Michezo hujenga afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wanamichezo wa Timu za Ikulu ya Zanzibar na Ikulu ya Dar es Salaam,wakati timu hizo zilipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais katika kusherehekea PASAKA utamaduni wa timu za michezo kufanyika Zanzibar na Tanzania bara ni wa muda mrefu ukiwa na lengo la kudumisha mashirikiano katika ya nchi mbili hizo.

MICHEZO hujenga afya pamoja na uhusiano na mashirikiano mema katika jamii hivyo hatua ya kutembeleana kimechezo kati ya wanamichezo wa Afisi ya Rais Ikulu Dar-es-Salaam na wanamichezo wa Ikulu ya Zanzibar kutazidi kujenga uhusiano kimichezo na kikazi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na wanamichezo kutoka Ikulu ya Dar-es-Salaam na wale wa Ikulu ya Zanzibar,ikiwa ni miongoni mwa kuendeleza utamaduni wa kutembeleana kimichezo katika skukuu ya Pasaka.

Dk. Shein alisema kuwa michezo hujenga afya na ustawi wa jamii pamoja na maelewano mazuri katika jamii hatua ambayo hupelekea kujuana kwa kupitia michezo.

Alisema kuwa michezo huanza kuleta udugu na uhusiano tokea utotoni hali ambayo hupia, hujenga maelewano na watu walio wengi ndani na nje ya jamii unayoishi.

Dk. Shein alisema kuwa michezo hii ya kutembeleana baina ya wanamichezo wa Tanzania Bara na Zanzibar iliyoanzishwa na wazee wetu ilikuwa na lengo la kujenga udugu na maelewano zaidi baina ya wanamichezo wa pande mbili hizo.

Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza na kudumisha uhusiano huo kwa lengo la kujenga zaidi udugu na maelewano kama ilivyokuwa lengo la wazee na waasisi wa pande hizo mbili.

Dk. Shein pia, aliwasisitiza wanamichezo hao kuwa uhusiano wa kimichezo wauendeleze hata katika shughuli zao za kazi hali ambayo itasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Aidha, Dk. Shein aliwataka wanamichezo kutoka Tanzania Bara kuitumia vizuri nafasi hiyo katika michezo kuijua zaidi Zanzibar pamoja na kujua namna ya watu wake wanavyoishi na kuwasisitiza kuendelea kuja kuitembelea Zanzibar.”Zanzibar njema atakae aje”,alisema Dk. Shein.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa michezo yote ina msisimko hivyo aliwataka wanamichezo hao kucheza michezo yao kwa upendo na maelewano ili lengo la michezo hiyo liweze kufikiwa”Mimi sijacheza bao siku nyingi lakini nikipata tobwe nitamfunga”,alisema Dk. Shein.

Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na wanamichezo hao alieleza historia fupi ya Dk. Shein katika michezo na kueleza kuwa ni miongoni mwa viongozi wanamichezo na wanaopenda michezo kwani ana historia kubwa kimichezo hapa Zanzibar.

Akieleza juu ya upendo wa michezo kwa viongozi wakuu wa hapa nchini Dk. Makame alimtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa naye ni mpezi mkubwa na mpenda michezo kwa kiasi kikubwa hivyo anamatumaini makubwa kuwa uhusiano huo wa kimichezo kwa pande zote mbili utaimarishwa zaidi.

Nae Mwenyekiti wa Michezo Ikulu Zanzibar Abduli Mpechi alisema kuwa uhusiano wa kimichezo uliopo kati ya wanamichezo wa Ikulu ya Dar-es-Salaam na Ikulu ya Zanzibar umeweza kuleta mafanikio makubwa.

Alisema kuwa katika ziara ya wanamichezo hao wa Ikulu Dar-es-Salaam hapa Zanzibar watashindana katika michezo mbali mbali ambapo leo hii kutakuwa na bonanza litakalohusishwa michezo mbali mbali ukiwemo mpira wa miguu, mbio za kufukuza kuku, mpira wa pete na mbio za magunia ambapo michezo yote hiyo itafanyiia katika viwanja vya Polisi Bomani, mjini Unguja.

Naibu Katibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Bwana Shaaban Gurumo akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wanamichezo na wafanyakazi wote wa Ikulu alitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi.

Aidha, katika maelezo yake Ngurumo alitoa shukurani kwa Dk. Shein kwa makaribisho yake na kusisitiza kuwa katika michezo yote watakayocheza watahakikisha wanacheza kwa upendo mkubwa kwani lengo zaidi ni kuzish uhusino na ushirikiano mwema.

Pamoja na hayo, Ngurumo alisema kuwa licha ya ziara hizo za kimichezo kwa Ikulu za Dar-es-Salaam na Zanzibar hazikuanza muda mrefu lakini pamekuwa na mashirikiano na mahusiano pamoja na upendo wa hali ya juu kati ya wafanyakazi na wanamichezo wa pande hizo mbili ambao aliahidi kuendelezwa zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s