Wananchi Wasizimiwe Simu

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mama Asha Seif Ali Iddi akiwa anakwenda kutunza waimbaji katika mkutano ya hadhara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa Zanzibar

WANANCHI WASIZIMIWE SIMU

MKE wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Balozi, amewataka viongozi wa Majimbo kuacha tabia ya kuwakimbia wananchi kwa kuwafungia milango na kuwazimia simu pale wanapowafuata kutaka kuelezea mambo yanayowakera katika majimbo yao.

Mama Asha aliyasema hayo juzi wakati akizindua rasmi Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Fuoni (JUMAJIFU), huko katika Skuli ya Fuoni Wilaya ya Magharibi Unguja ambapo pamoja na mabo mengine amewataka viongozi wa majimbo kuwavumilia wananchi wao na sio kuwakatia simu au kuwazimia kwa kukimbia kero zao.

Alisema baadhi ya Viongozi wa majimbo wameanzisha mtindo wa kuwakimbia wananchi kwa kuwafungia milango na kuwazimia simu jambo ambalo linahitaji kuchwa tabia hiyo kwa wanatoifanya kwa vile inachangia kwa kiasi kikubwa kuleta mifarakano kati ya viongozi na wananchi.

Alisema kinachohitajika kama wananchi wanapowafuata ni vyema kuwasikiliza kwanza na kama wakiona hoja wanazowaletea hazina maslahi na maendeleo ya Jimbo bali ni mambo binafsi ndipo wawwawaeleze ukweli namna ya kutatua shida zao.

Alisema wanachotakiwa kukitambua kazi ya Uwakilishi na Ubunge, si ajira bali ni utumwa kwa kuwatumikia wananchi na sio vyema kuendelea ama kuaitumia njia hiyo kwa kukaa mbali nao.

“Mimi mwenyewe ningekuwa napokea mkoba wa samaki nikala ingekuwa hakuna maendeleo kitope uongozi wa bwana ni wa bibi sio kuwabania milango au kuwazimia simu” alisema Mama Asha.

Akiendelea alisema kinachohitajika kwa viongozi wa Jumuiya hiyo kuona wanajenga ushirikiano na wananchi wao kwa kuwapelekea mahitaji ya maendeleo badala kushughulikia mambo binafsi.

Mama Asha aliitaka Jumuiya hiyo kuona inafanya kazi kubwa ya kutengeneza miradi ambayo wataweza kuipeleka kwa wafadhili na kuiza ili waweze kupata mafanikio.

Alisema hivi sasa kuna mashirika ya kimataifa ambayo yamekuwa yakisaidia shughuli za maendeleo na itakuwa vyema Jumuiya hiyo ikaona umuhimu wa kuyatumia ikiwa ni hatua itayoweza kukuza Jumuiya yao na kuondoa shida za wananchi.

Hata hivyo Mama Asha aliwaonya viongozi wa Jumuiya hiyo kuona wanafanya kazi kwa pamoja na kuacha tabia ya kupikiana majungu kwani inaweza ikaharibu uwezo wa Jumuiya hiyo.

“Wekeni maslahimanufaa mbele sio chama katika suala la kamati za maendeleo mtambue kuwa mtapata mikiki mingi ili nia kumuangusha kiongozi wenu muwe wastahamilivu mjenge mshikamano msipokee majungu kwani juweni zitakuja fitina nyingi na za kila aina” Alisema Mama Asha.

Alisema inawezekana kabisa bada ya kupata mafanikio yakazuka maneno ya kumgeukia Mbunge aliyeanzisha Jumuiya hiyo kudaiwa kuwa anafanya hayo kama ni sehemu ya kampeni zake za kutaka achaguliwe tena kushika nafasi hiyo.

Alisema hiyo sio sahihi kwani lengo la Chama cha mapinduzi kuona serikali yake inakuwa na maendeleo kwa wananchi wake na hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Jimbo hilo inatekeleza dhamira hiyo ya kuleta maendeleo.

Hata hivyo aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kuona wanapokutana na viongozi wao kuwapelekea mahitaji ya Jimbo lao katika mambo ya maendeleo na sio mambo binafsi kwa kuomba vyakula ama pesa za kangha kwani ni mambo yatayoweza kuwachosha viongozi wao.

Mama Asha katika sherehe hiyo aliendesha harambee kwa ajili ya kuisaidia Jumuiya hiyo ambapo yeye binafsi alitoa dola za kimarekani 300 na Viongozi na wananchi wa Jimbo hilo walichangia zaidi ya shilingi milioni 2/=

Mapema Mbunge wa Jimbo hilo, Iddi Mohammed Zubeir, aliwashukuru wananchi kwa kukubali kuitikia wito wa kuanzisha Jumuiya hiyo na kuahidi kuendelea kutoa misaada mbali mbali.

Kutokana na dhamira hiyo Mbunge huo ameamua kutoa pikipiki aina ya bajaji yenye thamani ya shilingi milioni 11 kwa ajili ya kubebea wagonjwa ambayo itatumika katika Jimbo hilo ikiwa pamoja na kuihumia katika matengenezo.

Mapema mmoja wa viongozi wa Jumuiya hiyo Salama bakari Wakati, alisema dhamira ya kuunda Jumuiya hiyo ina lengo la kuona inaongeza maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo afya, barabara, Elimu na kuwawezesha wananchi kuinua hali zao za maisha pamoja na uchumi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s