Kawasheni mwenge

BENKI ya Biashara ya Taifa (NBC) Tawi la Zanzibar imeikabidhi ofisi ya Mkuu wa Wilaya hundi ya shilingi 1,500,000 kwa ajili ya kuchangia mchango wa kukimbiza mbio za mwenge.

BENKI ya Biashara ya Taifa (NBC) Tawi la Zanzibar imeikabidhi ofisi ya Mkuu wa Wilaya hundi ya shilingi 1,500,000 kwa ajili ya kuchangia mchango wa kukimbiza mbio za mwenge.

Makabidhiano ya hundi hiyo yalifanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo, ambapo Meneja wa Benki hiyo kwa Zanzibar Rajab Hamza alimkabidhi Mkuu wa wilaya Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiano hayo, Hamza alisema kuwa wameamuwa kutoa mchango huo, ili kuweza kusaidia juhudi za ofisi hizo za kuwasaidia wananchi kupitia miradi mbali mbali.

Alisema kuwa mara baada ya kuletewa taarifa za kuomba kuchangia mbio za mwenge walishauriana na kutoa uamuzi wa wa haraka hasa kwa kuzingatia benki yao imekuwa ikijishughulisha na shughuli zake nyingi za maendeleo na kusaidia masuala mbali mbali hapa Zanzibar.

Hamza alisema kutoa mchango huo ni moja ya kuwasaidia wananchi wake kusogeza maendeleo mbele nchini na kuahidi kusaidia zaidi masuala kama hayo kila itakapopatikana fursa ya kufaya hivyo.

“Benki yetu imekuwa ikijishughulisha sana na shughuli mbali mbali za kijamii, na hivi sasa tumekuwa tukijitahidi kusaidia miradi mbali mbali ya jamii kila mwaka ikiwa ni moja katika faida zetu tunazozipata kutoka katika shughuli zetu za biashara”, alisema.

Mkuu wa Wilaya hiyo Kanal Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa ofisi yake kupata msaada wa fedha unaofikia kima hicho na kusema kuwa kitendo chao cha kuwaopatia fedha hizo kimeonesha kujali juhudi maendeleo ya wananchi.

Aidha alitowa wito kwa wananchi wenye uwezo pamoja na wafanyabiashara kujitolea kuchangia mbio hizo, ili kuweza kukamilisha lengo la ofisi yake la kuendeleza maendeleo ya wananchi.

“Huu mwenge ni wetu sote, na kila mmoja anastahiki kuuchangia na kwa kudhihirisha hili natowa wito kwa wafanyabiashara wote pamoja na wananchi kupamba na kufanya uisafi wa mji siku hiyo ili kuonesha kwamba wanajali mbio hizo’, alisema.

Sambamba na hilo pia alitowa wito kwa mabenki mengine kuchangia mbio hizo kama walivyofanya benki hiyo ambayo haikujali wingi wala idadi ya fedha hizo.

Mbio za mwenge hufanyika kila mwaka mara moja ambapo katika wilaya ya mjini unatarajiwa kutembezwa Julai 2 na 3 katika maeneo yote ya mji huo pamoja na tasisi za Serikali.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s