CUF wafungua tawi Donge

Chama Cha Wananchi kimefanikiwa kufungua tawi lake katika JImbo la Donge ambapo ni kwa mara ya kwanza kufunguliwa tawi katika Jimbo hilo linaloshikiliwa na Mwakilishi wake ambaye ni miongoni mwa wahafidhina wakubwa wa siasa za Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Donge kwa takribani miaka zaidi ya kumi sasa, Ali Juma Shamhuna

 

HATIMAE Chama Cha wananchi (CUF) jana kimefungua rasmi tawi la chama hicho katika Jimbo la Donge Mchangani Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo kwa mara ya kwanza tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi chama hicho kuweza kujipendeza katika jimbohilo.

Juhudi za kuingia katika jimbo hilo zimefanyika mara kadhaa bila ya mafanikio kwa madai kwamba jimbo hilo limetawaliwa na wahafidhina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wasiotaka mabadiliko wala kusikiliza sera za vyama vyengine licha ya kuwepo uhuru wa vyama vyengine vya siasa ambapo CUF ina wanachama 105 katika jimbo hilo..

Sababu zilizoelezwa kwa sasa kuweza kufunguliwa tawi hilo jipya huko Donge ni kutoka kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa ambapo yameridhiwa mwaka juzi na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Mstaafu Amani Abeid Karume kwa lelngo la kusameheana, kusahau yaliopita na kujenga Zanzibar mpya ambapo viongozi hao walikubaliana kuendesha siasa za kistaarabu bila ya kugombana.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiano ya Umma, Salim Bimani alisema hatua hiyo ni ya kihistoria na ina kila sababu ya wazanzibari kujivunia kwa kuwa ni moja ya matunda ya maridhiano yaliofikiwa na viongozi wao wakuu wan chi.

Bimani aliwataka wanachama wa chama hicho kutumia tawihilokwa vizuri na kuongeza wanachama ili wazidi kuwa wengi kwa lengo la kufanikisha malengo ya chama hicho kupaa wanachama wengi lakini pia hatimae kuchukua kiti cha jimbohilokatika uchaguzi ujao wa 2015.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba chama cha CUF baada ya miaka kumi na tano kimefanikiwa kuandika historia mpya ya kufungua tawi katika jimbo hilo, jimbo ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa na nguvu za viongozi wasiotaka mabadiliko kuingia katika jimbo hilo lakini wananchi wa jimbo hilo hawakuchoka kutaka hatakati za mabadiliko yab kisiasa yaendelee na kutaka demokrasia ya kweli ya kuchagua chama wakitakacho.

Alisema wananchi wa Donge wanahaki ya kupewa pongezi kwa hatua kubwa na ukomavu wao wa kisiasa kwa kupigania suala la kutaka wafunguliwe tawi katika jimbo lao licha ya changamoto kadhaa zilizopo jimboni hapo lakini hatimae wamefanikiwa ombi lao kukubaliwa na kufunguliwa tawi katika jimbo hilo.

Mkurugenzi huyo aliwaambia waanchi wa Donge kwamba mafanikio hayo hayakuja bure isipokuwa ni matunda ya maridhiano yaliyofikiwa na vyama vya siasa vya CCM na CUF na baadae kuzaliwa serikali ya umoja wa kitaifa ambapo aliwataka wanachama hao kufanya kazi kubwa ya kukiunga mkono chama chao pamoja na kuenzi juhudi za kufikia maridhiano.

“Sisi leo tunafuraha kubwasanatumeandika historia katika chama chetu, tena historia mpya chini ya maridhiano CUF imekabidhiwa Donge na si muda mrefu tutakabidhiwa mamlaka yote ya kuliongoza jimbo hili …jambo la msingi kuendeleza siasa za kistaarabu na kutokubali kurejeshwa katika siasa za chuki na uhasama tunajengaZanzibarmpya yenye maelewano” alisema Bimani.

Naye kwa upande wake akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini, Ashura Sharif alisema kufunguliwa kwa tawihilokatika kijiji cha Donge ni hatua nzuri ya kufikia demokrasia ya kweli.

Alisema wananchi wa Donge amefanikiwa kufikia ndoto yao ya muda mrefu ya kutaka kufunguliwa tawi katika jimbo hilo ambapo mara kadhaa juhudi zake zimegonga mwamba kutokana na pingamizi za hapa na pale kwa kutumiwa kisingizio cha wazee wa jimbo hilo kukataa vyama vyengine vya siasa kuingia katika jimbo lao.

Alisema wananchi wa Donge kwa miaka zaidi ya 15 sasa wamekuwa wakikosa haki ya kidemokrasia ya kushiriki katika mikutano ya hadhara ya vyama vyengine vya kisiasa kutokana na kukatazwa kufanyika mikutano ya hadhara katiak jimbo hilo zaidi ya Chama Cha Mapinduzi lakini sasa wanancho watapata kuona na vyama vyengine vikiingia katika jimbo hilo hatua ambayo itaharakisha demorkasia ya wananchi hao kutoa na kupata maoni tofauti.

Mwakilshi huyo wa wanawake alisema atatumia fursa yake katika baraza la wawakilishi kuwatumikia na kuwatetea wananchi wa Jimbo la Donge kwa kuwa yeye anawawakilisha wananchi wa wote wa Mkoa wa Kaskazini.

Tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi Jimbo la Donge limekuwa likishikiliwa na Chama Cha Mapinduzi ambapo kwa sasa Mbunge wa Jimbo hilo ni Sadifa Juma Khamis na Mwakilishi wake ni Ali Juma Shamhuna ambaye analishikilia jimbo hilo kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Vyama vya siasa vimeshindwa kufungua tawi wala kufanya mkutano wa hadhara katika jimbo la Donge tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi kwa madai kwamba wazee wa jimbohilohawataki kusikiliza sera za vyama vyengine.

Chama Cha Mapinduzi CCM ndio pekee kilichokuwa kikifanya mikutano yake ya hadhara ikiwemo ile ya kampeni pamoja na Chama Cha Safina kilichokuwa kikidaiwa kuwa ni CCM B kilichokuwa kikiongozwa na Marehemu Omar Awesu Dadi ambaye alikuwa ni mwana CCM na Mkereketwa mkubwa wa CCM kabla ya kujiengua CCM na kuunda chama hicho cha Safina kilichokuwa na nguvu kubwa ndani ya mkoa wa kaskazini.

Chama Cha Safina ambacho kiliibuka ghafla mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais Mstaafu Amani Abeid Karume baada ya uchaguzi mkuu wa wa mwaka 200 baada ya CCM kumeguka na kutofautiana kati ya kundi lililokuwa na nguvu kubwa wakimuunga mkono Dk Salmin Amour Juma na kundi la Amani Abeid Karume kukhitilafiana ambapo wajumbe walitaka Dk Mohammed Gharib Bilal achukue nafasi ya urais wa Zanzibar huku wajumbe wengine wakimtaka Amani Abeid Karume.

Chama Cha Safina kilichokuwa ni tishio kwa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kilikuwa na nguvu kubwa huko Mkoa Kaskazini Unguja na kikiungwa mkono na wazee wa mkoa huo ambapo baadhi ya viongozi wa sasa wa kisiasa walihusishwa na uundwaji wa chama hicho lakini hakijaishi muda mrefu kutokana na kupigwa vita na baadhi ya waanzilishi wake kununuliwa na hatimae vifa ghafla na kuundwa chama chengine cha Jahazi Asilia ambacho kimepata usajili na kuendela na shughuli zake kama kawaida lakini kimekosa nguvu zile za Safina.

Advertisements

4 responses to “CUF wafungua tawi Donge

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s