Asilimia 80 hawana Bima

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi za mamalaka ya usimamizi wa Bima Tawi la Zanzibar,wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la mamlaka hiyo jana huko Kilimani Mjini Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee,(kulia)Kamishna Mkuu Isarael L.Kamuzora na Mwenyekiti wa Bodi Prof Mgongo Fimbo.

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein amesema changomoto kubwa kwa makapuni ya bima ni kuelekeza juhudi zake katika kueneza huduma za sekta hiyo vijijini.Alisema kwa sasa huduma hiyo imebaki kuwanufaisha watu wachache na kuwaacha sehemu kubwa ya asilimia 80 ya wanaoishi vijijini bila kunufaika na huduma hiyo.

Rais Shein alikuwa anazungumza baada ya kufungua jendo la ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Zanzibar ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya jumla ya shilingi milioni 325 mjini Zanzibar.

“Katika hali ya sasa ni watu wachache sana wa vijijini wananufaika na huduma mbali mbali za bima wakati wale wa mijini wanatumia huduma hiyo hata kwa huduma za elimu kwa watoto wao,” alisema Dk Shein.

Shein aidha ametoa wito kwa makampuni ya bima kufanya bidii zaidi katika kueneza huduma zao kwa wananchi hasa wanaoishi vijini pamoja na kutoa elimu ya bima kwa jamii.

Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye ukumbi wa hoteli ya Ocean View,mara baada ya kulifungua jengo la Mamlaka ya Bima, Zanzibar huko Kilimani mjini Zanzibar.

Katika hotuba yake hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa ni wazi kwamba kwa upande wa mijini, wafanyabiashara wengi wenye viwanda wanajilinda kwa kuchukua bima hivyo ipo haja kuwalenga wananchi wa vijini ili nao wapate kunufaika sanjari na kupata elimu ya bima.

Alisema kuwa mkulima na mfugaji ambao ndio wahimili wakuu wa uchumi nchini, hawana hifadhi ya mali zao panapotokea janga kama ukame au mafuriko pamoja na madhara makubwa au kupoteza maisha yao na kusisitiza kuwa hayo ndio masuala ya kuyafanyia kazi.

Dk. Shein alisema kuwa takwimu za watu hapa Zanzibar na Tanzania Bara zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wananchi, hasa wanaoishi vijijini hawafikiwi na huduma za bima .”Hili ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa uzito na umuhimu wake mkubwa”,alisema Dk. Shein.

Rais Dk. Shein alisema kuwa asilimia ndogo ya wananchi ndio wanaofaidika na bima ya elimu ya watoto wao, afya za jamii na pia, ulinzi wa mali zao.

Aidha, Dk. Sherin alisema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinatambua thamani na umuhimu wa sekta ya bima katika maendeleo ya nchi na kutokana na sababu hiyo ndio maana Serikali ya Jamuhuri ya Muungano iliunda Shirika la Bima la Taifa.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa kutokana na mageuzi ya uchumi, nafasi zilitolewa kwa sekta binafsi nayo kuanzisha mashirika ya shughuli za bima mnamo mwaka 1997 ambapo kuanzia hapo makampuni ya bima yaliongezeka kuanzia mawili na hadi hivi sasa kufikia 27.

Pamoja na mafanikio hayo pia, Dk. Shein alizitaja changamoto kubwa katika sekta hiyo ambapo miongoni mwa changamoto hizo ni kufikisha huduma zake katika sehemu zote za taifa.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alisema kuwa wataalamu katika fani ya bima ni wachache hivyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inashughulikia jambo hilo na siku chache zilizopita kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanzisha mafunzo ya bima hapa Zanzibar.

Akinukuu Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 Dk. Shein alisema “Kuendelea kuwahamasisha wananchi ili waone umuhimu wa kujiunga na huduma za bima mbali mbali ili zitumike pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kukuza uwekezaji katika uchumi”.

Mapema akimkaribisha Rais wa Zanzibar kutoa huduma baye, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee, naye alisisitiza haja ya kutoa elimu kwa jamii hasa vijijini.

Alisema kuwa Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Bima Nchini Tanzania, imeanzishwa mwezi Julai mwaka 2010 chini ya kifungu aamba 5 cha Sheria ya Bima ya namba 10 ya mwaka 2009, hiyo ni baada ya kuona haja ya kuwepo msimamizi mkuu wa shughuli za bima nchini.

