SMZ hamjatutendea haki-Kanisa

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustino Shao akihutubia katika ibada ya mkesha wa Pasaka katika kanisa la Katoliki Minara Miwili liliopo Shangani Mjini Zanzibar

ASKOFU wa Kanisa Katoliki jimbo la Zanzibar Augustine Shao amesema ameshangazwa na muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kuwa viongozi wake ni watu wa itikadi ya dini moja.Askofu Shao hayo jana katika mkesha wa siku ibada ya Pasaka katika kanisa la Minara miwili Shangani Mjini Zanzibar ambapo alisema viongozi wa dini mwaka jana kabla ya uchaguzi mkuu walikemea ubaguzi wa itikadi za dini lakini alisema serikali iliyoundwa ya umoja wa kitaifa asilimia 99%.1 viongozi wake ni watu wa itikadi wa dini moja.

“Mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu 2010 tuliwaonya sana viongozi wetu wa siasa, kwamba kuna wasiwasi wa kuigawa nchi kwa misingi ya itikadi za dini. Tulikubali kwa dhati kwamba hili litatupeleka pabaya na hivyo, lkemewe kwa ukali na kwa nguu zote” alisema Askofu Shao.

Aidha alisema matarajio ya wananchi baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huenda yasifikiwe kutokana na kutokuwepo nia ya dhati ya kuleta mabadiliko hayo yaliofanyika kati ya vyama viwili vya CCM na CUF.

Akitoa vipande vya aya za Biblia Askofu Shao alisema ufufuko wa Yesu ni kielelezo kuwa mwisho wa mateso na mahangaiko ni furaha, kama wote wataamini Kristo aliye mwanga wa ulimwengu ambapo waisrail waliteseka utumwani Misri miaka 400, hatimae mwishowe walikuwa huru na kuona nchi ya ahadi kwa kuwa walikubali mabadiliko katika maisha yao hivyo aliwataka waumini kumpokea Kristu ili nchi iwe na amani na mabadiliko.

“Ndugu zangu ni muda mrefu takriban miezi sita, tumepata serikali ya umoja na serikali ya muungano watanzania wote tulikuwa na matumaini makubwa, ndio ni mapema mno kutathmini lakini kwa kusoma alama za matukio machache tunaweza kusema, matarajio tuliotarajia kwa kikubwa huenda yasifikiwe kwa sababu wengi wetu hatujaona nia ya dhati ya kutaka mabadiliko na utayari wa kupokea mawazo na changamoto za wengine”alisema Askofu Shao.

Alisema wananchi walitarajia kuona nguvu mpya na ubunifu mpya wa rika mbali mbali, changamoto za vipaji tofauti na itikadi mbali mbali katika wizara, wilaya, mikoa na taasisi za serikali lakini wananchi wanashuhudia zaidi ya mabadiliko ya nafasi ambazo hazingezi tija.

Mabadiliko yaliyofanyika katika serikali ya umoja wa kitaifa Shao alisema ni mabadiliko ya nafasi kwa viongozi wale wale mabadiliko ambayo hayana tija katika kuharakisha maendeleo ya nchi ambapo alitoa mfano wa walimu wazembe wale wale wasio na juhudi wamehamishiwa shule nyengine jambo ambalo amesema haliwezi kuongeza ufanisi kazini.

Akizungumzia suala la katiba Askofu Shao amewataka viongozi wa serikali kuwa makini katika maoni yaliotolewa katika makongamano ya kujadili katiba mpya kwa kuwa wananchi walionesha hisia zao.

“Sote tunaomba suala la katiba lichukuliwe kwa uzito wake yale yaliojiri dar es salaam na Zanzibar wakati wa kujadili katiba yalifichua hisia na matamanio ya watanzania. Tunawaasa viongozi wenzetu wazingatie hisia na matumainio hayo, na wae waangalifu kutotumia madaraka kuonesha kwamba kuna mwenye haki zaidi. Katiba inayotarajiwa ni ya watanzania wote” alisema.

Askofu Shao akizungumzia suala la kuchumi alisema maendeleo katika nchi yatapatikana haraka kwa kuhakikisha wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wanalipa kodi ipasavyo badala ya kuwabana wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwaacha wakubwa wenye utajiri.

Alisema bahati mbaya serikali imekuwa ikitoa misamaha ya kodi kwa wafanya bishara wakubwa na wawekezaji na kuwabana wafanyabishara wadogo wadogo na wakulima.

Askofu Shao alisema kwamba wananchi ambao wanatafuta riziki kwa kufanya biashara ndogo ndogo wamekuwa wakibebeshwa kodi kubwa wakati kodi hizo haziwezi kusaidia lolote katika maendeleo ya nchi.

