Ziara ya Dk Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk ALi Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mzee Khamis,alipotembelea eneo la viwanja vya Mnazi Mmoja jana,akiwa katika ziara ya kutembelea sehemu mbali mbali za Mkoa wa Mjini Magharibi, zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amenza ziara ya kuzitembelea Wilaya zote za Unguja na Pemba, ambapo alianzia Wilaya ya Mjini Magharibi kwa kutembelea maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ufunguzi wa skuli ya Chekechea Meya, iliyopo Jimbo la Mpendae.

 

Mara baada ya uzinduzi wa skuli ya msingi ya Meya, Dk. Shein alitoa nasaha zake ikiwa ni pamoja na kuwapongeza wazee wa Meya kwa hekima waliyotumia katika kubuni mradi huo wa ujenzi wa skuli hiyo ya chekechea na kusaidiana bega kwa bega katika ujenzi wake.

 

Alisema kuwa hakuna kitu bora duniani isipokuwa elimu, hivyo alisisitiza sekta ya elimu ni lazima iendelezwe hasa kwa vijana kwani ndio nyenzo pekee ya maisha ya mwanaadamu.

 

Dk. Shein alisema kuwa katika vipaumbele vikubwa vilivyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni pamoja na kuiimarisha sekta ya elimu.

 

Alieleza kuwa moja katika malengo makubwa ya Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ni kuwapa bure elimu wananchi wote wa Unguja na Pemba.

 

Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuiimarisha sekta ya elimu sanjari na kuwaelimisha vijana wadogo na wakubwa kwa lengo la kupata huduma hiyo ya elimu.

 

Aidha, Dk. Shein alitoa wito kwa viongozi na wananchi kukusanya nguvu zao katika kukisaidia kituo hicho ambapo yeye mwenyewe binafsi alianza kuchangia hapo hapo shilingi milioni saba kwa ajili ya skulu hiyo ya chekechea ambayo bado ina changamoto inazozikabili ikiwemo uhaba wa vifaa vya kusomeshea na vikalio.

 

Katika risala yao wananchi wa Meya walitoa shukurani zao kwa viongozi mbali mbali pamoja na watu binafsi kwa michango yao ya hali na mali iliyopelekea kujengwa hadi kumalizika kwa ujenzi wa skuli hiyo.

 

Walieleza kuwa hadi kumalizika ujenzi wa skuli hiyo shilingi milioni thalasini zimetumika amKatika ziara yake hiyo, Dk. Shein alianzia afisi ya Mkoa wa Mjini Magaharibi na kupata maelezo juu ya shughuli za mkoa huo zikiwemo shughuli za sekta za maendeleo ikiwemo elimu, maji safi na salama, afya, mazingira. Shughuli za kijamii na nyenginezo.

 

Mapema  Dk Shein mara baada ya kuondoka katika afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  alifika katika viwanja vya MnaziMmoja na kujionea athari za kimazingira katika viwanja hivyo na kupata maenelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ndugu Mzee Khamis.

 

Mara baada ya kuondoka hapo na msafara wake Dk. Shein alitembelea Bwawani na kuangalia athari za kimazingira katika bwawa la bwawani na kupata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Manispaa pamoja na maelezo kutoka Idara ya Mazingira  juu ya bwawa hilo.

 

Aidha, wahusika wote hao walisisitiza haja ya kuundwa kamati ya pamoja itakayowahusisha watu wa Mazingira, Manispaa pamoja na wengine kutoka sekta za serikali ili kuangalia uwezekano wa kulitamfutia ufumbuzi bwawa hilo.

 

Katika maelezo yao wahusika hao walisisitiza haja ya kutafutia ufumbuzi wa maji yanayotuama bwawani hapo kutokana na kuwa maeneo mengi ya mjini maji taka yake huishia katika eneo hilo.

 

 Dk. Shein alimalizia ziara yake hiyo ya Wilaya ya Mjini hivi leo kwa kutembelea Hospitali ya Daraja la Pili iliyopo Mpendae, mjini Unguja ambayo imejengwa kwa mashirikiano ya viongozi, wananchi, Mashirika, Mawizara, Benki pamoja na wahisani wengine wa ndani na nje ya Zanzibar.

 

Akitoa nasaha zake katika hospitali hiyo mara baada ya kuitembelea na kupata maelezo, Dk. Shein alisema kuwa serikali ina lengo la kuiimarisha na kuiongezea uwezo hospitali hiyo ya Daraja la pili pamoja na ile ya Kwamtipura kama alivyoahidi katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

 

Dk. Shein alieleza kuwa katika kampeni za uchaguzi uliopita alitoa ahadi ya kuiimaisha hospitali hiyo na nyengine za daraja la pili. Aidha, alisema kuwa lengo la kuzipandisha daraja hospitali zote za wilaya na mkoa lipo pale pale pamoja na kuifanya Hospitali ya MnaziMoja kuwa ya rufaa.

 

 Pamoja na hayo, aliitaka Wizara ya afya kukaa pamoja na kamati ya ujenzi ya hospitali hiyo kuangalia namna ya kuiendeleza ujenzi katika awamu zinazofuata na kusisitiza kwa Wizara ya afya kuwa katika vipaumbele vya bajeti yao ya mwaka huu hospitali hiyo nayo iwemo.

 

Nao wananchi wa Mpendae katika risala yao walieleza kuwa hadi kumalizika kwa ujenzi wa hospitali hiyo shilingi milioni 400 zinahitajika  ambapo hadi sasa shilingi milioni 152 zimeshatumika.

 

Hospitali hiyo tayari imeshaanza kufanya kazi ambapo imekuwa ikitoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo la Mpendae na maeneo mengine ya jirani.

 

Dk. Shein ataendelea na ziara yake hapo kesho katika Wilaya ya Magharibi ambapo ataweka  jiwe la msingi la skuli ya Bweleo pamoja na kutembelea maeneo mengine ya miradi ya kilimo, afya na elimu katika Wilaya hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s