Waziri Mzee alisema kuwa Bodi ya Taifa ya ilinunua jengo hilo kutoka Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), ambapo limefanyiwa matengenezo ya kugeuzwa kuwa afisi na kugharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania milioni 325,885,538.

Aidha, Waziri Mzee alisema kuwa utendaji wa soko la bima katika mwaka 2010 ulikuwa ni wa kuridhisha ambapo mauzo ya biashara ya bima za kawaida yaliongezeka kwa kiasi cha asilimia 21.6 kutoka shilingi Bilioni 209.6 mwaka 2009 hadi Bilioni 254.8 katika mwaka 2010.

Aliongeza kuwa mauzo ya biashara ya bima za maisha yaliongezeka kwa kiasi cha asilimia 41 kutoka shilingi Bilioni 21.7 mwaka 2009 hadi Bilioni 30.6 katika mwaka 2010.

Pia, alieleza kuwa jumla ya rasilimali za makampuni ya bima iliongezeka kwa kiasi cha asilimia 130 kutoka shilingi Bilioni 320.6 mwaka 2009 hadi Bilioni 362.3 mwaka 2010 ambapo mtaji wa makampuni ya bima uliongezeka kwa kiasi cha asilimia 7.6 kutoka shilingi Bilioni 101.6 katika mwaka 2009 hadi Bilioni 109.3 mwaka 2010.

Kwa upande wa uwekezaji Waziri Mzee alisema kuwa uwekezaji wa Makampuni ya Bima uliongezeka kwa kiasi cha asilimia 24.3 kutoka Shilingi Bilioni 204.8 mwaka 2009 hadi Bilioni 254.4 mwaka 2010 na kueleza kuwa mchango wa (ZIC) katika pato la Bima Kitaifa ni sawa na asilimia 5.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bima (TIRA) Profesa Gamaliel Mgongo Fimbo, alieleza kuwa jengo hilo limenunuliwa kutoa Shirika la Bila la Zanzibar (ZIC) kwa shilingi milioni 108 kwa ajili ya matumizi ya shughuli za usimamizi wa soko la Bima hapa Zanzibar.

Profesa Fimbo alisema kuwa Shirika la Bima la Zanzibar limeweza kufungua matawi yake Tanzania Bara katika miji yote mikubwa kwa lengo la kutunisha pato la Shirika hilo pamoja na pato la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika ufunguzi huo viongozi mbali mbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walihudhuria pia, ngoma za utamaduni zilitumbuiza katika ufunguzi huo.

Advertisements

2 responses to “Asilimia 80 hawana Bima

  1. bima ni biashara inayotegemea fedha za watu. wanaonufaika zaidi ni hayo mashirika ya bima kuliko wananchi wenyewe. nadhani hapa tunadanganyana tu tena kwa zanzibar hata sio katika utamaduni wetu. kuna wale wanaosema kimsingi kukata bima kwa ajili ya ajali, maisha, maradhi n.k ina walakin mkubwa na imani za kiislam.

    • hayo mamillioni muliyoyatumiya kurekebisha hilo jengo kwanini musinunuwe vitanda na madawa na kuiripeya ila hospitali yaa mnazi moja munakwenda kuleta bima ndio nini muwamalize znz sio kwa njia ya ulaghai mnasi moja chafuu inanuka na mashamba hakuna hata hospitali kisha nyinyi munanzisha bima au kwanini serekali isijenge jengo kubwa zaidi likawaweka vijana wanaotaka kuwacha kula unga (drugs)ili wakimaliza wawe na afya nzuri tuwe na vijana wakufanya kazi kwa nini hayo mamillioni musiyatumiye kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi munawawekeya jengo ooooh bima umeme mpaka leo hamujauweza munatuleteya bima hebu wacheni mambo ya kipumbavu na fanyeni mambo ya maana bima hiyo yenye kampuni ndio itakayo faidika ss wazanzibar watafaidika lini au ndio MZEE KARUME KAFA na wazanzibar pia nao wote wafee hakuna wa kuwatetea tena wala anaewajali tena bofulo mtu hawezi kununuwa unataka kumtiya kwenye madeni ya bima umalize kabisa thamira yanu nini???????????????????????????????

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s