Ziara ya Dk Bilal Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwera Misufini baada ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya CCM ya Tawi la Misufini Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar

BILAL AKERWA NA CHOKOCHOKO ZA MUUNGANO

MAKAMO wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal anakerwa na watu wanaoleta chokochoko za Muungano na kufanya vitendo vinavyohatarisha amani na utulivu nchini.

Akiivitaja vitendo vya kuchoma moto vibanda vya biashara vya wananchi huko Mkoa wa Kaskazini na kuchana mswada wa marerekisho ya katiba ni ishara ya kuwepo kwa watu wanaoleta chokochoko za Muungano ambao umedumu kwa miaka kadhaa bila ya matatizo yoyote.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Mwera Misufini ikiwa ni moja ya ziara yake ya miradi ya maendeleo na kutoa shukurani kwa wananchi kufanikisha uchaguzi mkuu uliokwenda salama na kukipa ushindi chama chake kwa Unguja na Pemba Makamo amesema mswaada wa katiba hauna lengo la kuhatarisha Muungano au kuvuujunga bali umekuja kwa ajili ya kuuimarisha.

Alisema wenye kuleta chokochoko hawataachiwa na kamwe serikali hazitavumilia kuona baadhi ya watu wanatumia mwanya huo kwa ajili ya kuwadhoofisha wenzao kwa kisingizio cha kuukataa Muungano.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tayari umetimia umri wa miaka 47 sasa ni ishara ya upendo na mshikamano wa wananchi wa pande mbili hizo ambao wamekuwa wakiishi kama ndugu tangu zamani hivyo serikali inataka kuona umoja huo ukiendelea na sio kuvunjika.

Alisema yeye kama makamo wa rais pamoja na mwenzake waziri anayeshungulikia mambo ya muungano Samia Suluhu watahakikisha kwamba matatizo na kero za muungano zinapatiwa ufumbuzi kwa kutumia vikao halali vya pande mbili ili zile kero zilizokuwa hazijapatiwa ufumbuzi zinapatiwa.

“Mimi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ofisi yangu ndio yenye jukumu la mambo yote ya Muungano na mwenzangu Samia Suluhu huyu hapa tupo kwa ajili ya kuangalia maslahi ya Muungano kwa upande wa Zanzibar basi sisi tutahakikisha kero zote zinapatiwa ufumbuzi” aliongeza kiongozi huyo.

Aidha aliwataka wananchi kuachana na ndoto za kufikiria kuuvunja Muungano kwa wakati huu ambapo dunia ndio kwanza inazidi kufanya harakati za kuungana pamoja na kuunganisha nguvu hivyo sio jambo la busara kwaZanzibarkufikiria suala la kuuvunja muungano wa pande mbili hizo.

“Ulimwengu wa sasa unahitaji umoja kwa sababu umoja ni nguvu hebu angalieni kule ulaya wao wameungana na ipo jumuiya ya ulaya lakini pia kuna bara la Asia kule wameungana hadi bara la Arabuni kwa lengo la kukuza uchumi na kudumisha umoja inakuwaje watanzania tuwe na mawazo ya kukataa kuungana na kuimarisha nguvu zetu pamoja” alisema Dk Bilal.

Dk Bilal alisema ni kweli hivi sasa ndani ya Muungano kumekuwa kukijitokeza kero mbali mbali lakini bado haijawa ni kigezo cha kuutenga ama kuukataa kwani unaweza kuwaumiza wengi.

Alisema hivi sasa sehemu kubwa ya watanzania hasa wazanzibari  wameonekana kuwapo sehemu mbali mbali zaTanzaniana haitakuwa busara kuanza kufikiria kuvunja Muungano.

“Hatutafanya kuandika katiba mpya kwa kuutenga Muunganohilohapana ‘No’ watu wanachoma miswada kuchokonoa Muunganokamahaufai waacheni CCM wao ndio waliowafikisha hapo” alisema Dk. Bilal.

Kinachotakiwa kuona kuwa wananchi wanafaidika na Muungano uliopo na kuuendeleza ili vizazi vijavyo viweze kupata matunda yake kwani dhamira ya viongozi walioanzisha Muungano ilikuwa inatizama zaidi kuunganisha nguvu za pamoja.

Dk. Bilal alisema, serikali ya Muungano na Serikali yaZanzibaritahakikisha kuwa inaandaa mipango mbali mbali ya kuzitatua kero ziliopo kwa haraka ili kuweza kuona wanaenda vizuri.

Alisemahiloserikali hizo italifanyia kazi kutokana na hivi sasa baadhi ya mataifa wameamua kuitumiaZanzibarkujifunza namna ya kuendesha muungano wan chi mbili.Kutokana nahiloDk Bilal, alisema Muungano ambao serikali itahahakikisha inaufanyia kazi ni ule utaoleta nuru kwa wazanzibari wote.

