G 15 wasema Muungano ni batil

Makamu Mwenyekiti wa G 15 Rashid Yusuf Mshenga akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari (MAELEZO) Zanzibar jana, amesema kuwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar hauna uhalali kwa kuwa Zanzibar hawakupewa mkataba wa Muungano huo pembeni kwake ni Rashid Hemed Rashid (Joe) Makamu Mwenyekiti wa chama cha NLD Zanzibar.

Advertisements

3 responses to “G 15 wasema Muungano ni batil

  1. Muungano una faida na hasara,kwa upande wa Zanzibar hainufaiki na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani si tu inanyimwa haki zake nyingi za kimsingi lakini pia inanyanyaswa na kukandamizwa ni Tanganyika. Ikumbukwe wazi kuwa licha ya udogo ulionao Zanzibar ni nchi huru na Muungano unaoendeshwa kwa misingi batili hauna maana kwa Zanzibar naona upo upo tu kuwanufaisha Watanganyika. Wito unatolewa ili kuunusuru Muungano huo,’Vijana wa Kizanzibari tumechoshwa na mgawanyiko usio sawa wa mapato, fursa, maliasili, misaada, madaraka na mambo kadha wa kadha ya Muungano unaoendeshwa kwa njia zisizo halali wala za kisheria kama vile kuongezwa vipengele vingi ambavyo ni batili na haramu. Ziundwe Tume huru zinazokubalika na wananchi kutoka pande zote mbili, tume ambazo zitachukuwa maoni kutoka kwa wananchi na maoni hayo yalinganishwe na vipengele vya mwanzo vya Muungano wa kwanza na iundwe katiba mpya kwa kushirikisha pande zote mbili na kwa kuzingatia makundi mbali mbali ya wananchi wa nchi zote mbili(Zanzibar na Tanganyika) ili kushughulia hayo kutoka Zanzibara na Zanzibar na watu wakae chini vyenginevyo Muungano utaendelea kuwa wa haramu na wa batili na hakuna atakayeweza kustahamilia hili labda Mtanganyika kwa sababu wananufaika na Muungano hewa lakini sisi Wazanzibar tuna rikodi zote kuwa yale tunayofanyiwa ni Tanganyika au kama hii ni kwa sababu ‘Mchuma janga hula na wa kwao’ sawa lakini pia ‘Mchwa anapokaribia kuangamizwa huoteshwa mbawa mbili’ akajiona anaruka na kwenda atakapo lakini husahau kuwa mwisho wake unakaribia.

  2. Jee huo mkataba wa muungano waliopewa bara umeandikwa nini? na jee iwapo bara wana mkataba ule tunaotegemea sisi ni photocopy ya huo wa bara au sisi tulitakiwa tuwe na wa kwetu tofauti? na ni mamlaka ipi ilipaswa kutoa huo mkataba? naomba kwa nia njema kabisa wanaofahamu watuelekeze baadhi yetu ambao hatufahamu

  3. Ili kuepusha migagaisho au sintofahamu katika suala la Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ni bora kuundwe serikali tatu( serikali ya Zanzibar,serikali ya Tanganyika na serikali ya Muungano) hili ni jepesi na linawezekana au kama hili ni gumu na haliwezekani Muungano uvunjwe kama vile ilivyokuwa kabla ya mwaka 1964 Muungano kati ya nchi hizi mbili huru (Zanzibar na Tanganyika) haukuwepo wala haikuwa chochote bali nchi ya Zanzibar ndipo ilipopiga hatua kubwa zaidi,kisiasa ,kijamii, kiuchumi na hata kiutamaduni hadi kufikia ndiyo kitovu na kituo cha kibiashara Afrika Mashariki,leo hii ni kinyume chake Zanzibar ni ya mwisho kwa kila kitu. Ni akili ya Mzanzibar gani isiyoweza kufikiria juu ya suala kama hili?. Ni haki ya kila mtu kufikiri na mimi kwa upande wangu nimetoa mawazo yangu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s