Asili yetu ni Zanzibar

Kiongozi wa ‘wazanzibari’ wageni kutoka Afrika Kusini, Ismail Fraser wenye asili yao hapa Zanzibar akiwa na wenzake waliofika kwa ajili ya mkutano wa ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti na Mtandao katika nchi za eneo la Bahari ya Hindi (ZIORI) Franser ameelezea furaha yake ya kufika Zanzibar, nyumbani kwao kwa asili, kwa mara ya kwanza, na kushukuru taasisi ya ZIORI kwa kuwazinduwa na kuwaleta kwao.

WATAALAMU wa siasa za Kiamataifa na utamaduni katika maeneo ya nchi za bahari ya Hindi (Indian Ocean) wamekusanyika mjiniZanzibarkuzungumzia maendeleo ya eneohilo  katika kipindi hichi cha kasi ya mabadiliko makubwa duniani.
Hii itakuwa ni mara ya pili kongamano kufanyikaZanzibar, lakini kivutio pekee mwaka huu ni ujio wa ‘Jamii ya wazanzibari’ wanaoishi Afrika ya Kusini ambao asili ya wazee wao ni visiwa vyaZanzibar.
Wengi wa Wazanzibari hao, wazee wao walikwenda katika karne ya 19 wakiwa ni watumwa, wanaishi katika mji waDurban ulio pembezoni mwa bahari na mji uliopokea watu wengi pia kutoka Ulaya na hata Bara laAsia.
Professa Abdul Sharif  Mkurugenzi wa  Taasisi ya utafiti na mtandao katika nchi za eneo la bahari ya Hindi (ZIORI), iliyotaarisha mkutano, amesema wakati wa kuwakaribisha wageni kuwa kongamano hilo limewakusanya wasomi na wataalamu kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo nchi za Norway, Sweden, Denmark, Marekani, Ujerumani, Msumbiji, India, Kenya, Uganda, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar.
Kongamano hilo la siku tatu ambalo linafanyika katika ukumbi wa hoteli ya ‘ Zanzibar Ocean view’ limefunguliwa na utafunguliwa na Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ambaye katika Hotuba yake alielezea umuhimu wa wasomi kujadili mabadiliko ya kisiasa na utamaduni unaendelea dunia, kwa maslahi ya wananchi.

“Nimefarijikasanakuona jamii ya wazanzibari kutoka Afrika ya Kusini, wamekuja kujumuika nasi leo hii hapa katika mkutano huu muhimusanani nafasi nzuri ya kujenga uhusiano na mashirikiano yetu zaidi kati yetu na Afrika ya Kusini,” Maalim Seif Alisema.

Kiongozi wa ‘wazanzibari’ wageni kutoka Afrika Kusini, Ismail Fraser ameelezea furaha yake ya kufikaZanzibar, nyumbani kwao kwa asili, kwa mara ya kwanza, na kushukuru taasisi ya ZIORI kwa kuwazinduwa.

Alisema jamiiyaonchi afrika kusini inakaribia watu elfu kumi, na kwamba licha ya mabadiliko kadhaa waliyotokea nchini Afrika Kusini, wameweza kudumisha utumaduni waZanzibar.

Akitoa mada katika kongamano hilo Renu Modi kutoka Chuo Kikuu cha Mumbai ameonesha uhusiano wa tamaduni kati ya India na Zanzibar ambazo zimedumu kwa karne nyingi, huku akitaja mambo kama mavazi,vyakula na dini na wadudu kama kunguruwa Zanzibar ambao chanzo chake wametokea Bombay.

Mtaalamu huyo amesema mahusiano hayo ya kihistoria yanafaa kuendelezwa na pende mbili hizo kwa maslahi ya vizazi vya nchi mbilizi hizo ambazo kwa karne kadhaa zimekuwa na mahusiani ya kidugu katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Mkutano kama huo ulifanyikaZanzibarmwaka 2008, na lengo la kongamanohiloni kuzungumzia athari za mabadiliko ya  siasa na utamaduni katika jamii zilizoopo katika nchi za eneo la bahari ya Hindi.

Katika kongamano la mwaka huu, mada kadhaa zimepangwa kuwasilishwa na wasomi maarufu akiwemo Prof Issa Shvji, na kujadiliwa ikiwemo mahusinao ya ‘Africa naIndia,’ ‘Norwayna harakati za utafutaji na uchimbaji wa mafuta ya petrol katika ukanda watanzania,’

Mada nyengine ni ‘Njia bora za kuwa na amani na kuepuka ugomvi wa kisiasa,’ na ‘Ukuwaji wa miji na maendeleo ya watu katika nchi hizo.”

Prof Sharif ni msomi wa historia na utamaduni ambaye taasisi yake imekuwa ikishughulika na kutayarisha mihadhara ya kongamano inayozungumzia mada mbali mbali zinazohusu historia.
ZIORI ni moja ya taasisi chachesana hapaZanzibar zenye kushughulika na utafiti na imejikita zaidi utafiti wake katika zinazozunguka au zenye au zilizokuwa na mahusiano kwenye eneo la Bahati ya Hindi.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ni Professa Issa Shivji ambaye pia ni Mkuu wa Kigoad cha Mwalimu Nyerere, tasisi inayosimamia na kufautilia historia na kumbukumbu za Rais wa Kwanza waTanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s