Zanzibar imeonesha mfano

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Mohammed Bakari akitoa mada juu ya hali kabla ya kura ya maoni ya kuruhusu kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa mwaka 2010, katika warsha ya siku tatu iliyofanyika kwenye Hoteli ya Bwawani semina ambayo imeandaliwa na Kamati ya Wangalizi ya Uchaguzi (TEMCO) kwa ajili ya kujadili ripoti ya mwisho ya waangalizi wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka 2010.

MHADHIRI wa Chuo Kikuu chaDar es Salaam, Dk. Mohammed Bakari amesemaZanzibaritazidi kupiga hatua katika suala la ushirikishaji wa wananchi katika kumaliza migororo ya kisiasa na kijamii baada ya kukubali mfumo wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Alisema kutumia mfumo wa kuwashirikisha vyama vyengine bua siasa katika serikali ni mfumo mzuri kwa kuanzia hasa kwa kuzingatia hali ya kisiasa ya visiwa vya Unguja naPembaambapo ushindani wake unakaribiana.

Dk Bakari alikuwa akitoa mada juu ya hali kabla ya kura ya maoni ya kuruhusu kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa mwaka 2010, katika warsha ya siku tatu iliyofanyika kwenye Hoteli ya Bwawani semina ambayo imeandaliwa na Kamati ya Wangalizi ya Uchaguzi (TEMCO) kwa ajili ya kujadili ripoti ya mwisho ya waangalizi wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka 2010.

Bakari alisema uamuzi waZanzibarkuunda serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kura ya maoni ni mwanzo mzuri wa juhudi za kujenga mfumo rasmi wa kuwashirikisha wananchi katika kuamua mambo makubwa ya kitaifa.

Katika mada yake Dk. Bakari alisema uamuzi wa kutumia kura ya maoni kuamuaZanzibariwe na muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa, ulikuja baada ya kuundwa sheria iliyoruhusuZanzibarkuwa na katiba yenye mfumo wa kura ya maoni.

Hatua hiyo alisema imesaidia kurejesha amani na utulivu Zanzibar kupitia uchaguzi wa mwaka 2010, baada ya changuzi zote zilizoshirikisha vyama vingi kuanzia mwaka 1961 hadi 2005 kukumbwa na migogoro mikubwa kutokana na ushindi wa vyama kupishana kwa kura kidogo hali ambayo baadhi ya wakati huvuta mivutano mikubwa kwa wanasiasa na wafuasi wao.

Zanzibarbaada ya kuwa na katiba yenye mfumo rasmi unaoruhusu rasmi wananchi kushirikishwa katika kuamua kwa njia ya kura ya maoni juu ya aina ya mfumo wa serikali wanayotaka, uhasama na chuki za kisiasaZanzibarumetoweka na sasa hali imekwa shuwari jambo ambalo linapaswa kuendelezwa katika chaguzi nyengine zijazo.

“Zanzibarkatika uchaguzi uliopita imeonesha mfano mzurisanajambo ambalo kwa maoni yangu naonaTanzaniabara wanapaswa kuiga mfano huo ili suala la kura ya maoni katika kuamua mambo makubwa ya kitaifa liwe rasmi (kikatiba) kuliko kuwa la matakwa ya viongozi peke yake ambayo mwishowe huzusha mivutano ya wanasiasa,” alisema Dk. Bakari.

Mhadhiri huyo aliwaambia hadhara ya waliofika katika semina hiyo kwamba kulikuwa na dhamira ya kweli kwa viongozi wa kisiasa kumaliza chuki na migogoro ya kisiasa na ndio sababu ya kufanikiwa ambapo Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad wenyewe walisimamia sualahilohadi mwisho wake.

“Kupitia makubaliano yasiyokuwa rasmi, dhamira ya viongozi hao iliwezesha kumaliza mgogoro ambao haukuweza kupatikana hata kwa njia iliyokuwa rasmi ya kutafuta maridhiano kwa njia ya mazungumzo baada ya uchaguzi mkuu uliojaa kasoro wa mwaka 1995 na licha ya kuundwa tume na kamati mbali mbali lakini suala hilo lilishindikana lakini dhamira ya mara hii ilikuwa na nguvu kwa kuwa walikusudia kumaliza migogoro kwa haki”aliongeza Mhadhiri huyo. 

Akifungua semina hiyo Makamu wa Pili wa Rais waZanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema taasisi za uangalizi wa uchaguzi zina nafasi kubwa ya kutoa ushauri unawezesha serikali kuimairisha mifumo yake ikiwa ni pamoja na muundo wa katiba.

“Masuala ya uchaguzi ni moja ya maeneo ambayo mapungufu yake tanatokana na kasoro za kikatiba,” alisema Balozi Seif.

Katiba yaZanzibarilifanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi wa mwaka jana ili kuruhusu wawakilishi wa vyama vya siasa kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa lengo la kurejesha imani ya wananchi na kuweka mazingira mazuri katika uchaguzi.

Balozi Seif alisema mabadiliko hayo yalichagua kupunguza malalamiko katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kwa maana yakuwa na tume inayoaminika na vyama viwili vya siasa ambapo kwa kiasi kikubwa wananchi wamekuwa na imani nayo licha ya kasoro ndogo ndogo ambazo hupatiwa ufumbuzi mara kwa mara.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s