Tamko letu ni hili

Naibu Amir wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Azzan Khalid Hamad

Kumekuwa na kauli nyingi tokea kamati ya bunge kuja Zanzibar, kukusanya maoni kuhusuru rasimu ya marekebisho ya katiba. Na wazanzibar wakaonesha msimamo wao kuhusu mustakbal wa nchi yao , na kuukataa mswada huo,Imekuwa ni kosa mpaka viongozi wa Dini wakaitwa wahuni.

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- E-Mail: jumiki@hotmail.com MKUNAZINI- ZANZIBAR

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
18/05/2011

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma.Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume (S.A.W.) na ahli zake na jamaa zake na waliowema katika Uslamu.

Kutokana na matukio yaliojitokeza katika nchi na ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko,chuki,na nchi kuingia katika mgogoro usio wa lazima,jumuiya ya UAMSHO imeona ichukuwe nayo nafasi kuelezea uoni wake juu ya hayo yaliojiri.

Kimsingi kuna matukio matatu yaliotokea Zanzibar ambayo sasa yanaonekana kuwa gumzo Zanzibar na Bara.

Kwanza . Suala la kuchomwa moto kwa mabanda ya biashara huko pwani mchangani

Pili. Suala la serikali ya S.M.Z chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa.

Tatu. Maoni ya Zanzibar kuhusu mswada wa mapendekezo ya marekebisho ya katiba.

1. Suala la tukio la pwani mchangani la kuchomwa moto mambanda ya wafanya biashara linapotoshwa kwa makusudi na watu wasioitakia Zanzibar kheri.
2. Sikweli kama mabanda hayo yaliochomwa ni 70. kama livyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, idadi ni 29.
3. wamiliki wa mabanda hayo si wabara kama inavyo elezwa 27 ni ya wazanzibar na mawili tu ndio ya wabara.
4. sikweli kua tukio hilo ni la kisiasa bali ni la kijamii baada ya malalamiko ya wananchi kulalamika kutokana na vitendo vya ubakaji,umalaya,ulevi,mauaji, biashara ya unga,
5. si suala la kuvunja muungano kwani baada ya malalamiko hayo na kuthibitishwa na vyombo husika serikali za mitaa iliwataka wafanya biashara hao kuondoka katika eneo hilo ifikapo tarehe 01/05/2011 wawe wameondoka katika eneo hilo sasa je serekali za mitaa zilitaka kufunja muungano?
6. sikweli kuwa wabara wanafukuzwa au kunyanyaswa Zanzibar ,wapo wafanya biashara wengi mji mkongwe marikiti wauza njugu,wanaofanya kazi mashambani za kulima mbona hawa hawajabughudhiwa? Jibu hawajafanya vitendo au biashara za uhuni unga,ulevi, nk.
Na hii hoja ya kuwa wazanzibari wapo bara mbona habughudhiwi suala ni wazanzibar gain wanaofanya biashara ya ulevi,unga ubakaji,ukahaba,halafu serikali ikawaachia kwa kisingizio cha muungano?
7. suala nani kachoma na kwanini kachoma liko mahakamini tuiwachie mahakama iamumuwe kwa mujibu wa sheria.

Masikitiko yetu makubwa na yenye masuala mengi bila jawabu ni kauli ya waziri wa mambo ya ndani mh:Shamsi Vuai Nahodha kukurupaka na kuwa hawa waliochoma ni wahalifu ,wanataka kufunja muungano na yeye kama waziri atahakikisha waliohusuka wanachukuliwa hatua.sasa suala kuhusu hawa wafanya biashara kharamu,ambao wanachi na vyombo vya serikali vimeamua wahame,je mbona hawa hakutaja sababu zilizopelekea kupewa amri ya kuhama?
Kauli za Mh:Nahodha zimewachukiza waislamu na wazanzibar na wameanza
Kumtafsiri kuwa ni miongoni mwa wasioitakia mema Zanzibar .

Tunawasihi waislamu na wananchi kwa jumla kutokubali katika kipindi hichi kupokea fitna za kutaka kuwagawa na kupandikiza chuki baina yetu.

Pili tunaiyomba serikali kuchukuwa khatua zinazo faa kwa gazeti la NIPE HABARI, kutokana na taarifa zake za kuhatarisha amani ya nchi za tarehe 13-19 mei 2011 kwa taarifa zake zilizopewa nafasi ya mbele UZANZIBARI,UZANZIBARA SASA WANUKIA ZANZIBAR. Ni taarifa zinazo weza kulitia taifa katika khatari ya vita vya kikabila na dini,

Pili: suala la serikali ya S.M.Z. yenye kufuata mfumo wa umoja wa kitaifa.

