Zanzibar anzisheni baraza lenu

Ali Rashid ni Mwandishi wa habari wa siku nyingi na pia mshauri wa waandishi hapa Zanzibar, akitoa mada katika mkutano wa waandishi wa habari na wadau wa habari uliotayarishwa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa mataifa (UNDP) kutathimini kazi za waandishi wakati wa uchaguzi iwapo muongozo uliowekwa na wadau hao umefanikiwa kwa kiasi gani na iwapo kuna upungufu uliofanyika kwa upande wa Zanzibar

WAANDISHI wa habari Zanzibar wameambiwa wanayo nafasi ya kuanzisha Baraza la Habari la Zanzibar linalojitegemea nje ya Baraza la Habari Tanzania (MCT).Ali Rashid ambaye ni Mwandishi wa habari wa siku nyingi na pia mshauri wa waandishi hapa Zanzibar, alisema kinachotakiwa ni kuwepo kwa wanataaluma ya habari wanaotaka kuwa na chombo hicho visiwani Zanzibar licha ya kuwa baraza la habari la Tanzania kufanya kazi zake hapa nchini.

Rashid alitoa tamko hilo katika semina iliyowashirikisha waandishi wa habari na wadau wa siasa na wanaharakati wa taasisi za kiraia kutathimini utendaji wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 visiwani humo.

Alisema mpaka sasa hakuna kikwazo kinachoweza kuwazuia waandishi wa habari na wadau wengine kuanzisha na kushiriki katika uendeshaji wa baraza hilo ikiwa wataamua wenyewe kufanya hivyo hasa kwa kuwa tayari sheria ipo wazi katika uanzishwaji wake.

“Naamini wakiwepo watu wanaotaka kuanzisha Zanzibar Media Council (ZMC), wanaweza kufanya hivyo, japokuwa huduma za MCT zipo Zanzibar na zinafanya kazi zake lakini na haki hiyo ipo pia” alisema Rashid wakati wa mkutano wa wadau wa habari huko Ocean View Hoteli.

Mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo katika semina hiyo, Dadi Kombo Maalim alisema baadhi ya ripoti juu ya utekelezaji wa mwongozo wa uandishi wa habari zinaonyesha kulikuwa na kulikuwa na uikukaji mkubwa wa maadili, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na MCT dhidi ya mwenendo huo.

Wasiwasi wa Dadi ulikuja baada ya Mratibu wa mpango wa kuwezesha uchaguzi unaothaminiwa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa mataifa (UNDP) Sebastian Sanga kuwaeleza washiriki wa semina hiyo mambo kadhaa yaliyojitokeza katika baadhi ya vyombo vya habari wakati wa kuandika matukio ya uchaguzi huo.

Alisema mambo hayo ni pamoja na uandishi wa habari kwa ushabiki na kutoa mfano, wa vichwa vya habari kadhaa vilivyojitokeza magazetini kikiwemo kilichosomeka: “Nilitaka Sitta ashindwe, nisichokitaka ni tabia yake ya uropokaji.”

Vichwa vingine vilivyoonyesha ukiukwaji wa mwongozo wa uandishi wa habari za uchaguzi huo, Sanga alisema ni kile kilichoasomeka: “Ahadi za Dk. Slaa ni za wendawazi, kauli za CUF zinahatarisha amani Zanzibar na Maalim Seif ni mwongo.”

“Hii ina maana kwamba walikuwepo waandishi wa habari walioamua kuweka kando miiko ya taalima yao pembeni na kufuata mirengo ya kichama ,” alisema Sanga katika semina hiyo.

Katika hatua hiyo, sehemu kubwa ya washiriki walishauri MCT ipewe meno ili baada ya kubaini ukiukaji huo wa maadili baraza hilo liweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wneye kukiuka maadili ya kazi zao hasa wakati wa uchaguzi ambapo idadi kubwa ya vyombo vya habari na wahariri hufuata mirengo ya kivyama na kuacha maadili ya uandishi.

Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Salim Said Salim, alisema baadhi ya waandishi wa habari wa upande wa Tanzania bara wana uwelewa mdogo kuhusu masuala ya Zanzibar na hivyo wanapoandika wanashindwa kuipa nafasi Zanzibar na matokeo yake uchambuzi wa habari zao zinashindwa kuwa na mashiko na kukosa hoja za msingi.

Alisema matokeo ya kuandika habari za aina hiyo zisizokuwa na ujuzi wengi wao wanaandika matukio ya Zanzibar, hasa yale ya wakati wa uchaguzi bila kuyafanyia utafiti na kusababisha upotoshaji mkubwa kwa wananchi kutokana na kutojituma.

Alisema ni jambo zuri kwa waandishi wa habari wanapoandika habari zao kuwa na uhakika wa jambo na kuandika ukweli na kuacha tabia ya kuwasikiliza viongozi wa kisiasa ambao huwa wanawatumia na baadae kuwaacha baada ya kumalizika uchaguzi.

Advertisements

2 responses to “Zanzibar anzisheni baraza lenu

  1. Hii ZMC itawapa waandishi wetu wa habari (Zanzibar) uhuru zaidi wakujiona nao ni Nchi kamili kama hiyo Tanganyika. Na kupanuka kielimu na kimawazo, Zanzibar ilikuwa na Magazeti yake mazuri na Waandishi wazuri tu wa habari . Lakini tatizo ni kwamba hakuna Freedom of Speeach. Sasa hii ZMC itawapatia Freedom of Speach

    Ni jambo zuri sana.

  2. Pingback: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar·

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s