Tunakataa kudhalilishwa

Salma Said ni Katibu wa muda wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Maedeleo Zanzibar (WAHAMAZA) na Mwandishi wa Habari wa Kampuni Mwananchi Communication inayochapisha Magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen na pia ni Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili Ujerumani (DW) aliyepo Zanzibar

WAHAMAZA inatoa wito kwa Serikali kuchukua hatua ya kutoa maelekezo
kwa vyombo vya ulinzi vikiwemo Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na kuwawacha waandishi
wa habari wafanya kazi yao kama mhimili wa nne wa dola.

 Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar
                                            (WAHAMAZA)

                          25 Mei, 2011

                          Kuh: Kukamatwa Haji Bwegege, TBC

Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) kimesikitishwa
na tukio la kukamatwa Mwandishi Haji Bwegege wa Shirika la Utangazji
Tanzania (TBC) hapo jana Mei 24 wakati akiwa kazini.

Kitendo cha kukamatwa Haji Bwegege kimetokea katika eneo la Makontena
Darajani wakati akifanya kazi yake halali na katika eneo ambalo
halilindwi kisheria.

Mwandishi huyo alikuwa akifuatilia kadhia ya Makontena ambayo kwa
hakika Mahakama Kuu ya Zanzibar tayari imeshatoa amri kuwa Makontena
hayo yaliokuwa yamefungiwa na Manispaa ya Zanzibar yafunguliwe wakati
shauri la kesi iliyo Mahakmani iliyofunguliwa na Wafanyabiashara hao
likisubiri kusikilizwa.

Mwandishi alikuwa akifanya wajibu wake kuona kuwa amri ya Mahakama
inatekelzwa katika hali ambayo ni wajibu wa taasisi za Serikali kuwa
mfano wa Utawala Bora, ambapo amri ya Mahakama iliyotolewa Alkhamis
iliyopita hadi jana ilikuwa bado haijatekelezwa.

Wana vikosi wanaofanya lindo katika eneo hili hii ni mara ya pili
kunyanyasa waandishi wa habari wanapofika katika eneo hilo , mara ya
kwanza ikiwa ni dhidi ya Mwandishi Munir Zakaria wa Channel Ten.

Jambo hili halikubalika hata kidogo tukijua kuwa Rais wa Zanzibar Dk
Ali Muhammed Shein katika hotuba yake ya kuingia Serikali alisema kuwa
utawala wake utakuwa karibu na vyombo vya habari na utaheshimu uhuru
wa vyombo vya habari.

Haya yakitokea waandishi wa habari wa Zanzibar kwa ujumla hawaridhiki
na namna wanavyowekwa kando na mfumo mzima wa Serikali ya Zanzibar na
kwa ujumla ikiwawia vigumu kupata habari, kama alivyotanabahisha Dk
Shein alipozungumza na watendaji wa Serikali baada ya semina elekezi
lakini pia kurudia baada ya ziara yake ya Mkoa Mjini Magharibi.

WAHAMAZA inatoa wito kwa Serikali kuchukua hatua ya kutoa maelekezo
kwa vyombo vya ulinzi vikiwemo Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na kuwawacha waandishi
wa habari wafanya kazi yao kama mhimili wa nne wa dola.

Pia WAHAMAZA inapenda kutoa wito wa Serikali kujivua gamba katika
suala zima la kutoa habari na kufungua milango kwa wananchi, ambao
hivi sasa miezi sita tokea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa,
hawajui mengi kuhusu Serikali yao na kwa hivyo si waelewa wa
kilichofanyika na kisichoweza kufanyika hadi sasa, lakini zaidi kwa
sababu gani na huku hali yao ya maisha ikiwa ngumu zaidi.

WAHAMAZA inapenda kutoa ahadi kuwa iko tayari kufanya kazi na Serikali
kwa karibu zaidi kwa kuelewa kuwa vyombo vya habari ni kiungo muhimu
baina ya Serikali na wananchi na tunajua kuwa Serikali iliyochaguliwa
na watu haitaki kujitenga na wapiga kura na wananchi.

Katibu wa muda wa Chama Cha Wananchi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA)

Salma Said 

Advertisements

One response to “Tunakataa kudhalilishwa

  1. Aslam aleikum,
    Pongezi mama maana hawa viongozi wakisha kulakiapo cha ukafiri maana wana ona wanamuhadaa M/mungu nakumbe wanajihadaa wenyewe huona wale waliwowachagua hawana maana tena na niwatumwa wa.
    Heko kwa taarifa yako M/mungu yuko pamoja na wateteao haki.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s