Hivi gamba la CCM kweli limevuka?

Ally Saleh ni Mwandishi Mwandamizi na Mtangazaji wa BBC anasema, Mwenyekiti wake wa kwanza Julius Nyerere, aliye wahi pia kuwa Rais wa Tanzania alishaonyesha dalili ya kuchakaa kwa CCM na kubashiri kuwa inaweza kukosa nguvu za kutawala kama haijabadilika.

Tumesikia mengi wiki iliyopita kuhusiana na Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachotutawala hapa nchini, Zanzibar na Tanzania kwa jumla bda ya ushindi wake wa mwaka jana tu.Chama hiki wiki hiyo iliyopita kilifanya mabadiliko makubwa ya ndani ambayo yamepelekea kujiuzulu taasisi mbili kubwa za ndani na kusaidia kuuna upya tasisis hizo ambazo zilikuwa na majukumu makubwa ndani ya chama hicho kikongwe kabisa nchini.

Tumeona kuwa katika taasisi hizo za ndani sura nyingi mpya zimeingia lakini wengi wakiwa ni wanachama ambao ni vijana kidogo na waliokuwa mstari wa mbele na maarufu toka mwanzo kwa kiasi fulani.
Kwa maneno mengine uundaji mpya wa taasisi hizo za ndani umewasogeza watu ambao tokea hapo baadhi yetu tulikuwa tukiwafikiria wangekuwapo hapo mbele lakini ukiritimba na ukongwe wa chama ulishindwa kutoa nafasi kwao.
Na hili ndilo ambalo limekuwa tatizo la chama hiki ambacho kina mitizamo hadi leo kuwa ni chama kilicholeta ukombozi, japo sicho moja kwa moja, na kwa hivyo fikra ya kukaa katika chama mpaka mtu afie humo inakitawal.
Kila mtu anjua kuwa kelele za kufanya mabadiliko ndani ya chama hicho si za leo wala jana na aliyekuwa akiliengwa wazi wazi alikuwa ni Katibu Mkuu Yussuf Makamba na timu yake ya Serkretarieti, ambayo kawaida hutakiwa iwe ni moyo au mashine ya chama chochote kile.
Tunajua majibu ya Makamba kuhusu kuondoka kwake ili chama kijipange upya, kije na fikra mpya, kije na mikakati ya kisasa yalivyokuwa nab ado chama kilikaaa kimya na kikaingia katika uchaguzi katika hali hiyo ya kuwa kinakosa nguvu, lakini kina fedha na uzoefu na kinashika dola na kwa hivyo nguvu.
Ilionekana wazi kuwa mtindo wa mtu kujiona mkubwa kuliko chama ulikuwa umesaki ndani ya mfumo wa CCM kwa kuwa hakuwa Makamba tu aliyepungukiwa na dira ya kuwa kiongozi, lakini wengine mbali mbali, ila kila mmoja alishikilia alipoweza kubaki uongozini.
Tulishuhduida CCM ikiteua tume kufuatilia mambo kadhaa ndani ya chama hicho kuhusiana na muundano, shutuma za kupoteza itikadi na pia kupungua mvuto wake jambo ambalo kila mtu anajua kuwa lilikuwa katika manada na chama hicho kuwa hatarini kupoteza sifa yake na uwezo wake na kwa hivyo hatarini kukosa utawala.
CCM ilijichukulia kwa ujumla tu kuwa bado ni chama imara, kinachopendwa na ambacho hata ndoto ya kuwa kitapata upinzani haikuwepo kabisa na imekuwa na kauli za kuashiria kuwa itatawala nchi hii milele.
CCM pia kwa sababu za kihistoria iliwahi hata kuwa na kauli kuwa ni chama peke yake ambacho kinaweza kuongoza nchi hii na kwa njia ya amani ingawa huko nyuma Mwenyekiti wake wa kwanza Julius Nyerere, aliye wahi pia kuwa Rais wa Tanzania alishaonyesha dalili ya kuchakaa kwa CCM na kubashiri kuwa inaweza kukosa nguvu za kutawala kama haijabadilika.
Lakini kulikuwa kuna vitu vinavyoipa jeuri CCM mojawapo ni ukubwa wa chama hicho, pili kule kutangulia kuwa madarakani na kwa hivyo kuumiliki mfumo wa utawala, tatu ni kule kuwa na rasilmali na uwezo mkubwa wa kifedha unaotokana na vyanzo mbali mbali.
Kwa hivyo katika hali hiyo CCM ikajiachia. Ikaanza kuwa ni chama kinachokimbia kidogo kidogo wanachama wake, chama ambacho kidogo kidogo kikkaanza kuwa ni cha matajiri, chama ambacho kidogo kidogo kikaanza kuwa cha makundi na chama ambacho kidogo kidogo kikaanza kuwa kinachopoteza itikadi lakini hata baadhi ya misingi yake mikuu.