“Kodi ya Machingana wakulima wadogo wadogo hata ikikusanywa asilimia mia moja bado itachukua robo karne tuweze kufikia maendeleo yanayotamaniwa na wananchi”alisema Askofu huyo .

Alisema iwapo serikali itasimamia vizuri ukusanyaji wa kodi Zanzibar itaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo na kufikia lengo la kupunguza umaskini kwawananchi wake badala ya kukimbizana na wafanya bishara wadogo wadogo kwa kuwataka kulipa kodi kwa biashara wanazozifanya kwa lengo la kutafuta riziki.

Kanisa la Assemble of God wamataka suala la kudmisha muungano liendelezwe na watu wenye kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Muungano wapuuzwe kwa kuwa Muungano huo umewanufaisha sana watanzania hadi sasa.

Askofu wa kanisa hilo liliopo Kariakoo Zanzibar, Dickson Kaganga alisema wapo watu wameanza kutiatia maneno kuhusu Muungano lakini amewataka watanzania kuuombea Muungano huo udumu na wasikubali kuchochewa na wale wasiopenda Muungano kuendelea.

“Yapo maneno wanaosema Muungano hatuutaki Muungano mbaya lakini sisi tunasema Muungano huu ni mzuri na tuumbee kwa Mungu ….Muungano dumu…ameen Muungano udumu …ameen ahhhh amin” alisema huku waumini wa katika hilo wakiitikia ameen

Kwa upande wao Kanisa la Anglikan liliopo Mkunazini, Dayosisi ya Zanzibar, wakisoma maombi ya yalioongozwa na Kasisi Kiongozi Emanuel Michael alisema wananchi wamekuwa wakiteseka na makali ya maisha na kuitaka serikali kuzingatia hali hiyo na kusikiliza kilio cha wananchi wake.

Amesema wakati wakati huu wenye changamoto nyingi za kimaisha Serikali ifanye juhudi za kukabiliana na na kushughulikia tatizo la mfumko wa bei ulijitokeza katika soko la ndani ya Zanzibar ambapo kwa kiasi kikubwa wananchi wanashindwa kumudu gharama za maisha.

Alisema kwamba tatizo la mfumko wa bei linaendelea kuathiri wananchi wenye kipato cha chini jambo huku serikali ikiwa imekaa kimya tangu kuanza kujitokeza tatizo hilo na wananchi wake wanazidi kuteseka na maisha.

“Tatizo lipo kwa viongozi wa kisiasa ambao hawataki kuviringisha jiwe la maisha bora wananchi wao hali ya maisha imekuwa ngumu kwa tatizo la mfumko wa bei za vyakula nchini, wananchi wanshindwa kumudu gharama za maisha”alisema kiongozi huyo.

Aidha alisema kwamba wakati huu wa kuelekea mjadala wa katiba mpya ni vizuri wananchi wakaacha jazba ili lengo la kuwa na katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liweze kufikiwa kwa muda muafaka.

“Matumaoni ya matarajio ya kanisa ni kuona waumini wake leo wanapata Baraka kwa viongozi wao wa dini wa dini kuwashajiisha na kuwaeleza kufuata maisha ya utulivu bila jazba wala chuki ili kuweza kuifanya nchi yetu kuwa pahala pa usalama zaidi” alisema Kasisi Kiongozi wa Angalikan.

Alisema matarajio ya Mungu ni kuona waumini wake wanaishi katika maisha mazuri na yenye kufuata maadili na ucha mungu.

Advertisements

One response to “SMZ hamjatutendea haki-Kanisa

  1. Askofu Shao lengo lako ni kuona Zanzibar inaingia katika Shimo la mizozo ya Itikadi za Kidini, mbona macho yako yana uoni hafifu kama wa popo,hebu angalia mbona suala lako huangalii Tanganyika na kusema pia kuwa Waislam wa huko hawatendewi haki ikiwa ni pamoja na kunyimwa kujiunga na OIC na Mahkama ya Kadhi? Kama unataka hivyo pia tafadhali iambie serikali ya Tanganyika ifanye usawa katika safu nzima ya uongozi kwani walio wengi katika serikali ya Tanganyika si Waislam bali ni wakristu na pia serikali ya Tanganyika inaongozwa kimsalaba salaba na wala haiwatendei haki Waislam. Hata nzi husema ukiujua huu,mwengine huujui. Wacha jazba zenye lengo la mizozo na kuisambaratisha serikali yetu njema ya nchi ya Zanzibar ya Umoja wa kitaifa sisi ndio tuilioichagua na kwa kweli wenyewe tupo macho kwa hujuma na njama zozote zile zinazopangwa dhidi ya Serikali yetu Tukufu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s