Uhuru wa waandishi kitanzini

Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Haji Bwigege

MWANDISHI wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Haji Bwigege leo amekamatwa na polisi wa Baraza la Manispaa laZanzibarwakati anapiga picha katika maduka ya eneo la Darajani.

Mwandishi huyo na mtangazaji alikuwa akipiga picha katika makontena yaliyofungwa na serikali katika eneo la Darajani ambapo kwa muda mrefu serikali imekuwa inakataa kuchukuliw ahabari na kupgwa picha katika eneohilolinaloendelea kulindwa na polisi nyakati zote.

Baada ya kukamatwa na askari wa vikosi vya SMZ wanaolinda eneohilo, mwandishi huyo Haji Bwigere, alipelekwa makao makuu ya Baraza la ManispaaZanzibarambapo alishikiliwa kwa masaa kadhaa.

Aidha mwandishi huyo alinyang’anywa vifaa vyake vya kazi ikiwemo kamera ya video ambayo aliyokuwa akiitumia katika kuchukua picha ya eneohilola Darajani kwenye makontena na askari waliokuwa wanamzuia kupiga picha.

Mwandishi huyo baada ya muda alirejeshewa kamera yake na kuikaguakamaimepata athari au laa lakini baadae aliona kamera yake haina athari yoyote lakini picha zake zote za tukio alizopiga zilifutwa na baadae kuondoka.

“Nasikitikasanamaana picha nilizopiga zimefutwa,” alisikika Bwigire akilalamika mbele ya maofisa wa Baraza la Manispaa.

Maafisa wa baraza la manispaa walikuwa wakitafuta ufumbuzi katiyaona mwandishi huyo ambapo kikao hicho kiliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wake, Mzee Abdallah.

Kaimu Mkurugenzi alielezea kukamatwa kwa Bwigire, alisema eneohiloliko chini ya ulinzi na kwamba mpiga picha huyo alitakiwa kuomba ruhusa ya manispaa kabla ya kwenda kutekeleza majukumu yake katika eneohilo.

Mwandishi huyo alisema alikwenda kufuatilia habari kuhusu kukwama kwa amri ya Mahakama Kuu inayotaka maduka hayo yafunguliwe hadi hapo kesi ya awali iliyofunguliwa juu ya mgogoro huo itakapotolewa uamuzi.

Hukumu hiyo ilitolewa Mei 19, mwaka huu na Jaji Rabia Hussein Mohamed kufuatia kesi iliyofunguliwa dhidi ya baraza la Manispaa na Haroub Changawe, Abdallah Said Mohamed na Abbas Juma kwa nianba ya wafanyabiashara 52 wanaomiliki maduka hayo.

Katika maamuzi ya hukumu ya Jaji Rabia pia ilipelekwa kwa Mkurugemnzi wa Baraza la manispaa hiyo, yakiwa na kumbukumbu Namba MMK/166/2011 ya Mei 19 mwaka huu.

Serikali imeamua kuwaondoa wafanyabiashara katika eneohiloili kuruhusu ujenzi bustani na maenegesho ya magari, lakini wafanyabiashara walifungua kesi kupinga hatua hiyo wakitaka makontena yanayomilikiwa na CCM pia yahusishwe katika mpango wa kuondolewa katika eneo hilo.

Eneo hilo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilalamikia hali hiyo kwa miezi kadhaa ambao hadi sasa wamekuwa hawana sehemu maalumu ya kufanyia biashara zao.

Advertisements

One response to “Uhuru wa waandishi kitanzini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s