Kumeanza kujitokeza watu kutaka kujenga fitna ili wazanzibar wanze chuki na viongozi wao na kuidhofisha serikali na kuirejesha nchi ya Zanzibar katika matatizo yale ya nyuma

Kidogo tukumbushe angalau watu wajielewe tunapo toka na tulipo sasa

Kwa miaka 46.kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 2005, Zanzibar imeshaingia katika chaguzi sita zinazohusisha vyama vingi vya siasa, lakini matokeo ya chaguzi zote hizo ni kudhalilika kwa waislamu,dini yao na utamaduni wao.Hakuna uchaguzi wowote wa vyama vingi ambao umepita Zanzibar, bila ya kuwacha athari mbaya kwa wazanzibari.matokeo yake ni kuwa kila uchaguzi mmoja unapofanyika huwa msingi umechimbwa kwa jengo la mateso na mfarakano kwa uchaguzi ujao.

Kwa mfano, uchaguzi wa pili wa juni 1961, chuki ya utumwa na ubwana,na Uarabu na Uafrika iliyopandikizwa kwa makusudi,ilipelekea waislamu zaid ya 70 kuuliwa huku watoto wa kiislamu katika kijiji cha bambi wakateketezwa kwa moto kwenye tanuri la mbata katika kijiji cha bambi.

Uchaguzi wa 1995 uliofanyika baada ya miaka zaidi ya 30 tangu mapinduzi ya 1964 na kufutwa kwa vyama vingi,haukupunguza chochote katika madhila ya waislamu wa Zanzibar,isipokuwa kuongeza.fitna ya upemba na uunguja ilipaliliwa na taasisi za dola na matokeo yake yakawa ni kuwafanya waislamu wan chi hii waangaliane kwa misingi ya maeneo wanayotoka na sio kwa Mungu Mmoja wa Haki wanayemuuamini na kumuuabudu. Badala ya kusimama na kalima tukufu ya laa ilaah illallah,muhamadarasuulullah, waislamu wa Zanzibar wakawa wanasimama na kauli za upemba na uunguja,uarabu na uafrika na ubwana na utumwa!

Uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 mambo yakawa ni yale yale. Tena majeshi yakamwagwa mitaani yakiwa na silaha za kivita. Rais wa wakati huo wa Tanzania, ambaye ni Amiri jeshi mkuu,Benjamin mkapa, alipoulizwa na waandishi wa habari sababu za kupeleka majeshi na vifaru Zanzibar,naye aliwauliza kulikuwa na sababu gain kwa wamarekani kupeleka wanajeshi iraq ! Kwa hivyo nchi ya waislamu ya Zanzibar ikawa imevamiwa na majeshi ya kigeni kama vile iraq ilivyokuwa imevamiwa na marekani. Matokeo yake ikawa ni muendelezo wa kile Rais Jakaya kikwete alichokuja kukiita “mpasuko” wa Zanzibar .

Hata baada ya matokeo ya chaguzi hizo na matokeo kutangazwa, waislamu wakawa wakifuatwa majumbani na misikitini kupingwa na kudhalilishwa kupita kiasi. Matokeo yake, makundi ya vijana wa kiislamu wakaanza kuhama visiwa hivi na kukimbilia ughaibuni,ambako wameselelea hadi leo, Miongoni mwa athari za vijana hao wa kiislamu wa kizanzibari kuselelea ugenini ni kupoteza kwa maadili ya dini yao na hivyo kuudhoofisha Uislamu.

Kwetu sisi huu ni mpasuko baina ya Waislamu, ambao mashiko yake hayako katika uislamu lakini athari zake zinawapata waislamu wa Zanzibar.tunaamini kwamba Zanzibar inapigwa vita kwa sababu ya Uislamu wake.

Tukumbuke kulijitokeza taasisi za kigeni jumuiya ya madola na pia kamati ya vyama vya siasa vyote vilishidwa kuziba mpasuko huo.hii imetokana na wengine hawakuwa na nia nzuri na Zanzibar

Baada ya madhara yote haya ambayo yamegharimu maisha ya watu, mali kupotea na mateso ya kila aina, wanzanzibar wenyewe wenye uchungu na nchi yao wakaona huku inakoelekea Zanzibar ni kubaya na wakuionea huruma Zanzibar ni wenyewe.
Mh: Amani Karume na Mh: Maalim Seif wakaamua kuzika yale yote tulioyaeleza kwa ufupi yakaja maridhiano, na nia ni kujenga Zanzibar mpya yenye amani utulivu umoja na maendeleo.sote tukakubali kufuta tafauti zetu na kujenga umoja na tukaahidi kushirikiana na viongozi kujenga Zanzibar mpya yenye maendeleo. Na hilo litafanikiwa kwa kuwepo serikali ya umoja,wengi wa wazanzibari wakawafiki hilo .

