Tupande miti mingi zaidi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja eneo la Mtowapwani, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali katika mkoa huo

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. Mohammmed Gharib Bilal, amewataka wananchi kuona wanaivushaZanzibarkwenye maendeleo  teknologia ili kuiepusha kufanywa kuwa ni makumbosho ya kihistoria ya dunia.

 

Dk. Bilal, aliyasema hayo juzi wakati akiwahutubia wananchi na wanafunzi wa Skuli ya Nungwi Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa madarasa katika skuli hiyo yaliyojengwa na mmiliki wa hoteli ‘Z hotel’.

 

Dk Bilal alisema hatua ya serikali ya marekani kuweka nia ya kutoa kopyuta kwa wanafunzi wote waZanzibarserikali ya Muungano na Serikali yaZanzibar, inaipokea kwa furaha kubwa kwani itaiwezesha Zanzibarkuvuka katika maendeleo ya teknologia na kuifanya kuachwa kuwa makumbusho ya dunia.

 

Alisemahiloni moja ya jambo la msingi ambalo Wazanzibari hasa wanafunzi katika skuli zaZanzibarwanapaswa kuona wanaaza kujiandaa kuyakubali mabadiliko hayo kwa kuwa wenye upeo wa kufahamu vyema mfumo wa teknologia.

 

Alisema tayari Ubalozi wa Marekani imemuhakikishia kutaka kuleta mradi huo kwa wanafunzi waZanzibarjambo ambalo serikali ya Muungano na Serikali yaZanzibaritahakikisha inashirikiana na Ubalozi huo ili kufanikisha adhmayaohiyo.

 

Alisemahilowatalisimamia ikiwa na lengo la kuiondoshaZanzibarkufanyawa kuwa makumbusho ya kihistoria kwa kushindwa kuwafanya wanafunzi waZanzibar, kutotumia mitandao jambo ambalo tayari baadhi ya mataifa hivi sasa yanatoa mafunzo mskulini kwa kutumia mitandao.

 

“Hatutaki kuwa makumbusho ya kale twendeni kwenye ushindani wa kilimwengu huku tukidhibiti silka zetu kwani maisha ni mapambano lazim mubebe jukumuhiloivusheniZanzibarifike mbali kazi ni kujiandaa na madudu haya yanakuja” alisema Dk Bilal.

 

Akiendelea Dk Bilal, aliwaomba wazazi kuona wanashirikiana na walimu ili kufanikisha masomoyaona kuacha tabia ya kuwatumikisha kwa muda mrefu huku akiwataka walimu kuona wanafanya jitihada za kutoa elimu badala ya kuweka maslahi binafsi ya kufundisha zaidi katika madarasa ya tuisheni.

 

Aidha Dk. Bilal, aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo kuona wanaendeleza tabia ya kuchangia maendeleo ya Jimbo lao huku akimpongeza Mkurugenzi wa Z hoteli kwa kuwajali wananchi wa Jimbohilokwa kuamua kujitolea kuwajengea skuli wananchi wa kijiji hicho.

 

Alisema hatua ya Muwekezaji huyo ni ya kizalendo kutokana na kutumia faida yake kujenga skuli kwa ajili ya wananchi wa eneohilojambo ambalo linahitaji kuigwa na wawekezaji wengine.

 

Dk Bilal, alichangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika skuli hiyo ambapo hapo mapema akizungumza na wananchi na wanafunzi wa skuli ya Kiwengwa aliwataka kuona wanaisimamia vyema miundo mbinu ya Elimu inayowekezwa kwa kuipa ulinzi katika skuli mbali mbali za Unguja naPemba.

 

Alisema serikali imeamua kwa makusudi kuwekeza miundo mbinu ya elimu ikiwa ni hatua ya kuwasogezea wananchi huduma bora na haipaswi kuona wachache wanashindwa kuitunza kwa sababu zao binafsi.

 

Dk. Bilali, katika skuli hiyo alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa nyumba ya walimu.

 

Aidha, Dk Bilal, aliwataka wananchi waliotiliwa moto makaaziyaokatika kijiji cha Pwani Mchangani kuwa wastahamilivu na serikalii itahakikisha misingi ya sheria inafuatwa.

 

Kwenye ziara hiyo pia Dk. Bilal, aliweka mawe ya msingi katika tawi la CCM la Shindoni, na Kipange na kufungua wa maskani ya Simba mtoto Kinyasini ambapo aliahidi kuwapatia Televisheni.

 

Katika matawi hayo Dk. Bilal, aliwataka wanachama hao kuona wanayatumia matawi hao kujiimarisha zaidi kuelekea katika uchumi huku wakidumisha amani ya nchi na kuacha kununiana kulikosababishwa na kura za maoni zilizopita.

 

Alisema lengo la CCm hivi sasa ni kuona wanajiimarisha vizuri zaidi kwa kuwa na wanachama wataoweza kutoa viongozi bora ambao watakivusha Chama katika uchaguzi Mkuu wa 2015.

 

Sehemu kubwa ya wananchi katika zira hiyo wakitoa risala zao walieleza kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya kumaliza majengoyaoambayo ni ya chama nay ale ya Serikali.

 

Mapema Dk. Bilal, alishiriki katika uzinduzi wa siku ya mazingira duniani katika Mkoa wa Kaskazini kwa kupanda mti katika jengo la afisi ya Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Unguja.

 

 

Advertisements

One response to “Tupande miti mingi zaidi

  1. Hawa viongozi wetu kwakweli wamezidi sana yaani mzanzibar gani na mkulima gani anapanda mti akiwa juu ya mkeka ? kwani kwa Dr Bilali akikanyaga mchanga itakuwaje ? na staili hii ndio anawaambia nini wananchi kua mchanga ni uchafu au?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s