Kina mama juu

Wanawake wakutana Zanzibar

MKE wa rais waZanzibarmama Mwanamwema Shein ametoa wito kwa serikali na taasisi binafsi kuendelea kuwasaidia wanawake ambao wengi bado wanakabiliwa na chnagamoto nyingi zinazokwamisha maendeleoyao.

Katika hotuba yake fupi wakati wa kufunguwa mkutano wa kimataifa wa wanawake uliyowashirikisha akinamama wajasiri amali kutoka zanzibar, na nchi za Czech na Slovak, Mama Shein alisema bado wanawake wanahitaji elimu zaidi na fursa sawa kukopa fedha.

“Wanawake waZanzibarwamekuwa wakijitumasanakatika kujenga nchi. Wanawake wengi wanafanya kazi za ujasiri amali, lakini bado wanahitaji msaada wa kuwaendeleza hasa katika elimu na nyenzo,” alisema mama Shein katika mkutano huo uliyofanyika Hoteli ya Waridi Beach Resort, Puani- Mchangani Unguja juzi.

Mama Shadya Karume ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo uliyowakutanisha wanawake hao kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili, pamoja na nafasi ya elimu katika kukuza biashara zao, alisema kuwa ukosefu wa elimu na ujuzi, pamoja na unyanyapaa bado nivikwazo kwa mwanamke.

Mama Shadya ambaye ni First Lady Mstaafu alitoa wito kwa serikali kuendelea kutoa upendeleo kwa wanawake katika fursa ya elimu na upatikanaji wa fedha za miradi.

“Wanawake wengi wanakimbilia katika ujasiri amali kwa sababu ya kutengwa katika kazi nyenginezo, hata hivyo bado idadi ya wanawake katika ujasiri amali ni ndogo kulinganisha na wanaume, na pia fursa za mikopo bado ni finyu, ni lazima wanawake wasaidiwe ili waweze kufikia malengo ya kuondokana na umasikini na kujitegemea kiuchumi,” alisema Shadya.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, na ushirika Bw Haroum Ali Suleiman alisema kuwa mchango wa wananwake wajasiri amali katika uchumi wa taifa ni mkubwa, lakini atakawataka wanawake kujiendeleza zaidi ili kuhimili ushindani wa kibiashara katika dunia.

Makamo mwenyekiti wa Bunge Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Czech Mama Alena Gojduskova, alisisitiza kuwa wanawake wanahitaji kuwa huru kiuchumi, na fursa sawa na wanaume katika kukopa “ili pia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia nyumbani na makazini.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s