Mvua yasitisha sherehe za Muungano

MVUA kubwa iliyoanza ghafla jana ilisitisha sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya muungano waTanganyikanaZanzibarkatika uwanja wa Amaan mjiniZanzibar.Sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 3;00 asubuhi ziliingia dosari hiyo huku tayari mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshakagua gwaride na kujumuika na viongozi wenzake katika jukwaa kuu.

Viongozi wengine waliokuwepo katika sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Dk Ally Mohammed Shein, Makamu wake wa kwanza Seif Sharrif Hamad na makamamu wake wa pili Balozi Seid Idd.

Wengine waliokuwepo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anna Makinda, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange, Mkuu wa jeshi la Polisi Said Mwema, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rais mstaafu wa awamu ya sita wa SMZ Dk Salim Amour.

Vilevile walikuwepo viongozi wa vyama vya siasakamavile mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Katibvu mkuu mstaafu wa CCM Philip Mangula, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia na wanadiplomasia wanaoziwakisha nchi zao nchini.

Rais Kikwete aliingia uwanjani hapo majira ya saa nne asubuhi akiwa kwenye gari la wazi na kuwapungua mamia ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo na baadaye kukagua gwaride.

Baada ya hapo gwaride lilipita mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa kasi na mwendo wa pole.

Ulipowadia wakati wa halaiki iliyoshirikisha wanafunzi 500, ndipo mvua ilianza kunyesha na baadaye kuivuruga kabisa sherehe hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo kipindi kilichokuwa kikifuata ni ngoma za asilia. Lakini mvua ilipozidi washereheshaji walitangaza kukatisha sherehe hiyo na viongozi wakaanza kuondoka.

Kauli mbiu ya sherehe hiyo ilikuwa ni “Miaka 47, tuwaenzi waasisi wetu, Tudumishe muungano, matunda ya miaka 47 ya mapinduzi na miaka 50 ya Uhuru, amani, utulivu na maendeleo ni matokeo ya muungano wetu, zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Sehemu mbalimbali za uwanja huo zilionekana kuwa wazi huku wafuasi wa CCM waliokuwa wamevaa sare nao wakiwa wachache.

Hata hivyo sherehe hizo zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Licha ya wanafunzi waliokuwa wamevaa sare nyeupe na wale waliovaa sawa na rangi za bendera ya Taifa na wafuasi wa CCM. Maeneo mengine ya uwanja huo yalikuwa wazi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Serikali ilituma mabasi zaidi ya 20 vijijini ili kukusanya watu kwaajili ya kuhudhuria sherehe hizo, lakini hawakufika.

Hali hiyo imejitokeza huku kukiwa na manung’uniko mengi kutoka kwa wananchi visiwani humo wakitaka muungano huo ufanyiwe tathimini upya.

Wakati huo huo, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar umetoa tamko kuhusu hali ya muungano.

Huku wakitoa ushahidi wa tume kadhaa zilizoundwa ili kutafuta maoni ya wananchi kama vile Tume ya Jaji Nyalali na ile ya Jaji Kisanga, jumuiya hizo zimesema kuwa muungano kati yaTanganyikanaZanzibarumekosa kukubalika ba Wazanzibari tangu siku yake ya kwanza  hadi leo.

Huku wakikilaumu CCM kwa kuhodhi muungano, wamesema kuwa nguvu zaZanzibarkatika kama mshirika mmoja kamili wa muungano huo hazipio kwa kuongezewa mambo ya muungano nay ale yasiyo ya muungano yamekuwa yakiilemeaZanzibar.

“Kwa karibu miaka yote 47 muungano huu umekuwa ni miliki ya chama kimoja cha siasa cha CCM, ukitoa miaka michache ya 1964-1977”.

Jumuiya hizo zimetaka kuwepo kwa majadiliano ya muungano ambapo wametaka pia nafasi ya Rais waZanzibarkatika muunganokamamakamu wa kwanza wa Rais.

“Mjadala wowote wa muungano ule urudishe nafasi ya rais waZanzibarkatika muungano na sio ilivyovyo hivi sasa ambapo Rais waZanzibarya maana wala amri yoyote ile katika muungano” imesema taarifa hiyo.

Advertisements

3 responses to “Mvua yasitisha sherehe za Muungano

 1. nasema ivi … MUUNGANO NDANI YA CCM HAUVUNJIKI … KUNA VIONGOZI NI VIBARAKA WA MUUNGANO HUO KWA MICHONGO YA MOJA MBIIL TATU ….. wekeni kasumba za kichama kando ….. umoja upo …lkn unahitaji vichwa vya juu vizima …sio vilivokuwepo na sera ya KIJINGA …sijakosea

 2. hakika muungano wa tanganyika na zanzibar ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya zanzibar.
  KWAHIVYO ILI ZANZIBAR KUPATA MAENDELEO NILAZIMA IPATE UHURU KUTOKA KWA UKOLONI WA TANGANYIKA

 3. Assalaam Alaaykum, Waungwana

  UMOJA, UHURU, UWADILIFU

  ZANZIBAR KWANZA

  Chenye kujengwa juu ya haramu ni haramu. Chenye kuzalikana na haramu ni haramu. Mzaliwa wa nguruwe na kondoo ni haramu sawa na nguruwe mwenyewe.

  Huu wenyekuitwa muungano umezalikana na haramu, haramu ya kuvamiwa Zanzibar kwa jina la mapinduzi. Kwahivyobasi, madhali mzazi – mavamizi – ni haramu, mzaliwa – wenyekuitwa muungano, ni haramu.

  Haramu ya muungano huu ni sawa na haramu ya mwana kondoo aliezalikana na nguruwe, kwa hukumu ya Kiislamu hakuna cha ku’tahirisha haramu ya nguruwe, hivyohivyo hakuna cha ku’tahirisha haramu ya mzaliwa wa nguruwe. Khwahivyobasi, muungano huu utaendelea kuwa ni haramu daima dawamu.

  Kutokana na hivi kuwa muungano huu ni haramu, ndivyo inavyothibi kila siku kwamba katika muda huu wa miaka 49 muungano huu haujaleta hata moja la faida kwa Zanzibar. Kinyume chake ndivyo sahihi. Kwa muungano huu ndivyo ilivyopotezwa Dola Huru ya Zanzibar na kufikishwa kuwa “ZANZIBAR SI NCHI:. Zanzibar ilikuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa tangu siku iliopata uhuru wake Disemba Kumi, 1963; Zanzibar imefutwa kuwa ni nchi na kufutwa uwanachama wake wa Umoja wa Mataifa.

  TUNAMUOMBA YEYOTE YULE ATUELEZE FAIDA YA MUUNGANO HUU. AKIFANYA HIVYO AZINGATIE KHASARA YA KUPOTEZWA DOLA YA ZANZIBAR NA KUFIKISHWA KUWA “ZANZIBAR SI NCHI”.

  Wa Billahi Tawfiiq

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s