Serikali ambazo CCM imekuwa ikizinogoza zikaanza kuwa regerege, zenye madai makubwa ya rushwa, zenye madai kibao ya ufisadi, zenye kupoteza uzalendo wan chi hii na zenye kujenga matabaka ambapo wenye nachona wasio nacho wakazalishwa kwa wingi na umasikini ukatamalaki kinyume na neema ambayo wana nchi waliitarajia seuze kuwepo kwa maisha boara kwa kila Mtanzania.
Kwa hivyo kwa fikra zangu ni kwamba CCM ilikuwa na gamba kwa muda mrefu lakini haikutaka kujivua kwa kuwa haikupata msukosuko wowote ule wa kuitisha kuiondosha madarakani.
Gamba ambalo linasifiwa kwa mbwembwe leo kuwa limevuliwa, kwa kweli ni moja tu ya magamba mengi ambayo CCM imejivua lakini bdo ina magamba mengine kadhaa ya kujivua hadi irudi katika hali ambayo tungeitarajia kwa chama kikubwa, makini na chenye uzoefu kama hicho.
Pengine wengine wanasema gamba linalovuliwa leo lilikuwa livuliwe tokea mfumo wa vyama vingi ulipokuja ambapo CCM ilitiwa kishindo cha kuondoshwa madarakani. Lakini tunajua jinsi NCCR ilivyosambaratishwa wakati ilipojitokeza kuwa tishio mwaka 1995.
Tunajua jinsi ambavyo CUF ilivyopigwa vita ilipoanza kwua tishio Bara lakini pia kuwa mbadala halisi wa CCM kwa upande wa uongozi wa kiserikali hapa Zanzibar. Uchakachuaji wa matokeo ya Zanzibar hautaki kuhadithiwa upya.
Kwa mawazo yangu uvuaji wa gamba unaodaiwa CCM kuufanya unatokana na kupata mshtuko mkubwa katika uUchaguzi Mkuu wa mwaka jana ambapo kulikuwa na nafasi kubwa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuchukua madaraka.
Kwa madhumuni ya makala hii sina haja ya kwenda kwenye mdai ya uchakachuaji au idadi ya kura ya chama hiki au kile au kukosekana uwazi au kubanwa chama hiki au kile, lakini nataka niamini kuwa kama kulikwua na wakati CCM ilioona tonge inawatoka Tanzania Bara ilikuwa ni mwaka jana.
Naamini hilo gamba kuvuliwa linatokana na mshtuko huo. Leo tunasikia CCM wakisema kuwa kimepoteza kura za Urais na kupokonywa majimbo kwa kuwa wananchi wanaawaadabisha kwa kutokuwa wasikivu wa vilio vyao. Lakini kweli hwakuwa wakivisikia, kitu ganikiliwafanya wawe na jeuri ya kutovisikiliza?
Kwa hivyo dhana inayojengwa ni kuwa gamba likishavuliwa basi chama kitarudi katika hali yake halisi na kwa hivyo kitaanza kujipanga kiitikadi, kimsingi, kimiundo na hata kiutekleezaji na hivyo kitarudisha mvuto na mapenzi yake kwa umma na wapiga kura.
Hiyo inaweza kuwakweli na pia isiwe kweli. Sio watu wote wnaoweza kuridsha mioyo yao iwapo wamesalitiwa, wameongopewa na wamefanywa ni takwimu tu ndani ya nchi yao na sio wanachama u rais wenye haki, usawa na kueza kuishi maisha yanayo wastahili.
Itategmeea mambo mengi CCM kuweza kurudisha wanachama iliowapoteza huko Bara kwa CHADEMA kama ambavyo tumeona CCM kushindwa kurusisha wanachama wake iliyokuwa imewapoteza hapa Zanzibar na mifano kama hiyo ikiwa nchi zilizopita mchakato kama wa CCM Barani Afrika.
Itategemea sana wanachama na wananchikuamini kwamba nikweli gamba limevuliw? Na jee kwa muda ambao CCM ilikuwa katika “kujisahau” kulikuwa kumeota gamba moja tu? Na jee baada ya gamba hilo ni rahisi kiasi gani kurudi katika uhalisi wa kichama?
Ninavyoamini kuna kazi kubwa sana ya kufanywa na CCM na ikijua kwamba huku yenyewe ikijinadi kuwa imevua gamba, chama pinzani cha CHADEMA kilicho shndikiza CCM kufikia hapa nacho kinajenga hoja kuwa gamba liko pale pale na kwa kweli hasa linazidi kuwa gumu na la hasara zaidi kwa Watanzania.
Maana kwa hakika kujivua gamba ni dhana tu, ukweli ni matendo. Jee CCM itakuwa na ukweli wa matendo? Na umma utaamini maana Waswahili husema Ukitafunwa na Nyoka Unaogopa Ungo’go. Kama muda wote CCM ilipigiwa kelele ikajitia haisikii, jee kwa nini iaminiwe tena haitafanya gamba jengine?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s