itapandwa pembezoni mwa barabara hiyo ili kuzuia mmongonyoko.

Aidha, Dk. Shein alitembelea shamba la ushirika, Mzabibo Junguni na kuangalia kilimo cha mirafuu,mihogo na midalasini na kueleza kuwa serikali ina mpago kabambe wa kuliimarisha zao la karafuu.

Aliwaeleza wakulima wa ushirika huo kuwa serikali itawaunga mkono ikiw n pamoja na kulitatua tatizo lao la umeme, mbolea, mbegu, dawa pamoja na wataalamu na kuahidi kuchangia shilngi milioni mbili.

Dk. Shein pia, aliwataka Wizara ya Kilimo kufanya jitihada za kuhakikisha watu kutoka maeneo bali mbal ya Zazibar wanakwenda kujifunza kilimo cha mikarafuu katika shamba hilo kutokana na kupiga hatua kwa kiasi kikubwa.

Akiwa Junguni Dk. Shein alizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi na kuwaelea kuwa madhumuni ya seikali ni kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaahidi kuwa ujenzi wa barabara yao ambao Rais mstaafu Dr. Amani Abeid Karume alianza nayo yeye ataendelea nayo na kuukamilisha.

Alisema kuwa tayari serikali imeshatenga fidia kwa ajili ya walioathirika na ujenzi wa barabara hiyo na kuwataka wananchi hao kuvumilia kwani watakao fanikiwa ni wengi na kueleza kuwa anamatarajio makubwa kuwa Gando taendelea na tangara wakati mfupi ujao.

Alieleza kuwa huduma zote muhimu zitapelekwa katikakijiji hicho ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya mazingira yatabadilishwa ambapo biashara, klimo na mambo mengineo yataimarishwa.

Pia, Dk. Shein aliweka jiwe la msingi skuli ya msingi Kizimbani na kutoa pongezi kwa skuli hiyo kutokana na matukio mazuri ya mitihani na kuwataka wanafunzi kuendelea kusoma na kupasi zaidi mitihani yao.

Dk. Shein alitoa pongezi kwa skuli hiyo iliyojengwa mwaka 1949 ambapo wakati huo kiitwa Catholic Mission School kwa kuendeleza historia yake ambapo Dk. Shei alifanya harambee iliowahusisha viongozi alofuatana nao wakiwemo Mawaziri Manaibu Waziri, Katibu Kiongozi, Wabunge na Wawakilishi pamoja na Mkuu wa Mkoa ambapo Shilingi Milioni kumi zilipatikana ambapo Mama Shein alichangia shilingi milioni mbili na Dk. Shein alichangia shilingi milioni tatu na nusu.

Akitoa maelezo, Waziri wa Miundommbinu na Mawasilano Hamad Masoud, alisema kuwa Wizara yake itahakikisha tatizo hilo inalifanyia kazi na kueleza kuwa kwa upade wa dongo ulioigia katika baadhi ya mashamba utafanyiwa kazi pamoja na kujengewa banda lao.

Aidha, alieleza kuwa barabara ya Wete-Gando inayojengwa na Kampuni ya MECCO hivi sasa imesita kutokana na tatizo la mvua lakini alieleza mara baada ya kumaliza mvua barabara hiyo itaendelea kujengwa.

Alisema kuwa tatizo ulipaji fidia nalo linaendelea licha ya kuwa fedha zinazohitajika ni Shilngi Biloi nne ambazo ni nyingi lakni wananchi wataendelea kulipwa fidia ambayo pia inahusisha umeme, maji na vipado vya wananchi.

Akiwa katika shamba la ngombe wa kisasa, Kisiwani kwa Bint Abeid Dk. Shein alisema kuwa ni vyema kwa wafugaji kuendelea kuzidisha uzalishaji sanjari na kujitangaza na kuwasisitiza wananchi kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa zetu zinazozalishwa na wafugji na wakulima wa hapa hapa Zanzibar.

Alisema kuwa juhudi za serikali zinaedelea kuchukuliwa katika kuhakikisha soko la bidhaa zao linapata nafasi kwa kuitaka Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kuliafutia ufumbuzi suala hilo.

Alisema kuwa serikali imeamua kwa makusudi kuhakikisha wakulima wanalima na wanapata tija ikiwa ni pamoja na kuwapatia wakulima mbegu bora, dawa, pembejeo na mambo mengie muhimu.

Dk. Shein alimalizia ziara yake Wilaya ya Wete ambapo aliangalia athari za mazingira katika eneo linalochimbwa matofali a kuwataka wananchi wanajishughulsha na kazi hiyo kujali mazingira wanayoyafanyia kazi kwani athari zake ni kubwa na fedha nyingi hupote katikakuirejesha ardhi hali yake ya zamani.

Alisema kuwa serikali iko tayari kuwawezesha wananchi hao ili kuepukana na uharibifu wa mazingira unaofanyika lakini bado haijawa na uwezo na kuwasisitiza kuwa maandalizi ya mikataba ya uchimbaji yaliofanywa yamefanywa kwa maslahi yao kwani hilo ni suala la kitaalamu.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa hakuna mtu atakaewaondosha kwa nguvu katika shughuli zao hilo lakinikubwa wazingatie mazingira na nia ya serikali ni kutengeneza kwan hatua hiyo pia, ni kwa ajili ya kuwatengenezea na vizazi vijavyo mazingira bora.

Nao wananchi na viongozi wa Mkoa huo wakiwemo wale wa Wilaya ya Wete walitoa pongezi kwa Dk. Shein kufuatia ziara yake hiyo na zile abazo mekuwa akizifanya mara kwa mara za kukagua shuhuli za maendeleo na kueleza kuwa ni mwanzo mzuri.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s