Wawekezaji wataka pombe

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sherif Hamad

WAWEKEZAJI katika sekta ya utalii Kisiwani Pemba wamelalamikia tatizo la miundo mbinu na ukosefu wa bidhaa muhimu zinazohitajika kwa watalii kukosekana jambo ambalo limekuwa likichangia kukosekana kwa watalii wengi kisiwani humo.

Wawekezaji hao wameyaeleza hayo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais waZanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad katika ziara yake kisiwani humo ambapo alitembelea maeneo mbali mbali ikiwemo katika sekta za utalii ambazo kwa ksi kikubwa zinachangia pato la taifa nchini.

Meneja wa Pemba Misali Beach Resort, Ajuwedi Mrisho alisema  ukosefu wa bidhaa muhimu, ikiwemo pombe, mbogamboga na baadhi ya vyakula vyenye viwango vinavyohitajika na wageni ni tatizo linalowakabili katika hoteli zilizopo kisiwani hapo ikiwem hoteli yake

Alisema tatizohilolimekuwa likiwarejesha nyuma wawekezaji kwa kuwa wageni wengi wanapokuja katika hoteli za kitalii wanategemea kupata huduma za vinywaji na vyakula vyenye viwango hivyo kukosekana kwa huduma hizo muhumu kunawafanya wanapoondoka kutorejea tena katika hoteli hizo.

Alisema ingawa pombe hupatikana kwa baadhi ya wakati lakini mara nyingi hukosekana kama ambavyo hukosekana kwa mboga mboga ambapo kilimo cha mbogamboga bado hakijapewa msukumo mkubwa kisiwani humo na wamekuwa wakitegemea bidhaa kutoka tanga na sehemu nyengine zaTanzaniabara .

Kwa upende wake Meneja wa Hoteli ya Mbuyu Mkavu Resort, Seif Said alimweleza Maaalim Seif na ujumbe wake kwamba wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa hasara kutokana na ukosefu wa maji safi na salama na jinsi tatizo la umeme linavyowaathiri katika uendeshaji wa hoteli yake iliyopo Wawi Mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema tatizo hilo linakwamisha lengo lake la kutoa ajira kwa vijana wapatao 150 na badala yake ameweza kuajiri vijana 15 pekee sambamba na kushindwa kuongeza vyumba kwa ajili ya wageni kutokana na mapato duni anayopata na kuiomba serikali kulichukua suala hilo ili kulifanyia kazi kwani wanafanya biashara katika mazingira magumu sana.

.

Akijibu malalamiko ya wawekezaji hao wazalendo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sherif Hamad amekiri serikali ya umoja wa kitaifa kukabiliwa na changamoto kadhaa katika utekelezaji wa mipango yake hasa katika sekta ya utalii lakini aliwaahidi wawekezaji hao kufuatiliwa malalamiko yao na kupatiwa ufumbuzi kwani serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto zote zilizopo.

Alisema katika juhudi za serikali za kuimarisha sekta ya Utalii nchini serikali inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo miundo mbinu katika sekta ya barabara katika maeneo mbali mbali Kisiwani Pemba na miundo mbinu ya maji na umeme wa hakika katika baadhi ya maeneo.

.

Maalim Seif ameyasema hayo juzi kwa katika ziara yake ya siku mbili kutembelea miradi ya hoteli za kitalii zinazomilikiwa na wawekezaji wazalendo katika maeneo ya Vitongoji na Wesha huko Kisiwani Pemba ambapo katika ziara yake alifuatana na waziri wa Habari Utamaduni na Utalii, Abdillah Jihad Hassan na maafisa wa wizara yake..

Sekta ya utalii Kisiwani Pemba bado haijaimarika kutokana sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, ukosefu wa umeme wa uhakika na tatizo la majisafina salama katika maeneo kadhaa ya kisiwa hicho hasa katika maeneo yenye hoteli hizo kubwa za kitalii.

