Unganisheni vikundi vyenu


WANANCHI wanaoanzisha vikundi vya ushirika wametakiwa kufanya mabadiliko ya namna ya kuunda vikundi vyao kwa kuacha kuanzisha vikundi vidogo vidogo na badala yake kuviunganisha ili kuwa vikundi vikubwa ambavyo vitaweza kuwa na mitaji mizuri

Wito huo umetolewa jana na mke wa Makamu wa Pili wa Rais, mama Asha Seif Iddi, wakati akivikabidhi michango ya fedha kwa ajili ya kuendeleza vikundi vya ushirika, pamoja na kuwapa zawadi wanafuzi 15 waliochaguliwa kuingia skuli za michipuo kwa jimbo la Kitope.

Sherehe hiyo ilifanyika katika skuli ya Upenja Wilaya ya kaskazini ‘B’ Unguja ambapo Mama Asha alisema muundo wa sasa wa vikundi vya ushirika vinaweza kutopata mafanikio mazuri ikiwa hawataviunganisha na kuwa vikubwa.

Alisema ni kweli serikali imeamua kushajiisha waananchi kuunda vikundi vya ushirika, lakini ipo haja kwa walianza kuunga mkono hatua hiyo ya kuanzisha vikundi wakafikiria kujiunganisha ili kujiwezesha kuwa na mitaji mikubwa katika Vyama vyao.

Alisema hivi sasa utaratibu waliouanzisha katika majimbo ya kuwa na zaidi ya vikundi 10 ambavyo vimekuwa na idadi ya watu kidogo vimekuwa vikishindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa mitaji mikubwa jambo ambalo wangeweza kujiunganisha wangeliweza kupata mafanikio.

Alisema hiyo inachangiwa na watoaji wa michango kwa vikundi vya ushirika kuwa ni kidogo huku sehemu kubwa ya vyama hivyo huitaji kuinuka kwa kutegemea misaada.

Alisema haiwezekani kwa watoa misaada kuweza kuvisaidia vikundi vyote jambo ambalo huenda likasababisha vikundi vyengine vikafa huku vyengine vikiinuka.

“Kaa hapa katika Jimbo la Kitope kuna vikundi 20 vya ushirika sasa inakuwa tabu kusema namtafuta mfadhili aje awasaidie vikundi vyote hivi na hapo tutaweza kuleta mgawanyiko ikiwa vyengine vitapewa msaada na vyengine visipewe sasa ni bora mkajikusanya mkawa na vikundi vitatu ambavyo vitakuwa vikubwa” alisema mama Asha.

Akitoa mfano alisema ndani ya Jimbo hilo hivi sasa kuna SACCOS ya Mkadini ambayo wamejiunganisha na kuanzisha benki ya vijijini ambapo tayari imekuwa ikipata mikopo katika mabenki makubwa jambo ambalo limewaongezea mtaji wao kwa kufikia zaidi ya milioni 50.

Alisema ni vyema kwa vikundi hivyo vikauchukulia mfano huo kwa kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha vikundi vya ushirika viliopo kuwa katika hali nzuri.

Akizungumzia juu ya kuwapongeza wanafunzi alisema ipo haja walimu wakuu wa skuli za Jimbo hilo kuona wanaanzisha utaratibu wa kuwafanyia ukaguzi afya za wanafunzi pamoja na suala la kudumisha usafi.

Alisema inasikitisha hivi sasa kuona baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakienda skuli wakiwa katika hali mbaya ya usafi jambo ambalo linaweza likawa linachangia kutosoma vizuri.

Mama Asha, aliwaasa wanafunzi hao kuona waliopasi michepuo kufanya jitihada zaidi na sio kuridhika na walipofika na kushughulika na mambo ya mjini.

“Mme kwenda Mjini sasa tulieni huko musome tunataka muwe mfano bora wa kutotumbukia katika mambo ya starehe kwa kujiona mko mjini mkasome na wala msiregee na mambo ya Mji jikazeni” aliasa Mama Asha.

Mama Asha katika sherehe hiyo alikabidhi vitambaa vya unifomu kwa akili ya kuwapatia wanafunzi wenye yunifomu zilizo katika hali mbaya pamoja na kuwakabidhi wanafunzi wa michepuo zawadi ya fedha pamoja na yunifomu na fedha kwa vikundi vya ushirika vya Jimbo hilo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa skuli ya chekechea ya Fujoni, ambapo vitu vyote thamani yake ni shilingi milioni 200.000

Mapema Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo, aliwaasa wanafunzi hao kuona kuwa wasiridhike na walipofikia sasa lakini wahahakikishe wanajibidiisha zaidi ili waweze kufikia kupata elimu ya juu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s