Sasa matunda ya maridhiano tumeanza kuyaona katika uchaguzi mkuu 2010 namna ya amani utulivu ulivyo tawala na hata baada ya matokeo wote wazanzibari walisherehekea kwa pamoja. Hakuna aliyepingwa,kubakwa,kuuliwa,wala kuharibiwa mali.haya ndio maamuzi ya wazanzibar.

Sasa kumeanza kujitokeza watu kutaka kuidhofisha juhudi hii yote kwa kisingizio cha kuwa serikali iliyopo haina la maana.na kuanza kuwakashfu viongozi wa juu kuwa waregevu. Hawa tunawahisabu ni maaduwi wa Zanzibar . na upo wasisiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa bara hawakupendezewa na hali hii na wengine wakataka kuwafurahisha kwa vitendo na kauli ili waonekane wao wema.au bora kuliko wengine. Na hii imetutia wasiwasi zaidi baada ya afisa wa ubalozi wa marekani alioko Zanzibar kuanza kupita kuhoji watu kuhusu uwoni juu ya serikali na tukio la pwani mchangani.hatua ya afisa huyu,inaweza kusababisha mgawanyiko, tuko macho na hatua za ya afisa huyo, na tukibaini kuna uchochezi au fitna hatuto weza kumvumlia.

Tunatamka wazi hatuko tayari kumnyamazia kiongozi au yoyote awe wa nje au ndani
Kutaka kuleta fitna na mgawanyiko miongini mwetu

Suala la ugumu wa maisha kupanda kwa bei bidhaa,serikali inalielewa na tunaamini Rais wa Zanzibar.na baraza lake wako makini kulitafutia ufumbuzi,huku tukiamini mabadiliko yatapatikana,

Si kweli kwamba serikali haina la maana inalofanya wanaosema hivyo wanataka kujenga fitna kwa wazanzibar waanze kuchukia serikali yao .

Tunasema nafasi hiyo haipo tena Zanzibar .

Wito wazanzibar tuwe macho na maaduwi

Suala la Tatu : Kuhusu Muungano

Kumekuwa na kauli nyingi tokea kamati ya bunge kuja Zanzibar , kukusanya maoni kuhusuru rasimu ya marekebisho ya katiba. Na wazanzibar wakaonesha msimamo wao kuhusu mustakbal wa nchi yao , na kuukataa mswada huo,

Imekuwa ni kosa mpaka viongozi wa Dini wakaitwa wahuni,

Mengi yamesemwa na hoja mbali mbali zinatolewa kulazimisha wazanzibari kukubali Muungano.tunasema miaka 47 ya Muungano huu umedumu kwa heshima na ustahamilivu wa wazanzibar.na kwa muda wote wamezibwa watu mdomo kuhoji au kukosowa kuhusu Muungano, tunasema karne hizo zimekwisha.

Muungano huu tokea kuundwa kwake umekuwa na kasoro nyingi na kuundiwa tume 21 na bado kasoro zipo pale pale.

Nasaha zetu iko haja kujadiliwa upya muungano na pande zote mbili na kushauriwa watanganyika na wazanzibar kuhusu mfumo wa muungano wanaoutaka,kinyume na hivyo kunaweza kukazuka mgogoro mkubwa na unaoweza kuleta uvunjifu wa amani

Mwisho
Tunatowa wito kwa serikali ya Zanzibar kulitatuwa tatizo la wafanya biashara wa jua kali ambao kwa muda wa miezi mine maduka yao yamefungwa, ingawa shauri lao lipo mahakamani.serikali ifikirie njia ya kuwaokowa wafanya biashara hao ili kuondosha dhana potofu na maaduwi wakapata njia ya kuitia sumu jamii.

WABILAH TAUFIQ

AZZAN KHALID HAMDAN
NAIBU AMIRI (JUMIKI)

Advertisements

3 responses to “Tamko letu ni hili

  1. Well said. Nadhani hata sisi Watanganyika tunapaswa kujiambia tunapopewa taarifa kama hizo za vyombo vya habari na wanasiasa

  2. Naunga mkono kauli ya JUMIKI mia kwa mia. Allah atujaalie kheri na mafanikio Zanzibar yetu iwe ya neema na mshikamano kwa wazanzibari wote. amin.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s