FAO ni wenzetu sana

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania Dr. Luise L. Setshwaelo aliyefika Ofisini Vuga kuagana na Balozi Seif baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi amesema Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) ni Taasisi muhimu sana katika maendeleo ya jamii duniani.

Makamu wa Pili wa Rais aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania Dr. Luise L. Setshwaelo aliyefika Ofisini Vuga kuagana naye baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

Alisema FAO ni Shirika linalogusa maisha ya watu wengi duniani hususan ikitiliwa maanani umuhimu wa chakula katika maisha ya mwanadamu.

Alieleza shukrani zake kwa misaada mbali mbali iliyotolewa na inayoendelea kutolewa na Shirika hilo kwa muda wote na kuomba misaada zaidi kwa kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Balozi Iddi aliahidi kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa kila msaada katika kufanikisha shughuli za Shirika hilo hapa nchini.

Naye Dr. Setshwaelo alisema Tanzania ni moja wapo ya nchi zenye umuhimu mkubwa na uhusiano mzuri na Shirika hilo.

Alieleza kufarijika kwake kwa kuanza harakati za Mpango wa usalama wa chakula visiwani Zanzibar na kusema umeacha kumbukumbu nzuri wa muda wake hapa nchini.

Alisema Zanzibar na watu wake ni nzuri na anategemea kuwa ataletwa mtu mzuri kuchukua nafasi yake kwa haraka iwezekanavyo. Dr. Setshwaelo ameshafanyakazi Tanzania kwa muda wa miaka sita na nusu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s