Sita mahakamani kwa kuharibu mali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein serikali yake inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo kero mbali mbali za wananchi ambazo zinaonekana kukosekana kuchukulikiwa hatua zinachochea cheche za uvunjifu wa amani nchini

Sita mahakamani kwa kuharibu mali

JUMLA ya watu sita jana wamepandishwa katika mahkama ya mkoa Vuga Mjini Zanzibar wakikabiliwa na tuhuma za kuchoma moto mabanda ya wafanyabiashara katika kijiji cha Pwani Mchangani wilaya ya Kaskazini Unguja.

Walioshitakiwa ni ni pamoja na Mohammed Masoud Afadhali (21), Mwinyi Abdallah Msanif (22) na Hassan Makame Chande (21) wengine ni Haji Ame Idd (45), Talib Faki Ame (60) na Mohammed Haji Sheha (21).

Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Mohammed Khamis Hamad Mwanasheria wa serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), aliieleza mahakama hiyo kwamba mnamo tarehe 5 Mei watuhumiwa hao wote kwa pamoja walichoma moto mabanda ya biashara na kusababisha hasara kubwa.

Alisema watuhumiwa hao wanakabiliwa na kosa ya kuharibu mali kinyume na kifungu cha 324 (a) cha sheria namba 6 sheria mwaka 1984 katika sheria za Zanzibar.

Washitakiwa hao walielezwa mahakamani hapo kwamba kwa pamoja walichoma moto mabanda ya wafanyabiashara ya wajasiriamali na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha za wafanyabiashara hao katika maeneo yao ya biashara mashitaka ambayo kwa pamoja walikana kufanya kosa hilo .

Mwanasheria huyo alisema watuhumiwa hao wamesababisha hasara kubwa kutokana na uamuzi wao wa kuchoma moto maeneo ya bishara ambapo jumla ya shilingi milioni 80,470,000 pamoja na paundi 70 za Uingereza na dola 60 za Marekani zimeteketea katika tukio hilo la uchomaji moto mabanda hayo .

Washitakiwa hao walipotakiwa kujibu shitaka hilo walikana, ambapo upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wake bado unaendelea.

Baada ya hoja hizo za upande wa mashitaka, upande wa utetezi unaosimamiwa na Wakili wa Kujitegemea Abdallah Juma uliwaombea wateja wake wapatiwe dhamana kwa vile ni haki yao kikatiba kupewa dhamana .

Alisema kuwa, kwa kuzingatia kifungu cha 150 (1) cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar , shitaka linalowakabili ni miongoni mwa mashitaka yenye dhamana hivyo wanapaswa kupewa dhamana .

Aidha wakili Juma alidai kuwa, kifungu hicho kimeainisha mashitaka yasiyokuwa na dhamana ambayo ni uhaini, mauaji, wizi wa kutumia silaha pamoja na kusafirisha dawa za kulevya, na kubainisha kuwa shitaka linalowakabili wateja wake ni shitaka lenye dhamana.

Wakili huyo alisema kwamba wateja wake wana wadhamini madhubuti na wapo tayari kutekeleza masharti yote ya dhamana watakayopewa, sambamba na kuhakikisha wanawafikisha mahakamani kila watakapohitajiwa wakati kesi yao ikiendelea.

Upande wa mashitaka ukiongozwa na Mohammed Khamis ulipinga hoja hizo za upande wa utetezi na kuiomba mahakama hiyo isiwapatie dhamana washitakiwa hao, kwa madai kwamba hatua hiyo ya dhamana inaweza kuingilia kati upelelezi ambao bado haujakamilika.

Mwendesha mashitaka huyo alidai kwamba, hivi sasa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea, na kuna washitakiwa wengine bado wanatafutwa ili waweze kuunganishwa katika kesi hiyo pamoja na wenzao.

Licha ya pingamizi hizo, Mwendesha Mashitaka huyo alikubaliana na upande wa utetezi kuwa dhamana dhidi ya washitakiwa hao ni haki yao ya msingi nay a kikatiba lakini aliiomba mahakama hiyo iwapo itaamua kuwapatia dhamana izingatie ukubwa wa kosa hilo lililotendeka.

Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Vuga George Joseph Kazi aliwaamuru washitakiwa hao kwenda rumande hadi Mei 23 mwaka huu, ambapo ombi lao la dhamana litakapozingatiwa siku hiyo na kesi hiyo kuakhirishwa.

Wakati kesi watuhumiwa wakifikishw amahakamani hapo mamia ya wananchi kutoka sehemu mbali mbali hasa kutoka vijijini walionekana kufika katika mahakama hiyo ya Vuga kuja kusikiliza kesi hiyo inavyoendeshwa huku baadhi ya wananchi hao wakiwa wamekaa nje ya mahakama kutokana na kuwa sehemu ya mahakama hiyo ni ndogo kulingana na wingi wa wananchi waliofika.

Advertisements

One response to “Sita mahakamani kwa kuharibu mali

  1. Pingback: Sita mahakamani kwa kuharibu mali·

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s