Kufuatia hali hiyo Maaalim Seif amesema mbali na changamoto hizo ambazo serikali ya umoja wa kitaifa inakabiliana nazo lakini serikali itaendelea kuthamini juhudi za wananchi katika kukuza sekta hiyo yenye kuongeza pato la Taifa, kutoa ajira na fursa za kibiashara kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya uwekezaji huku akiwapa moyo wawekezaji wazalendo kuendelea na juhudi za uwekezaji nchini

Akizungumzia matatizo yanayowakabili wawekezaji hao, Maalim Seif alisema Serikali itayazingatia matatizo na changamoto zinazowapata wawekezaji hao hasa wazalendo kwa umakini mkubwa kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wake ili kuvutia wawekezaji zaidi kuja kuwekeza katika kisiwa hicho ambacho kina utajiri wa rasilimali zake za asili.

Makamu wa kwanza wa rais alisema Serikali ina dhamira ya kulitafutia ufumbuzi tatizo la usafiri wa anga linalokikabili kisiwa hicho kwa kupanua na kuimarisha uwanja wake wa ndege,ili kutoa fursa kwa mashirika ya ndege kutoa huduma zao kwa uhakika na kuwepo ushindani, hatua itakayopunguza viwango vya nauli za ndege kwa watalii ili wafike katiak kisiwa hicho kwa lengo la kutanua biashara zaidi kisiwnai Pemba.

Aidha Maalim Seif aliwapongeza wawekezaji hao kwa mchango wao mkubwa kwa taifa licha ya kukabiliwa na changamoto hizo lakini wameweza kuwekeza katika nchiyaohuku wakikabiliwa na mazingira magumu katika uendeshaji wa miradi hiyo lakini bado hawajavunjika moyo katika kuwekeza nchi kwao.

Katika ziara hiyo ya siku mbili Makamu wa kwanza wa Rais alipata fursa ya kuyatembelea makumbusho yaliopo mjini Chake, ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya siku ya Makumbusho duaniani.

Advertisements

3 responses to “Wawekezaji wataka pombe

 1. mimi kila siku nauliza swali hili lakini sipati jibu hasa kwenye safari ya maalim seif za nje na za ndani lakini hatuzioni picha lakini namuona balozi seif zinawekwa picha za safari zake zote japo za kutoa kadi za c c m au maalim hana mpiga picha wake

 2. Leo nimeamini ule usemi maarufu wa kiswahili usemao “nyani akimaliza miti huja mwilini” Wakati sakata la ndugu zetu wa huko zanzibar ktk kijiji cha Pwani mchangani kuondoa uovu kwa mikono yao likiwa bado halijamalizika sasa nyani anaonekana kuwanyemelea ndugu zetu wa Pemba. Kutokana na nilivyofahamu makala hii inaonekana kuwa utalii hauwezi kwenda bila ya vileo? Jibu ni kuwa unawezekana lakini tunashindwa kuwa na sauti ktk nchi yetu wenyewe hebu angalia hii kauli ya Bwana Ajuwedi ati kisiwa cha Pemba utalii haujaimarika sababu hakuna vileo,
  Naomba niweke wazi kuwa hatuwezi kufaidiki kwa aina hii ya utalii tunayoiendesha hata kiama. Hivi kwa mtu mwenye akili zake ulevi ndio kutalii au ni laana. Hapa kwetu Zanzibar tunajisifia kwa sekta ya utalii laikini ukiangalia kwa undani faida yake wala tija bado haionekani.
  Hebu angalia asilimia kubwa ya vijana ktk vijiji kama vile Nungwi,Kiwengwa,Kizimkazi nk hawana ajira za kutambulika katika sekta ya utalii. Badala yake watu kutoka maeneo ya Bara wanadhibiti sekta hii kila nyanja. Huku Wazanzibari wakiambulia mporomoko wa maadili na uchafuzi wa mazingira.
  Ninachowataka viongozi wetu wasikurupuke katika kufanya maamuzi, kama tunataka utalii uendelee kuwa setka muhimu ya kiuchumi kuna haja ya kuipitia upya sera ya uwekezaji katika utalii ili iende sambamba na mila na silka zetu na kuwapatia manufaa wananchi wote wa Zanzibar.
  Vyenginevyo yale yaliyotokea Pwani mchangani tuyatarajie pia kisiwani Pemba kama tutaruhusu uingizwaji wa vileo kwa kisingizio cha kuimarisha sekta ya utalii.
  Naomba kuwasilisha.

 3. Swali kwa mwandishi: Maalim Seif kajibu nini kuhusu ukosefu wa pombe?vipi itapatika?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s