Mapema Wanachama wa Chama hicho katika risalayaowalieleza dhamirayaoya kuona wanashirikiana na serikaliyaokwa kuhakikisha wanadumisha Muungano pamoja na kufanya mabadiliko katika chama kwa kutoa wanachama bora wataokiwezesha Chama kupata ushindi 2015.

Dk. Katika zira hiyo alifuatana na viongozi mbali mbali mbali wa Wilaya hiyo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.Mapema Dk Bilali alitembelea bonde la mbunga la Bumbwisudi  na kuitaka serikali kuongeza nguvu katika sekta ya kilimo.

Advertisements

3 responses to “Ziara ya Dk Bilal Zanzibar

 1. Kuumwa wakati mwengine kuko. Inasikitisha kuona kuwa sasa viongozi wanne wa Zanzibar (au kutokea Zanzibar) wanatoa kauli zinazofanana: Shamsi Vuai Nahodha (Waziri wa Mambo ya Ndani kwenye Serikali ya Muungano), Balozi Seif Ali Idd (Makamo wa Pili wa Rais kwenye Serikali ya Zanzibar), Samia Suluhu Hassan (Waziri Mwenye Dhamana ya Muungano kwenye Serikali ya Muungano na sasa huyu Dk. Mohammed Gharib Bilal (Makamo wa Rais wa Muungano).

  Hoja zao ni nyepesi na kwa kutumia msamiati wa Samuel Sitta alipokuwa spika wa bunge la Muungano, “ni siasa za maji-taka”. Unapotoa mifano ya kuchanwa kwa mswaada na kuunganisha na kuchomwa moto kwa mabanda ya Pwani Mchangani na madai ya Wazanzibari kuukataa Muungano, maana yake ni nini kama si siasa za maji-taka? Siasa za kujipendekeza?

  Ushahidi umeshaonesha kwamba, kwanza, Wazanzibari waliukataa mswaada kwa kuwa serikali yao haikushirikishwa hata kidogo. Mkutano wa kwanza uliofanyika hoteli ya Bwawani ulithibitisha hivyo kutoka vinywa vya viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya Zanzibar. Sasa akina Dk. Bilal wanaposema hawatamvumilia anayetaka kuvunja Muungano, wanamtisha nani? Wanaitisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar?

  Pili, ushahidi umeonesha kuwa kati ya mabanda 29 yaliyochomwa moto, 27 ni ya Wazanzibari na mawili tu ndiyo ya Wabara. Sasa hizo chuki dhidi ya Wabara kwa nini zielekezwe kwa mabanda ya Wazanzibari? Hawaoni kuwa jawabu ni kwamba hapa lililoangaliwa halikuwa asili ya mwenye kumiliki banda, bali vitendo ambavyo ndani ya banda hilo vinafanyika na ambavyo havikubaliki katika jamii ya Kizanzibari? Leo hii viongozi hawa, kwa sababu ya nafasi walizonazo, wanadhani kwamba wanaweza kuwachuuza Wazanzibari wenzao kwa kauli zao nyepesi na siasa na maji-taka?

  Tatu, wanapoendelea kujenga hoja ya kuimarika Muungano (na hivyo uhalali wake) kwa kuwepo Wazanzibari wengi Bara wanakofanya biashara zao (na siku hizi angalau wameipamba kidogo, hawasemi tena Wapemba wengi kama alivyokuwa akisema Benjamin Mkapa na baadaye akaja akarudia Rais Jakaya Kikwete), wanakusudia nini?

  Kwamba kwa sababu kuna sehemu hiyo ya Wazanzibari ambao wanatafuta maisha kwa njia za halali ndani ya ardhi ya Tanzania Bara, ni halali kwa hivyo Wazanzibari wapoteze hadhi ya nchi na utamaduni wao kwa kukubali kila kitu, ati tu wanalinda Muungano?

  Kiwango cha chini kabisa cha kufikiri ndicho kitakachomfanya autoe sadaka uzalendo, utaifa na utukufu wa nchi yake kwa vipande vya fedha na kikombe cha chai.

 2. Huyu Bilali smeishiwa na amelewa na fupa alilopewa kungongona huko Bara!! Wazanzibari wamenyima fupa hilo, sasa Wabara kwake yuko tayari hata kuramba nyayo zao!! maneno gani haya ya kusema, ati huyu kiongozi ambae tunamtegemea kuwa yuko huko bara na kuwa labda atatupigania haki zetu? Huyu ni gari yake ya mwisho hii, anakuwa na gari gani tena ya kudandia?

 3. huyo bilali ni muiflis musishangae na ngojera zake katumwa huyo na bosi wake lakini ankula huuuu no zanzibari will buy his porojooooooooooooooooo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s