Najaribu kama mashine nzima

Katibu Mkuuwa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiijaribu moja ya gari zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni moja ya ahadi zao kwa wananchi wa jimbo hilo wakati wa kampeni za uchaguzi, ambapo waliahidi kuwapatia huduma wananchi wote wa jimbo hilo bila ya kujali mwananchi huyo anayoka chama gani cha siasa.

 

Wananchi wa Gando wapatiwa gari

WANANCHI wa Jimbo la Konde wamepatiwa msaada wa gari matatu na kanga kadhaa vyote hivyo vyenye thamani ya thamani ya shilingi millioni 71,000,000 ambazo zimetumika kununuliya magari pamoja kanga kwa ajili ya wanachi wa jimbohiloliliopo Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Shilingi millioni 46,500,000) zimetumika kwa ajili ya kununuliya magari ambayo kwa kila moja ni millioni 15,500,000 milioni ishirini 20 zimetumika kwa kununuliya doti 5,000 za kanga na millioni nne na 4,500,000 zimetumika  kwa ajili ya bima za magari hayo, ambapo bima zenyewe ni gred la juu (first gred).

Mbunge wa Jimbo la Konde, Khatib Said Haji alisema msaada huo utawanufaisha wananchi wote katiak jimbohilobila ya kujali mwananchi huyo anatoka chama gani ambapo kila mkaazi wa jimbohilona shehia zake atanunua kanga kwa shilingi 2,500 badala bei ya shilingi 4,000 bei ya kawaida huduma ambayo itaendelea kwa kipindi chote atachokuwepo madrakani.

Mbunge huyo alisema hayo katika viwanja vya ilima Vitatu huko Konde wakati akiwakabidhi wananchi magari hayo katika sherehe zilizofanyika na kushuhudiwa na Katibu Mkuuwa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad.

Haji alisema magari hayo yatatoa huduma bila ya kujali mtu anatoka chama gani na atahakikisha kipindi chote akiwa mbunge atawahudumia wananchi bila ya ubaguzi na atashirikiana na na wananchi hao na mwakilishi wa jimbo hilo ili kuto huduma katika jimbo lao hukua kiahidi magari hayo kuyashughulikia kwa garama zake ikiwemo mafuta, matengenezo na kuwalipa mishahara mdereva na ambo mengine yote watayasimamia bila ya kuchoka.

Mbunge huyo amewataka wananchi wa jimbo lake kuwa na subra juu ya hali ngumu ya maisha wakati huu ambapo dunia imekumbwa na tatizo la mfumko wa bei na ukosefu wa vyakula ambapo alisema hilo ni suala la kupita na kuwataka wavumilie utulivu uliopo na maelewano kwani yatazaa matunda ya kheri na yenye baraka kwa siku za baadae.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi wa  jimbo la konde kuzitunza na kuzithamini juhudi zilizooneshwa na mbunge na mwakilishi wa jimbohilokwani kutofanya hivyo kutawavunja moyo viongozi wao.

Aidha aliwataka wananchi hao kuzitumia vizuri gari ambazo wamepata kwani hiyo ni mali yao na sio tena ya mbunge na mwakilishi hivyo wana kila sababu ya kuzienzi na kuzitumia vizuri ili zidumu na ziweze kuwanufaisha katika harakati za maisha yao ya kila siku huku akitoa wito wa wabunge na wawakilishi kuiga mfano huo uliooneshwa katika jimbo la Konde.

Maalim Seif alisema ni vizuri kila mbunge na mwakilishi aliyetoa ahadi kama hizo atimize ili kujenga imani ndani ya chama chake na pia kwa wananchi wake kwani wapo ambao wameahidi lakini bado hawajatimiza ahadi zao jambo ambalo litawarejesha nyuma wananchi na kuwapunguzia imani juu ya viongozi wao amba wamewateuwa katika majimboyao.

Maalim Seif pia amewataka wananchi hao kuwangalia madereva gari hizo,kamawatazitumia kinyume vilivyo kusudiwa basi wawambie waheshimiwa wao ili wafanyie kazi kwani magari haya  si kwa ajili ya kubebea mkaa bali ni kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi.

“Wenyeviti wa wilaya  na makatibu wa  kuu wa chama cha CUF wa wilaya zote muwahimize  wabunge wenu na wawakilishi wenu watekeleze ahadi zao zote ambazo wameahidi kwa wananchi wakati wa kampeni ili kila mmoja aliyeahidi atimie ahadi yake hivyo ndivyo inavyotakiwa kutimiza ahadi ili wananchi wawe na imani nanyi” alisema Maalim Seif .

Akizungumzia suala la serikali ya umoja wa kitaifa Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar alisema anafahamu hali ngumu za maisha na bei za bidhaa kuwa juu hasa mchele,sukari na unga wa ngano  ambayo ndiyo vyakula vikibwa kwa wananchi wa Zanzibar lakini tatizo hilo sila Zanzibar peke yake bali dunia nzima imekubwa na tatizo hilo.

Alisema tatizohiloni kutokana na maafa mengi yalioikumba dunia ikiwemo matetemeko ya aridhi na mashamba mengi kufunikwa na barafu katika nchi ambazo zinatoa mchele kwa wingi duniani na kupelekea bei kuwa juu na bidhaa mbali mbali.

Amesema serikali imo katika juhudi kubwa ya kuliondoa tatizo hilo kwa kuwasaidia wakulima ili walime kilimo cha umwagiliaji pamoja na kutafuta ajira kwa vijana na kuondokana na umasikini pamoja na kupambana na wimbi la madawa ya kulevya ambalo limewaathiri sana vijana wa Zanzibar.

Amefahamisha kwamba serikali hii yenye muundo wa umoja wa kitaifa imeondoa tatizo moja sugu kwa wananchi kwani watu walikuwa wanalala kwa wasiwasi lakini sasa jambo hilo tokea kuja kwa muundo huu wa serikali tatizo hili halipo na litakuwa historiya katika nchi ya Zanzibar ambapo Maalim aliwataka wananchi kulithamini suala zima la kuwepo amani na utulivu ili wananchi wasireje tena katika mtafaruku huo..

“Kuwepo amani na utulivu ni muhimusanakatika nchi yoyote na ndio mwanzo wa maendele na jambo hili ndilo lililowapa moyo wawekezaji kuja kuwekeza katika nchi yetu, kuja kwa wawekezaji hapa nchini kutapelekea vijana wengi watapata ajira kupitia wawekezaji hao” alisema Maalim Seif.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s