Muungano utadumu kwa michezo

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fatma Mohammed Said, amewataka wanamichezo wa ofisi mbili hizo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, kuitumia michezo kama ni njia moja wapo ya kuleta ushirikiano, upendo, udugu pamoja na kudumisha Muungano baina ya pande mbili hizo.

Hayo aliyaeleza katika hafla ya uzinduzi wa Tamsaha la michezo kwa ofisi hizo uliofanyika viwanja vya Chuo cha Afya Mbweni wilaya ya Magharibi Unguja.

Amesema kuwa kimsingi michezo ni njia moja ya kuleta maelewano na sio ugomvi na waichukulie michezo hiyo kwa malengo hayo na si kwa ajili ya kupata kikombe au zawadi katika michezo hiyo.

“kinyume na hilo basi hatutaweza kwenda sambamba na lengo letu hili tulilokusudia na badala yake tutajenga uhasama miongoni mwetu”, alisema.

Nae Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Selina Lymo amewataka wanamichezo hao kuzingatia, sheria, kanuni na taratibu za michezo ili waendelee kujenga mashirikiano waliokuwa nayo.

Mapema katibu Msaidizi wa timu ya Soka ya Ukaguzi alisema kuwa umoja na mshikamano walionao baina ya taasisi mbili hizo utazidi kuendelezwa ili kuwa mfano mzuri kwa wafanyakazi watakaofatia baada yao.

Katika uzinduzi huo ambao ulitanguliwa na maandamano ya wanamichezo, timu ya Soka ya Ukaguzi ya Zanzibar ilishinda kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya wageni wao Ukaguzi kutoka Tanzania Bara.

Mabao ya Ukaguzi yaliweza kuwekwa kimiyani na wachezaji Haji Mohammed katika dakika ya 20 na Hakim Khamis dakika ya 48.

Katika hatua nyengine timu ya soka ya Wizara ya Fedha inaendelea kugawa pointi za bure kwa wapinzani wake, baada ya hapo juzi kushindwa kuhudhuria uwanjani, katika mchezo uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Amaani Nje kati yao na timu ya Red Cross, ikiwa ni michuano ya Kombe la Siku ya wafanyakazi.

Timu hiyo ambayo siku tatu tu ilionesha vioja baada ya kususia kucheza mchezo kati ya na timu ya Ardhi kwa kisingizio cha kuwa wapinzani wao hao walichezesha wacheaji wengi akiwa ni Mamluki.

Kutokana na hali hiyo timu ya Red Cross imeweza kujizolea pointi hizo bila ya kutoka jasho, huku wakiwa ndio mara yao ya kwanza wakiweza kupata pointi baada ya kufungwa katika michezo yao miwili waliocheza kwenye mashindano hayo, mchezo ambao ulipangwa kuchezwa wakati wa saa 10:00 za jioni..

Mbali na mchezo huo pia kiwanjani hapo kulipangwa kuchezwa mchezo kati ya timu ya Uhamiaji na Zimamoto lakini ulishindwa kuchezwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hapo juzi katika majira ya mchana.

Aidha timu ya Baraza la Wawakilishi nayo imeonja utamu baada ya kushinda mchezo wake na Wizara ya habari kwa kuwafunga kwa tabu bao 1-0, ambalo lilifungwa na Ali Khamis katika dakika ya 70.

Michezo hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo wakati Zimamoto itapambana na timu ya Baraza la Wawakilishi wakati wa saa 3:00 katika uwanja wa Maotze Tung, huku KMKM Veteran ikicheza na Red Cross saa 8:00 mchana katika uwanja wa Amaani nje na Ikulu na Habari wakicheza wakati wa saa 10:00.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s