Tutainua viwango vya elimu

MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema licha ya changamoto zilizopo, Serikali ya Umoja wa Kitaifa imenuwia kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kuinua viwango vya elimu mashuleni.

Kauli hiyo ya Maalim Seif imekuja wakati wa mazungumzo yake na ujumbe wa viongozi wa Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithinashir Muslim, ulioongozwa na Rais wa Dunia Dk. Asgara Meladina aliyemtembelea jana ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar.

Alisema sio siri kwama serikali inakabiliwa na matatizo mbali mbali lakini kwa kushirikiana kwa pamoja serikali imeona haja ya kutoa kipaumbele katika nyanja tofauti ikiwemo uimarishaji wa kiwango cha elimu hapa Zanzibar kwa kuwa elimu ndio msingi ya mafanikio.

Maalim Seif alisema mafanikio makubwa katika sekta hiyo yameanza kupatikana na kufikia malengo ya Melenia kwa kuwapatia nafasi za masomo watoto wote wenye umri wa kwenda shule, ila tatizo liliopo ni uimarishaji wa kiwango cha elimu.

Aidha alisema lengo la serikali ni kuinua hali ya maisha ya wananchi wake lakini inakabiliwa na changamoto kubwa ya umasikini kama zilivyo nchi nyingine za dunia ya tatu lakini alisema suala hilo serikali inakabilian analo na ufumbuzi wake utapatikana kwa kuwa ni matatizo ya kuja na kuondoka na sio ya kudumu.

Katika ujumbe uliofika kuonana naye ukiongozwa na Rais wa Dunia Dk. Asgara Meladina Maalim Seif aliwashukuru na kupongeza azma ya Jumuiya hiyo katika kusaidia maendeleo ya elimu Zanzibar na kuomba mashirikiano zaidi kati ya Serikali na Jumuiya hiyo, hususan katika nyanja za Teknolojia ya habari na kompyuta.

Serikali nayo imetilia mkazo sekta ya afya kwa kuwa n sekta moja wapo muhimu kwa wananchi wanaohitaji huduma za afya ambapo lengo la serikali ni kuwafikia wananchi wote wa Unguja na Pemba kupata huduma hiyo muhimu.

“Mbali na sekta ya elimu lakini pia sekta ya afya ni mhimili mwengine kwa wananchi ambao wanahitaji matibabu bora, lazima serikali jikite katika huduma bora kwa sababu unapowapa huduma bora wananchi wataweza kuishi vyema na wananchi wakiwa na afya njema ndipo taifa linapopata mafanikio katika malengo yake kwa kuwa kazi zitafanyika lakini unapowanyima wananchi huduma ya afya, afya zao zitadorora” alisema Maalim Seif.

Jumuiya hiyo pia imepongezwa kwa kujenga kliniki na kutoa huduma bora za afya kwa njia za kuwasaidia wananchi na sio ya kibiashara.

Hata hivyo Maalim Seif alitumia fursa hiyo kuwakaribisha kwa mara nyengine tena Jumuiya hiyo kuanzisha miradi yoyote itakayosaidia kuimarisha hali ya wananchi kijamii, ikiwemo uendelezaji wa huduma za maji nchini, ambapo zinazokabiliwa na miundo mbinu duni na iliochakaa.

Makamu wa kwanza wa Rais, alisema Serikali inahitaji kiasi cha Dola Milioni 123 kuweza kumaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama Unguja na Pemba.

Rais wa Dunia wa jumuiya hiyo Dr. Asgara Melodina, alisema Jumuiya yake inalenga kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika sekta za elimu, afya na huduma nyingine za kijamii hapa Zanzibar.

Alisema Jumuiya hiyo inalenga kujenga kliniki kubwa itakayotoa huduma mbali mbali za afya bila ya kuiendeshwa kibiashara ili kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa Zanzibar.

Katika hatua nyengine, Makamu wa kwanza wa Rais amewataka viongozi wa dini nchini, kuwaelimisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alisema hayawasaidii, isipokuwa kuwaangamiza vijana.

Akizungumza na mchungaji Bunga Edward wa Kanisa la Seventh Adventist Church, ofisini kwake Migombani, Maalim Seif alisema hatua hiyo haina budi kwenda sambamba na urejeshaji wa maadili aliyosema yameporomoka na kupelekea kuibuka kwa vitendo vingi viovu ikiwemo unyanyasaji wa watoto.

Ameitaka Serikali, wazazi na viongozi wa Dini zote nchini kushirikiana na kila mmoja kuchukua nafasi yake katia kupiga vita maovu.

Kwa upande wake Mchungaji Edward aliipongeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa na zile zilizotangulia kwa kutoa uhuru wa kutosha na kuabudu.

alisema kuwepo kwa amani na utulivu nchini ni dalili nzuri na kupongeza kwa kuundwa wa serikali yenye mfumo wa Umoja wa kitaifa, ambapo alisema amani iliyopo ni matunda yanayohitaji kueziwa kwan bila ya amani hakuna maendeleo yoyote nchini.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s