Msitosheke na elimu ya vyeti

Mwandishi Mwandamizi na Mratibu wa wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Shifaa Said Hassan akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari juu ya kuongeza elimu kwa waandishi wa habari pembeni kwake ni Khatib Mjaja Mshauri wa Radio Jamii ya Micheweni Pemba

Wahitimu wa Chuo Cha Mwenge (MCC) cha Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi wameshauriwa kutotosheka na kiwango cha elimu walichofikia na waitumie fursa hio kama ngazi ya kujiendeleza zaidi.

Ushauri huo ulitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi katika Mahafali ya Pili ya Chuo hicho cha CCM Mkoa Mjini Magharibi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa Amani.

Alisema kuwa elimu haina mwisho kandri watakavyojifunza ndipo watapopata maendeleo zaidi, hivyo aliwataka wajiandae kwa mafunzo ya Diploma yanayotarajiwa kuanza hapo baadaye.

Halikadhalika alikipongeza Chama cha CCM Mkoa wa mjini kwa kubuni mradi huo ambao ni pekee katika Mikoa yote nchini ambao utasaidia sana kupunguza wimbi la vijana wazururaji mitaani.

Kuhusu Muungano Mhe Balozi Seif Iddi alisema Chama cha CCM kitaendelea kuimarisha Muungano ili udumu milele kama kilivyourithi kutoka katika vyama vya TANU na ASP.

Alieleza kuwa hivi karibuni kumejitokeza watu wachache wanaotumia mbinu mbali mbali zikiwemo za dini kuupiga vita muungano wa Tanzania, lakini alisema hawatofanikiwam kuuvunja.

Kabla ya hapo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Green Valley ya Arusha Ndg Yahaya A. Mtarita aliahidi kuwapatia ajira wahitimu watano kutoka katika Chuo hicho mwaka huu kwa lengo kudumisha uhusiano wao.

Vile vile Mkuu wa Chuo Cha Uwandishi wa Habari (DSJ) Ndg JOACHIM Rupepo alieleza hatua iliofikiwa katika kuimarisha mahusiano yao baina ya Chuo chake na Chuo cha MCC likiwemo suala la kuanzisha Diploma ya Uwandishi wa Habari chuoni hapo.

Naye mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Seif Iddi alikabidhi Track suit 60 kwa wanafunzi wataoshiriki mashindano Mkoani Arusha na aliwataka wahitimu wajitume kwa kutumia ujuzi walioupata na wasisubiri ajira za Seriklini pekee.

Jumla ya Wahitimu 53 walikabidhiwa vyeti vyao vya kufuzu masomo yao wakiwemo wa fani tano zinazosomeshwa Chuoni hapo ambazo ni Uwandishi wa habari, Ushoni, Umeme, Afya na Komputa.

Mapma Mhe Makamu huyo wa Pili wa Rais alitembezwa kuangalia kazi mbali mbali za wanafuzni hao na kutumbuizwa kwa ngoma utenzi na mchezo wa kuigiza

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s